Sitasahau Special Thread

Sitasahau Special Thread

The Death Of My Beloved Father...nakumbuka siku, saa, tarehe, sehemu na tukio lenyewe and the worse part is i saw how the death happened.
Pole sana Mkuu, Ni vigumu sana kusahau lakini Mungu ndiye Muweza wa Yote.
 
Aisee, hii kali!
Unajua naogopa kukusimulia wewe mkasa huo maana huwaga tukikutana unaninunuliaga kiroba!...nahofia utaghairi!
Ongea vyema na @FL1, huenda akakufowadia!


hahaha Preta nitumie kiroba by DHL nikufowadie maana kila nikikumbika mkasa huu nacheka mwenyewe
 
Aaaargh! kamanda kadada kalikuwa faifu star, hiyo hela ya vibuti yenyewe niliiba kwenye kiduka cha faza enzi zile na nyengine nikaongezea kwa mkopo, kibuti kile kilinipatia mahitaji yangu yote ya ngono kijijini na nilikuwa na uhakika na haka kadada ningekakamata thru kibuti kale lakini kibaka akachafua mchezo wote
Klorokwini na wewe ndo ukaahirisha kidate kisa viatu|? kwani huwawa na ndala ?
 
Siku baba yangu mzazi alipofariki. Ilikuwa tar 5 January 2006. Alituita watoto wake wote ktk xmas tukasherehekea, baada ya new year akatwambia kila mtu arudi kwake. Nilibaki. Tar 5 saa moja usiku nilishuhudia akiwa ktk comma, miguu yake ilikuwa ya baridi. Kufika hospt hali ilizidi kuwa mbaya, hadi anakata roho nashuhudia. Kila nionapo msiba popote, scene yote ya kifo cha baba inanijia.
R.I.P Baba.
 
Mie nilifurahi sana nillipoona matokeo yangu ya form 6,coz wakati nasubiri pepa ya mwisho nililala nikawaomba wenzangu waniamshe mda ukufika wakanisahau,
Niliposhtuka ilikuwa saa nane na nusu na mtihani ulianza saa nane kamili,nilikurupuka na shimizi na sketi na soksi miguun bila viatu wala,shati nikiwa nalia kwa sauti huku nikielekea chumba cha mtihani nikikimbia,
Dah namshukuru mungu nikaruhusiwa kufanya mtihani na nikafaulu vizuri sana.
 
Mie nilifurahi sana nillipoona matokeo yangu ya form 6,coz wakati nasubiri pepa ya mwisho nililala nikawaomba wenzangu waniamshe mda ukufika wakanisahau,
Niliposhtuka ilikuwa saa nane na nusu na mtihani ulianza saa nane kamili,nilikurupuka na shimizi na sketi na soksi miguun bila viatu wala,shati nikiwa nalia kwa sauti huku nikielekea chumba cha mtihani nikikimbia,
Dah namshukuru mungu nikaruhusiwa kufanya mtihani na nikafaulu vizuri sana.

pole cantalisia ila hongera kwa kufanikiwa kufanya mtihani ,,ni kweli hapa huwezi sahau
 
Nikiwa darasa la saba mwalimu akawa anafundisha nishati. Akasema mwanga ni nishati inayotuwezesha kuona, nikamuuliza giza ni nini? Nilikula fimbo za kutosha.
Nikiwa sekondari nilimuuliza mwalimu mkuu, dagaa kwa kiingereza anaitwaje, nikapewa suspension ya mwezi mzima.
Walimu wa shule za upe na za kata hatari kabisa

Pleaseeeeeeeeeeeeeeee! inatosha shemeji!
 
Mie mkasa wangu nilishausimulia hapa, nilipanda daladala la kwenda Mbagala, abiria mmoja wa Iringa nadhani alikuwa ni House girl kwa mtu akanifananisha na binamu wa mwajiri wake, na kwamba kuna siku nililala kwao nikamvizia usiku nakumbaka........ Alisema eti naitwa James na ninafanya kazi kwenye kutengeneza Simenti na ni Dereva.................LOL
 
Pleaseeeeeeeeeeeeeeee! inatosha shemeji!

shem, mbona umehamaki?
Tatizo ukiwa mtundu kwenye zile shule alizo tuachia Nyerere, basi wewe ni mkosaji wa makosa yote.
Kuna siku mtoto wa darasa la kwanza kakutwa amejikojolea, mwalimu kataka kuchapa, akajitetea amepigwa na kaka hadi amejikojolea.
Bila uchunguzi wala udadisi kufanyika, nikaja kutafutwa darasani. Thanks God siku ile nilikuwa nimebanwa na pumu, kwa hiyo sikutoka tangu nilipoingia shule asubuhi.
 
ni visa vingi sana nimekutana navyo sipendi kuvikumbuka vitaniharibia siku kabisa, am sorry
 
pole cantalisia ila hongera kwa kufanikiwa kufanya mtihani ,,ni kweli hapa huwezi sahau
Yani ww acha tu,
Pata picha nilikuwa na wakati gani kipindi nasubiri matokeo?!!!
Nilikuwa kila nikikumbuka nalia tu na nakujiona safari yangu ya chuo ndio iliishia pale!
Nilikonda mpaka watu wakaanza tetesi!!!
 
Siwezi sahau darasa la tatu, Imla ya Sadiki Na Sikiri, kalamu yangu ikagoma kuandika halafu mwalimu alikuwa mkali kama simba.
Bahati nilikuwa mwembamba ingekuwa watoto hawa wa sasa wanaojua stress siku hiyo wangeita ambulensi maana hiyo presha haikiwa ya kawaida.

Thank God akamwambia monita akusanye madaftari, nikapata muda wa kukopi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom