Sitakuja kumsahau huyu daktari kwa alichonifanyia

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
11,763
Reaction score
27,149
Wakati najifungua mtoto wangu wa kwanza kuna daktari nafikiri alikua bado ni mwanafunzi Muhimbili alinishika mkono kwa zaidi ya lisaa limoja wodini akinituliza, na kunitia moyo.

Yule daktari alikaa pembeni ya kitanda changu akawa ananiambia itakua fine, itakua fine, kwa sababu niliingiwa hofu (anxiety) nikawa nalia nasema “naogopa”.

Hakunifokea wala kuniongelesha kwa ukali na alielewa situation yangu (nilienda hospitali kliniki yangu ya mwisho kumbe tayari nimeshaingia kwenye labour bila kujijua, nikabaki hospitali kujifungua bila kutarajia).

Sitasahau alivyonicomfort na kubaki na mimi wodini mpaka mume na mama yangu walivyofika. Na aliendelea kubaki wodini mpaka nilivyojifungua masaa mawili baadaye.

Tired Season 5 Episode 1 GIF by One Chicago.gif

Ule moyo wake ulinigusa sana, huwa namkumbuka mara kwa mara na kumuombea mema. Sikuwahi kukutana naye tena baada ya kujifungua na sijui yuko wapi. Natumai popote alipo anazidi kubarikiwa sana.

Nani alikutendea wema kwenye kipindi chako cha uhitaji hautakuja kumsahau?
 
Wakati najifungua mtoto wangu wa kwanza kuna daktari nafikiri alikua bado ni mwanafunzi Muhimbili alinishika mkono kwa zaidi ya lisaa limoja wodini akinituliza, na kunitia moyo.
Mwenzako alikua anafanya kazi ya kuandaa report yake ale marks wewe unasema moyo waa kujitoa wakati umemkuta mtu yupo field hivi unaelewa nini maana ya field? Mafunzo kwa vitendo
 
Sidhani kama ilikua ni marks, mimi sikua mgonjwa wake. Na hata kama, hakuwa na haja ya kunishika mkono na kunitia moyo kwa namna ile.

Comfort Holding Hands GIF by One Chicago.gif

Nilikua na nesi na daktari wangu ambao walikuja baadaye. Shift yake iliisha ila alibaki almost 3 hours more (labda alitaka kujifunza, sijui) ninachojua alikua mwema sana kwangu.
 
Wakati najifungua mtoto wangu wa kwanza kuna daktari nafikiri alikua bado ni mwanafunzi Muhimbili alinishika mkono kwa zaidi ya lisaa limoja wodini akinituliza, na kunitia moyo.

Yule daktari alikaa pembeni ya kitanda changu akawa ananiambia itakua fine, itakua fine, kwa sababu niliingiwa hofu (anxiety) nikawa nalia nasema “naogopa”.

Hakunifokea wala kuniongelesha kwa ukali na alielewa situation yangu (nilienda hospitali kliniki yangu ya mwisho kumbe tayari nimeshaingia kwenye labour bila kujijua, nikabaki hospitali kujifungua bila kutarajia)! Sitasahau alivyonicomfort na kubaki na mimi wodini mpaka mume na mama yangu walivyofika. Na aliendelea kubaki wodini mpaka nilivyojifungua masaa mawili baadaye.

View attachment 3276598

Ule moyo wake ulinigusa sana, huwa namkumbuka mara kwa mara na kumuombea mema. Sikuwahi kukutana naye tena baada ya kujifungua na sijui yuko wapi. Natumai popote alipo anazidi kubarikiwa sana.

Nani alikutendea wema kwenye kipindi chako cha uhitaji hautakuja kumsahau?
Endelea kumuombea baraka ili aendelee kuwa faraja kwa wahitaji wanaopita katika mikono yake.
 
Back
Top Bottom