Sitakubali kuvuliwa uwaziri - simbachawene | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitakubali kuvuliwa uwaziri - simbachawene

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jun 4, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD] Simbachawene: Sitakubali kung’oka uwaziri


  na Happiness Mtweve, Dodoma


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesema hatakubali kung’oka katika wadhifa huo kwa uzembe, ubadhirifu, urasimu na ufisadi unaofanywa na wafanyakazi katika wizara hiyo, na badala yake atawawajibisha mara moja.
  Simbachawene alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.
  Alisema kumekuwepo na tatizo la baadhi ya watumishi kuingiza siasa kazini na kuharibu kazi, ili watu wengine wanaofanya vizuri waonekane hawafai baada ya kuibuka tatizo la nchi kuwa gizani na kuwalazimu mawaziri kutakiwa kujiuzulu na kusema kuwa hatang’oka madarakani kwa mtindo huo.
  Simbachawene alisema watumishi hao wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuibua mianya ya rushwa kwa kuwacheleweshea kuwaunganishia umeme wananchi kwa makusudi.
  Naibu waziri huyo alionekana kuibeza taarifa iliyotolewa na Meneja wa Mkoa wa TANESCO ambayo inaeleza mafanikio na juhudi zilizopatikana kutokana na utendaji kazi wao, ambapo alisema taarifa hiyo ni ya uongo na haina ukweli wowote ndani yake.
  “Nashangaa eti mnasema kuna mafanikio, hakuna lolote, mmelala tu, wala hakuna kazi mliyoifanya, siku tatu tu nilizokaa hapa Dodoma nimefuatwa na watu zaidi ya watano ofisini kwangu wakinilalamikia urasimu mnaoufanya huku wengine wakiwa wamekaa miaka miwili wakisuburi kuunganishiwa umeme bila mafanikio.
  “Hapo mnaweza mkajisifu mmefanya kazi kweli, tusidanganyane na tutaonana wabaya kama mtu atashindwa kusimamia kazi yake vizuri, lazima wananchi wapate umeme mpaka vijijini,” alisema Simbachawene.
  Alisema uongo wa taarifa ya meneja huyo unatokana na idadi ndogo ya wananchi waliounganishiwa umeme mkoani hapa, ambayo haiendi sambamba na idadi ya wananchi wenye mahitaji hayo.
  Pamoja na hayo, alisema TANESCO Mkoa wa Dodoma bado haijaenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia na kuwataka wajiulize wamechelewa wapi kufanya mabadiliko hayo.


  My take.tunahitaji vitendo zaidi sio vitisho vya maneno


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huwa wanaanza hivyohivyo!
  Kwani hatukuwahi kuwa na askari wa miavuli, ambao waliyofanya ndio haya tunayolia kilio cha mbwa?
  Unaweza kuwa na dhamira njema ya utendaji, lakini utafika mahala utakwamishwa na sera na kanuni za CCM!
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Kwanini wanaolalamika wengi ni watu wa jamii fulani ya aina moja?
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  fisichawene umewekwa hapo kulinda dili za ridhiwan na barick
   
Loading...