Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

fungu langu la kumi nitaenda kulitoa kwa mayatima na wagonjwa hospital lakini sio kanisani
kisha uje na andiko lililosema fungu la kumi pelekni kwa maskini/yatima. nadhani umemwonea wivu Mungu maana ndiye ameelekeza kutoa sadaka nyumbani mwake. suala la matumizi ya fedha ya sadaka hayakuhusu sana kama mshirika ila yanamhusu Mungu na yule aliyempa kazi ya uchungaji.
 
Hongera kwa kufumbua macho
 
Maisha ni unavyojipanga. Biashara ya dini inalipa sana ndiyo maana watu wengi wanakimbilia. Makanisa yanaongezeka sbb biashara ipo. Jiulize kwanini Ulaya vijana na watu wa umri wa kati wanaojitambua hawasali bali ni wazee tu pamoja na kwamba ndo walikuletea majina unayoyatumia ya Patrick, Peter, James n.k, na makanisa mengi yanafungwa.
 
Hawa nawakumbusha wale wafia dini lakini kipato kama mimi halafu unapeleka nusu mshahara eti sadaka ya ujenzi nyumba ya Ibada. STUKA
 
Hapana,hayo makanisa3 uliyoyataja no makubwa kinachoingia ni kikubwa ,na kinacholiwa pia kikubwa.


.
Wewe unaenda kutoa sadaka Makanisa ya Kilokole unategemea nini..??

Makanisa yanayojielewa kama Katoliki, KKKT na Anglican ni mahala pa kutoa sadaka...Maana huko Mashule, vituo vya watoto yatima, hospitali zinajengwa..
 
fungu langu la kumi nitaenda kulitoa kwa mayatima na wagonjwa hospital lakini sio kanisani
Fungu la kumi ni tofauti na sadaka, na fungu la kumi litaliwa na watoao Huduma madhabahuni kama ma padri, wachungaji na kadhalika na imeandikwa kwenye biblia, na huo ndio mshahara wao na kama ataamua kununua magari ni yy ila ww toa tu, ni kama ww unavyopokea mshahara wako hakuna anaekupangia nn cha kufanya tusiwe na wivu na watoa Huduma Wa madhabahuni
 
Ashukuriwe Mungu Kwa kondoo wake kutoka kifungoni kwa makanisa ya sadaka tu..karibu KKKT apa utasomewa kila j2 mapato yako na Mgawanyiko wake..
 
Nina uhakika sadaka uliyowah toa hapo haifiki hata kununua baiskeli. Kw hyo hata usipotoa ataendelea tu kununua Magari bora ukatoa tu hiko kidogo Mungu akubarikie. Labda ingekuwa ni sadaka yako tu ndo imenunuela magari hayo ndo ungekuna kulalamika.
 
Kuna tatizo katika kanisa la leo. Yesu angekuja angekemea na hata kuwachapa na kuwafunga baadhi ...
Baadhi ya wachungaji na wahubiri tamaa yao kubwa ni pesa.
Jana nilipanda basi hapa Dar ndani alikuwepo kijana mmoja mhubiri kaweka hadi maspika alisoma tu mstari mmoja wa Biblia na kuanza maneno meengi hadi kusema kuwa baba yake alikuwa mchawi! Mwisho alianzaa kuomba sadaka.
siku hizi hata maombezi ni kwa pesa. Tusikatae, kuna haja ya kujihoji tunakoenda kiimani usanii umeingilia imani!
 
Wachungaji wengine ni wauza sembe. Kanisa ni geresha tu.
 
Usimamizi mbovu huo mimi katika parokia ninayosali ipo poa sana kila Kitu kipo wazi Hakuna usiri tumejenga chekechea tumejenga kanisa jipya kubwa tumejenga chuo cha ufundi stadi nk paroko wetu ni zaidi ya msikivu bajeti tunasomewa mwisho wa mwaka unapokuwa na wasiwasi unaruhusiwa Kuuliza hata ukiwa peke yako huduma zote hutolewa kulingana na utaratibu wa kanisa, matumizi ni wazi
 
Ww sio muislam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…