Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
Wanachama sita wa Chadema wamechukua fomu kuwania Ubunge wa Jimbo la Chalinze, Mkoa wa Pwani katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mapema Aprili, mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Said Bwanamdogo kilichotokea Januari 22 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Chadema, Jimbo la Chalinze, Idd Ucheche iliwataja waliochukua fomu katika jimbo hilo kuwa ni Franes Mugusa na Mathayo Torongeyi.
Alisema, wengine wanne walichukulia fomu Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni, Dar es Salaam. Alisema fomu zilianza kutolewa tangu Machi 4, mwaka huu na mwisho wa kuzirudisha itakuwa leo saa 10.00 jioni.
Alisema upigaji wa kura za maoni katika chama hicho utafanyika kesho Machi 8, katika Mji wa Chalinze na baadaye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho itamteua mgombea mmoja atakayeshindana na vyama vingine.
Ucheche alisema fomu za kuwania ubunge zinapatikana katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kinondoni, Dar es Salaam, ofisi za Chadema Jimbo la Chalinze na kwenye tovuti ya chama hicho.
Wakati Chadema kikianza mchakato wa kumpata mgombea wake, Ridhiwani Kikwete alishinda kura za maoni kuwania ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM na sasa anasubiri uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho.
Ridhiwani aliwashinda wapinzani wake; Imani Madega, Ramadhani Maneno na Mkwazu Changwa. Ridhiwani aliwaacha kwa kura za mbali wagombea hao.
Wakati huohuo, Chama cha CUF, kimetamba kwamba Jimbo la Chalinze ni ngome yake na kwamba kitamsimamisha mgombea wake.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema jana kwamba, wako kwenye maandalizi ya mwisho wa kuanza mchakato wa kumpata mgombea.
Pale Chalinze ni ngome yetu kuna wanachama na wafuasi wengi wanaotuunga mkono na tunauhakika wa kulinasa jimbo hii. Sina wasiwasi kwamba Chalinze ni Jimbo la CUF, alisema.