Notorious thug
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 2,817
- 10,595
Mwishoni mwa mwaka 2018 nilikuwa natokea Arusha kwenda Moshi ilikuwa ni usiku kama saa nne hivi kutokana na changamoto ya magari (coaster) pale stand ilibidi nipande hadi mianzini pale kucheki kama naweza kupata usafiri.
Nikiwa pale Mianzini nilikutana na baba mmoja nae alikuwa anaelekea Moshi baada ya kumuona pale akaniambia tusubiri tunaweza kupata gari tukiwa pale ilikuja gari Noah ila walituambia wanaishia Kibosho road walikuwa watu wawili dereva na jamaa yake tulipanda mimi na yule baba kwenye ile noah kuanza safari ya kwenda Moshi.
Tukiwa Kikatiti gari iliharibika tukashuka mimi na yule baba na wale jamaa wawili ghafla walitucheki kwa kutumulika na simu wakamwambia wewe mzee upo tumekutafuta sana kumbe upo huku chuchumaa safari yako ya kwenda Moshi imeishia hapa na safari yako ya kuishi duniani imeishia hapa.
Wakanigeukia wakaniambia dogo Dk 15 uwe ushafika kilomita 20 kutoka hapa ondoka sasa hivi au tukuondoe na huyu mzee, niliondoka kwa mwendo mkali sana sijui nini kilimtokea yule mzee ilibidi nikimbie nilale chini ya mti asubuhi nikapata coaster hadi Moshi, niliwaza hili jambo sijawahi pata majibu hadi leo.