impongo
JF-Expert Member
- Feb 18, 2015
- 8,846
- 7,904
katika likizo ya mhula wa kwanza miaka ya 90- nilipewa pesa kiasi cha sh2000 nikajinunulie sare za shule kaptura 1000+1000 shati
Njia iliyokuwa inaingia sokoni kwa upande wa nilikotokea kulikuwa na wapishi wengi wa Supu ya nguruwe iliyokatwa katwa mapande makubwa makubwa ya nusu kilo na yakichemshwa huvimba na kuwa makubwa kama kilo 1 hivi.
Mapande hayo yaliuzwa sh500 uchovu wa kutembea umbali na njaa nilijishitukia napitia kila sufuria kuonja mchuzi nilianza sufuria la kwanza naonja hadi la 7 nilipofika la 8 uvumilivu ulinishinda
Hakika nilipo onja namba8 Supu ilikuwa tamu sana na watu wengi walipanga foleni maana huyu alikuwa anakupa Supu kwa 600 na anakuongezea ndizi 2 nilinunua Supu ya 600 nikajaziwa bakuri kubwa na ndizi 2 sikushiba nikaongeza bakuri lingine la 600
Nikawa nimetumia pesa ya kununulia sare nikabakia na 800 ilikuwa haitoshi hata nguo moja nikarudi nyumbani mikono mitupu.
Yaliyonikuta siwezi kusimulia ngoja iendelee kuwa siri yangu na Baba yangu mzee mkatili sana.