Sitafutwi na mtu, kama yupo aje Bariadi - CHENGE. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitafutwi na mtu, kama yupo aje Bariadi - CHENGE.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pretty, Oct 29, 2009.

 1. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Na Bahati Mwiko, Bariadi
  28 October 2009


  MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge amesema hakuna mtu anayemsaka kwa ufisadi na kama yuko amfuate Bariadi amkamate.

  Vile vile Bw. Chenge amewataka wapiga kura wake kuwapuuza wanasiasa aliosema wanaeneza uvumi huo kwa madai kuwa ni wanasiasa uchwara, waliofilisika kisiasa.

  Mbunge huyo aliyelazimika kujiuzulu uwaziri wa Miundombinu Aprili 20, mwaka huu baada ya akaunti yake ya nje kwenye Kisiwa cha Jessey kubainika ina zaidi ya sh. bilioni moja zinazodaiwa kupatikana kwa rushwa ya rada, alisema kuwa yeye ni safi na pia mbunge wa vitendo.

  "Ndugu zangu nataka niwaambie kitu kimoja, wapo wanasiasa uchwara hasa hawa wa chama cha (UDP) wenye chama cha ukoo, wanasema eti mie siwezi kuja kwenye jimbo langu. Ni waongo mimi sitafutwi, msiwasikilize wana nia ya kuwalaghai muwape kura, kama natafutwa wakawambie niko Bariadi waje wanikamate," alisema Chenge.

  Bw. Chenge aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Bariadi alipokuwa akihitimisha kampeni za wagombea wa uongozi katika Uchaguzi wa Serikari za Mitaa uliofanyika Jumapili iliyopita.

  Aliwalaumu Mwenyekiti wa UDP, Bw. John Cheyo na mdogo wake, Bw. Isack Cheyo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2005 kabla ya kiti hicho kuchukuliwa Bw. Chenge, kuwa wanaeneza maneno ya uongo kwamba yeye (Bw. Chenge) hawezi kufika jimboni hilo kwa sababu anatafutwa na makachero wa Uingereza.

  Bw. Chenge anachunguzwa na Taasisi ya kuchunguza Rushwa ya Uingereza (SFO) kama alihusika na rushwa ya rada iliyoligharimu taifa zaidi ya sh bilioni 40. kutoka kwa Kampuni ya kuuza zana za kijeshi (BAE Systems) ya Uingereza.


  Chanzo gazeti la majira.

  Sio mpenzi wa siasa, lakini baada ya kuona hii habari imenitouch kwa kweli. Hivyo nimependa kushare nanyi watu wa jukwaa hili.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,429
  Trophy Points: 280
  Huyu Fisadi Vijisenti Chenge alishanyunyiza "uchawi" wake pale Bungeni na anajua siri ya ufisadi wa Rada na hakuna wakumgusa maana yeye ndiye aliyekuwa mgawa Bulungutu kwa wahusika wote akina Idrissa, si ajabu Mramba (hata majani tutakula lakini Rada lazima inunuliwe, Mkapa na wengineo)

  Sasa amepata kiburi cha hali ya juu, TAKUKURU haijawahi kumuhoji yeye wala Idrissa Rashid ambao kuna ushahidi wa kutosha kwamba wamepata pesa chungu nzima kutokana na ufisadi ule. Vethlani tuliambiwa kwamba alikuwa anachunguzwa na vyombo vya dola lakini "akatoroka" nchini katika mazingira ya kutatanisha.

  Mafisadi wote wa (EPA, Kiwira, Richmond/Dowans, Rada n.k) akina Mkapa, Karamagi, Jeetu, Rostam, Manji, Subash Patel na wengine wanapeta uraiani na TAKUKURU wala haina habari nao kabisa eti sasa wamewashupalia Wabunge kwa kuchukua masurufu mara mbili!!!

  Ingekuwa vizuri wangeanza kumchunguza na Rais ambaye alitumia mabilioni ya pesa za kifisadi ili kumchafua SAS kwa kutoa hongo ili aibuke kama mgombea wa CCM. Hawa TAKUKURU ni hovyo kabisa kazi imewashinda na hawana maana yoyote katika vita hii dhidi ya mafisadi. TAKUKURU kazi ya kupambana na ufisadi imewashinda ni bora tu ivunjwe badala ya kutumia mabilioni ya walalahoi bila kupata mafanikio yoyote katika kupambana na rushwa.
   
 3. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Watatamba sana maana wanajua fika kuwa watanzania wengi ni bongolala.
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Sasa wapambe wa Hosea na Zitto wako wapi kusema TAKUKURU imchunguze mbunge huyu maana huu ni ufisadi kweli... lakini katika hili naona kimyaaaaa, eti TAKUKURU wanachunguza posho za wabunge na kumhoji Mwakyembe.... na ndo wanalisapoti kwa nguvu zote.....
  Kweli tunacheza tu hapa na sisi wananchi tumelala.......
   
 5. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  I say, jamani hii inatia uchungu!!!!
  Kikwete ndio kalala fofofo!!! Kwa kweli siamini!!!
  Chenge baada ya kukutwa na pesa tele bado anatamba na hakuna la kumfanya!!!
  Japokuwa wengine watasema hizi ni fikra za usaliti, lakini naona wakati umefika wa kuiga yale yaliyotokea kule Philippines na kule Romania, bila ya hivyo tutafedhuliwa kila siku!!!
   
 6. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani hoja hii ni nzito sana,mzee wavijisenti atafutwe nchi hii,kaiba msenti kibao,kaua mtu akiwa hana leseni,bima lakini anadunduda tu.kweli nchi hii tunakokwenda bado akujajulikana-si jui kama tutafika????
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  chenge anaongea ukweli mtupu! hakuna wa kumtafuta ndani ya tanzania hii...............
   
 8. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kikwete mwenyewe unayemsema huanguka anguka, sasa unashangaa akilala fofo fooooo?
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Oct 29, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  KWeli Tanzania yetu inatia aibu. Hivi hawa mafisadi na viongozi wababe tutawavumilia mpaka lini? Ni hata lini tutawaacha waendelee kutuchezea namna hii? Wizi wao, ufisadi wao, EPA, wao wanajinufaisha kwa jasho letu na bado hakuna maendeleo yoyote wanayotuletea zaidi ya kuendeleza matumbo na koo zao tu. Watanzania tuamke jamani hivi silaha yetu ni ipi hasa ambayo itasaidia kuwaamsha hawa viongozi wajue kuwa tumechoka kutumiwa kama madaraja yao kuelekea kwenye ufalme wa utajiri? Wao wanaishi maisha mazuri hawaijui dhiki kama sisi wananchi wa kima cha chini. Tuamke.

  Kwa hali inavyoonekana sidhani kama tutaimaliza miaka kumi pasipo watu kuingia msituni. Si wanasema vita ni njia mojawapo ya kuelekea kwenye maendeleo? angalia mataifa karibia yote yaliyoendelea yalipitia katika vita na yameendelea wakati Tanzania tumebakia na sifa ya Amani tu ambayo bahati mbaya haichangii katika maendeleo sanasana watu wanatake advantage to kwayo.

  Tujiandae kupigana!
   
 10. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kikwete na Mafisadi wenzake wanatia aibu sana, yaani huyu Jambazi Fisadi Chenge ambaye hivi sasa alitakiwa awe lupango bado anatamba mitaani akiwa akiwa bado mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Chama Cha Majambazi (CCM). Halafu sitoshangaa huyu jambazi Fisadi Andrew Chenge akashinda ubunge mwakani.

  2010 ndio inakaribia Dr. Slaa uko wapi ugombee urais wa Tanzania ili hawa Majambazi wa CCM wapelekwe wanapostahili ndani ya jela.
   
 11. k

  kisikichampingo Senior Member

  #11
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Atashinda Ubunge, tena kwe kishindo! Kwani Wasukuma wanajua nini? Si ajabu mpaka leo 90% ya Wasukuma wa Bariadi Mashariki/Magharibi? hawajui kama Chenge ana mabilioni kaficha kisiwa gani sijui,wakati kule kwao hamna kitu.
  Yaani Tanzania, we acha tu!
   
 12. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nd. MwanajamiiOne,
  Kwanza nakupa hongera kuwa wewe ushaamka. Tukipata mtu mwengine kama wewe, na mwengine kama wewe na mwengine basi tatizo litakuwa lishakwisha.
  Silaha yetu kubwa ni wingi wetu. Tunatakiwa tutoke mabarabarani kama walivyotoka wananchi wa wa_Philippines siku ile waliyomuangusha Marcos. Inatakiwa tutumie wingi wetu ili tumzunge Kikwete kama alivyozungukwa Ceascescu na akashindwa kuruka kwa helicopter yake.
  Dr Slaa hata akigombania urais hatopata kutokana na wizi wa kura na kwahivyo tutumie wingi wetu sisi wananchi ili tuwaangushe hawa mafisadi.
   
 13. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Sidhani wale wote waliounga mkono hoja ya uchunguzi dhidi ya wabunge kuhusiana na uchukuaji wa posho mara mbili ni wapambe wa Hosea na Zitto, Kama tunataka kupiga vita Ufisadi, Wizi, Ujambazi na ukiukwaji wa maadili kwa viongozi wetu nchini Tanzania basi ufanywe kwenye ngazi zote husika, tusiweke matabaka kuwa watu fulani wanastahili kuchunguzwa na wengine hawastahili. Iwekwe mamlaka husika ambayo itafanya kazi zake kwa uadilifu na kufuata haki na sheria kuchunguza mambo yote yanayohusiana na ubadhirifu dhidi ya wabunge, bunge letu limejaa kila aina ya watu, kuna mafisadi, kuna majambazi, kuna matapeli, kuna vihiyo, kuna wapambe na pia kuna wachache ambao ni wazalendo waadilifu. Hakuna mtu aliye juu ya Sheria. Jambazi Fisadi Chenge anastahili kuwa jela hivi sasa lakini kama unavyoona bado ni mjumbe wa Kamati ya maadili ya Chama Cha Majambazi (CCM) huku watu wake ndani ya CCM wakiwa kimya na kumlinda.
   
 14. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye nyekundu:
  Nani mwenye uwezo wa kuhakikisha wahusika wote wanashughulikiwa bila upendeleo? Ingekuwa ni kwa nguvu yangu au yako akina Chenge, Lowasa, na wenzao wasingekuwa wanaitwa waheshimiwa leo. Lakini bado Chenge na wizi wote huo wa wazi ana nafasi ya uongozi ndani ya chama chake. Watanzania tunafanywa wajinga sana.
   
 15. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni sisi wenyewe wananchi wa Tanzania ndio tuna nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko, sidhani kama tunafanywa wajinga bali sisi wenyewe ndio wajinga kwa kukubali kuwachagua hawa Majambazi wa CCM katika ngazi zote katika kila chaguzi. Muelemishe ndugu, jamaa, rafiki, jirani juu ya umuhimu wa kura zao na ni jinsi gani nchi yetu itazidi kudidimia ikiwa chini ya utawala wa Chama Cha Majambazi (CCM)
   
 16. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yieki,

  Take that middle finger Kikwete ... and the rest!

  Nina mpango wa kuongeza character ya Chenge kwenye video game ya mafisadi wenye spines ninayodevelop - yaani jamaa anamwonyesha kidole cha kati Kikwete na timu yake yote ya usalama na wala hakuna mtu anayekohoa.

  Chenge is my new "hero".
   
 17. l

  lukule2009 Senior Member

  #17
  Oct 29, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  teteteh hivi JK change ya Rada vipi tulipata? lol
   
 18. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kikwete ndiye mshitakiwa namba moja, wewe unasema Kikwete kalala, nani kasema kalala? yeye ndiye godfather mwenyewe anayewapa kichwa hawa wote.
   
 19. m

  mtangi Member

  #19
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania tumezidi uoga jamani, Mambo kama Haya yakitokea kule kwa kina queen elizabeth, siku nyingi watu wamesha wajibishwa. lakini Sisi Viongozi wetu wataanzaje, wakati wao wenyewe wameoza kabisa.
   
 20. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si ndio maana Chenge anaongea anachoongea. The problem begins and subsequently lies with Kikwete.
   
Loading...