Sitaki Riba iongezwe kwenye salio langu la Benki nifanyeje?

msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,826
1,731
Maalum kwa waislam tu,

Assalam aleikum, kwa mujibu wa dini yangu Riba ni kharam, na mwenye kula riba anakua ametangaza vita na Allah ( SW) nimesha iambia Benki yangu wasiniwekee Riba kabisa na ninashaka hata pesa yangu wanakopesha wengine kwa Riba. Mimi ni mwajiriwa na kila mwezi Alhamdulillah mshahara unaingia... napenda kula khalal, sipendi kumkosea Muumba wangu.. wataalam wa islamic Banking na wataalam wa dini hii adhim karibuni otherwise nafikiria kufunga accout yangu shida ni kwamba niko nje ya nchi na benkii hii ni miongoni mwa Benki za zenye option ya VISA ambayo hunisaidia kuchukua pesa popote ili kujikimu na kutuma home.

Fadhwal mashhkura
 
Unaongelea waislamu gani wewe? Au wale wanaosema kuua ndugu yako wapata thawabu kwa allah?
Acha ujinga wewee,mtu kauliza swala la msingi wewe unaleta upumbavu.Aliyekwambia uislamu ni kuua mtu asiye na hatia nani?
 
Acha ujinga wewee,mtu kauliza swala la msingi wewe unaleta upumbavu.Aliyekwambia uislamu ni kuua mtu asiye na hatia nani?
Al shabab.. Boko haram, Hawa boko haram nawajua nilienda kwenye operation dhidi yao, wanaamini kuua Ni kufika akhera.
 
Al shabab.. Boko haram, Hawa boko haram nawajua nilienda kwenye operation dhidi yao, wanaamini kuua Ni kufika akhera.
Tatizo ni kutoelewa,ni kwamba kuna UISLAM na WAISLAM.Unaweza kuwa muislam kwa kuwa wazazi wako ni waislam lkn uislamu kama dini ina misingi yake na moja ya misingi hiyo ni kutokuua mtu asiye na hatia.Wale wanaoua ni kwa maslahi yao lkn si kwa kanuni ya uislam.
 
Suala la riba limekuwa mtihani sana kwa maisha ya siku hizi,inshaallah Allah atufanyie wepesi tuiepuke,riba ni dhurma.
 
Jamaniiii si kuna islamic bank si mwende huko..hizo riba sie wengine twazitaka huku..watu mmetosheka pesa jamanii.basi na biashara msiwe mnafanya..maana kama umenunua bidhaa efu tano alafu ukauza elfu kumi nayo pia dhambii.
 
Nadhani hujui maana ya riba,acha nikusaidie; Riba ni biashara inayohusisha fedha tu,mfano unakopa alfu moja unarudisha alfu moja na mia tano.Hiyo mia tano iliyozidi ndio riba ama biashara inayohusisha bidhaa na fedha sio riba.Mfano ukanunua mchele kwa mkulima kwa sh 5000 na kisha ukamuuzia mlaji sh 10000 ni halali kwa kuwa imehusisha bidhaa.
 
Hamna tofauti..zote ni biashara tuu.maana bidhaa pia ni pesa.watu wananunua dhahabu wanakaa nazo ni bidhaa lakini ndo jinsi ya kutunza pesa for future.sasa kama pesa yangu nikamkopa mtu akaenda fanya nayo biashara akadhalisha faida kwanini asinipunguzie faida aliyoipata..wakati na mimi pesa yangu niliipata kwa shida..na ikamsaidia yeye..vitu vingine bana...imekaa kiimani zaidi lakini kiuhalisia sioni mantiki yake..fungueni islamic bank zenu....msituharibie wapenda riba wengine huku
 
Mkuu kwani tatizo ni kitu kinachoitwa pesa au tatizo ni kitu kinacho tumiwa kama medium of exchange huo mfano wako hapo juu bado ni unyonyaji
 
Hamna tofauti..zote ni biashara tuu.maana bidhaa pia ni pesa.watu wananunua dhahabu wanakaa nazo ni bidhaa lakini ndo jinsi ya kutunza pesa for future.sasa kama pesa yangu nikamkopa mtu akaenda fanya nayo biashara akadhalisha faida kwanini asinipunguzie faida aliyoipata..wakati na mimi pesa yangu niliipata kwa shida..na ikamsaidia yeye..vitu vingine bana...imekaa kiimani zaidi lakini kiuhalisia sioni mantiki yake..fungueni islamic bank zenu....msituharibie wapenda riba wengine huku
Imani yako ni tofauti na yangu so huwezi elewa japo nimekufahamisha kwa ufasaha.
 
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

A very late reply, lakini itawafaidisha wengineo In sha Allah.

Andika barua fupi peleka kwenye branch yako inayosema hutaki kuwekewa riba. Simple, inachukua chini ya dakika 5 tu. Basi wanacancel hapo hapo (kwa sababu ni profit kwao). Benki kama Exim Bank na BancABC ipo wazi kabisa.

Alternatively, kama hutaki unaweza kufungua prepaid card ambayo unaweka pesa na ni VISA card inafanya kazi mahala popote duniani na nzuri kwa online transactions. Hizi huwa haziwekwi Interest kabisa na unaweza kuioperate kama account ya kawaida although its not an official account. BancABC ndio nafahamu wanatoa hii huduma.

Matawi ya Islamic banking nayo yameongezeka sana kwa sasa kwa hiyo itakuwa kheri kama ukiweza kujiunga huko ili kukwepa hiyo fitna.

Allahu Aalam
 
Mkuu hizo pesa za riba zikiingia nipatie niwape wahitaji kama wajane na yatima. Mifutari yote inayotolewa na benki kwa waislamu ni pesa inayotokana na riba.
 
Back
Top Bottom