KICHAKA
Member
- Jun 17, 2009
- 58
- 9
Katika hali ambayo ilijulikana na ambayo inaelezwa kukolezwa kwa kutokuwepo jawabu la kujivua gamba, ni wazi sasa Sitta na kundi lake katika kuwania urais mwaka 2015 wameanza harakati za kujiweka sawa na wana CDM ambao wanaamini wataweza kuwapigia upatu kujiunga na chakma hicho mwaka 2015 kama mambo hayatakuwa upande wao katika CCM.
Taarifa za karibu na mbunge wa Arusha Mjini CDM zinaeldeza kuwa, mbunge huyo alikutana na Sitta kabla ya Sitta kumwagia sifa huku Sitta akimuelezea kuwa anakubaliana naye katika hatua za kuufanya mkoa wa Arusha usitawalike kwa kuwa unampaka matope EL. Hata hivyo, Sitta aliambiwa na watu wa karibu na Mbunge Lema kuwa, Arusha ikibaki hivi ilivyo CDM watashinda kirahisi mwaka 2015 lakini Sitta asijihakikishie kuwa huo ndio utakuwa mtaji wake kuingia CDM kwa kuwa chama hicho kwa sasa kina vigogo wengi wenye ushawishi kuliko yeye Sitta. Hata hivyo kauli kutoka kwa kiongozi mmoja wa CCM ambaye yuko karibu na Waziri Mkuu Pinda alikimbia chanzo cha habari hii kuwa, Sitta sasa ameanza kupambana na serikali na hasa nafasi yake Waziri Mkuu ambayo ndiyo hasa kimsingi inasimamia mgogoro huo wa Arusha. "Tunajua katika CCM nini anachofanya Sitta, naona wameanza kuungana na kuonyesha kambi yao mapema. Hii inatupa urahisi kwa kuwa kambi zote sasa zinazjulikana kama ulivyoona kule Arusha juzi," chanzo hicho kilifafanua. Chanzo hiki kinaonyesha kuwa mpango wa kuchangisha harambee mbalimbali ulioasisiwa na Edward Lowassa sasa umechukuliwa na kambi ya Sitta akishirikiana na watu wake wa karibu na una lengo la kuhakikisha kuwa wanashindana na Lowassa katika kupita maeneo mbalimbali ya nchi.
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliozungumza na vyanzon vyetu wameonyesha kufurahia harambee hizi na wakawataka wanaojipitisha pitisha kuongeza nguvu ili kutatua kero za wananchi kwa kuwa serikali inaonyesha kulemewa. Taaarifa zaidi subiri magazeti yajayo.