mr clean
Member
- Jun 19, 2012
- 16
- 1
waziri wa afrika mashariki mh samweli sitta amehujumiwa na viongozi wa ccm tawi la kongowe na kata ya toangoma jimbo la kigamboni katika uzinduzi wa ofisi ya serkali ya mtaa wa kongowe uliofanyika tarehe 11/01/2014,katika sherehe hiyo ambayo Waziri Sitta alikuwa Mgeni rasmi uongozozi wa CCM tawi la kongowe na kata ya toangoma ulisusia sherehe hizo kwa madai MH sitta alialikwa na mwenyekiti wa mtaa huo Ndg Matugula pasipo kufuata taratibu za kichama
hata hivyo baada ya kufanyika uchunguzi toka kwa wanaccm wenyewe ni kwamba viongozi wa ccm wilaya ya temeke waliwazuia viongozi wa kata na tawi wasishiriki katika sherehe hiyo kwa kuwa uongozi wa wilaya unamuunga mkono LOWASA na kwamba kufanya hivyo ni kusaliti Mh Lowasa.katika kutekeleza hujuma hii viongozi hawa wa chama kata ya toangoma na tawi la kongowe waliahidi katika kikao cha maandalizi kuwa watatoa muziki,viti na maturubai lakini mpaka siku ya tukio wakaingia mitini ili kumwaibisha Mh Sitta na mwenyekiti wa mtaa,jambo lililomlazimu mwenyekiti huyu wa mtaa kuomba msaada kwa viongozi wa chadema aliowaalika katika sherehe hiyo na ndiyo waliomsaidia kupata mahitaji waliyogoma kutoa na ndipo sherehe ikafanyika.hata hivyo inadaiwa kuwa viongozi wa ccm tawi la kongowe wamaemtenga mwenyekiti wao wa mtaa kwa sababu hawagawii mapato ya mtaa kwenye chama jambo linalowaudhi.pia wanamshutumu mwenyekiti huyu wa mtaa kwa kupokea michango mingi ya wanachadema ambayo kwa kiasi kikubwa imejenga ofisi hiyo na kwamba anawasikiliza sana viongozo wa chadema kuliko wa ccm kana kwamba chama chao ndicho kinachotawala.mmoja wa mtu wa karibu na viongozi wa ccm alisema,mwenyekiti huyu haelewani na viongozi wake wa ccm kata kwa kuwa aliiangusha kambi ya diwani Mh mikuki wakati wa uchaguzi wa baraza la katiba la wilaya kwa kumpitisha mtu wa chadema na kuwabwaga viongozi wa chama hicho akiwemo katibu wa kata hiyo.kama haitoshi walihujumu mpaka chakula na kupika kibichi na mwisho wa picha viongozi wa ccm wakaiba mchele kilo 30 zilizosalia na mafuta lita 20,wakasepa nayo.
mpka sherehe inaanza hapakuwepo na viongozi wa tawi,kata wala wanachama wa mtaa wa kongowe mwishoni baada ya mgenei rasmi MH SITTA kumaliza kujibu risala ndipo aliingia mwenyekiti wa ccm kata na kisha kuongea baada ya ya mgeni rasmi.