Sisikii sioni, Magufuli milele, hii sasa ndio imekuwa nyimbo yangu

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Yaani kila nikiiangalia CCM kusema kweli hawana anaeweza kumrithi Magufuli, hamna nikiwaangalia naona hawaiwezi kazi ambayo Mheshimiwa anaendana nayo, Sasa hata kule kwa wavaa makoti wala bata na pilau nako ndio yaleyale maji ya futi kwa nyayo.

WaTanzania walio wngi sasa wameanza kuona matunda sio ya CCM maana CCM wamepita wengi, matunda ya Magufuli ukianzia kwenye usalama, leo Tanzania unatembea muda wowote ule hakuna mwenye habari na yeye, leo kila mtu alie na simu basi hakosi net live, hayo ni maendeleo na yalikuwa hayapo, wengi sasa wanamiliki vitu ambavyo wakiviona ni ndoto kwenye maisha yao.

Sasa ikiwa mitano iliyopita tumefarijika kiasi hiki, je mitano mingine tuseme mpaka aridhike kuwa amewafikisha waTanzania sehemu ambayo hawatajuta milele.

Na wala sio vibaya kuna nchi nyingi maraisi wao ni wa milele, haitokuwa ajabu kwa Tanzania.
 
Mara nyingine shirikisheni ubongo kabla ya kubonyeza keyboard. Jiulize kama kusingekuwa Demokrasia ya vyama vingi na ukomo wa kipindi cha Urals, Je Magufuli angepatikana vipi?

Hata kama tunataka Rais wa milele basi tukabadili katiba halafu tufanye mchakato wa kugombea upya na wengine wagombee inclusing Jakaya Kikwette.

Hii mnayodanganya watu kwamba eti hakuna Mtanzania mwingine zaidi ya Magufuli anayeweza kuleta maendeleo Tanzania ni UWONGO ambao hata mtoto wa primary school hawezi kukubali. Kwanza 80% ya mambo anayoringia yameanzishwa aidha na Mkapa au JK.

Magufuli anabebwa na MEDIA ambayo inaripoti mambo yake tu kwa kuwa wakisema mabaya yake wanafutiwa usajili wa chombo cha habari au wanashtakiwa kwa makosa ya Anti Money Laundering.

Kama media ingekuwa HURU kama wakati wa JK na Mahakama nazo zikawa HURU na Bunge liwe linajisimamia, Leo hii Magufuli angekuwa siyo Rais wa Tanzania.
 
Mkapa nae tungesema awe wa milele, Magufuli angeonekana??

Wewe unaona hawapo, ila wapo wazuri kuliko huyo Magufuli kinacho mfanya umuone yeye pekee ni aina ya ufanyaji wake kazi! One man show! Akitawanya mamlaka utawaona walio wazuri kuliko yeye kama ambavyo yeye tulimuona akiwa Waziri wa Miundombinu.

Katiba iendelee kuheshimiwa, hata kama tunampenda vipi
 
Wapo wengi watz wazuri mara 200 zaidi yake mitano ya tosha tuwape nafasi na wengine.Huyu amegusa maisha ya wachache ikiwemo wanufaika Kama wwe mliopita bila kupingwa,lkn still wengi tu utamani Hadi kesho afike kituo chake cha daladala ashuke, mwingine apande.
 
Wandugu hasira hazitawasaidia au kuonyesha wapo wengi ndani ya CCM wakati sio kweli,Magu imetokea kama bahati au tumeletewa atusimamie,na kama kazi basi ameiweza kuliko yeyote yule aliepita.

Mwenye macho haambiwi tazama,anachokifanya Raisi mtarajiwa wa milele,hakijatokea popote pale hapa Afrika, najua wapo wapinzani ambao si ipinzani kiuhalsia bali wamejaa choyo.

Mungu atupe nani kwa sasa zaidi ya Magufuli, CCM hawana mbadala kwa sasa na simuoni.
 
Sasa mnakuwa kama malimbukeni,halafu mnafananisha na mambo ambayo sio kigezo cha utendaji wa kazi, mtu aseme tu anitajie kiongozi aliethubutu kufanya na kusimamia waliochini yake kama Magufuli, mtaje, walau kukemea tu, nani ?

Anachokifanya Magu ndicho ambacho WaTanzania tulikihitaji ,leo tungelikuwa mbali sana na kila kitu imeshakaa kwenye mstari,ila haohao ccm wametuchelewesha sana.

Ndio nikasema hamna mwengine kwa sasa,huyuhuyu aendelee kugombea na hao vilaza wa upinzani milele,tusisikie kuna liccm eti linataka kugombea ,atavuruga kila kitu, Magu aendelee atukabidhi watanzania kitu na boxi yake.
 
Hapa naona neno milele limetumika visivyo. Neno sahihi ni "wa maisha". Rais hawezi kuwa wa milele kwani itafika kipindi atakufa na hivyo anatafutwa mwingine kushika nafasi yake. Huyo Rais mnayetaka awatawale hadi kifo kiwatenganishe ni wa maisha SI wa milele.
 
15032020.jpg
 
Yaani kila nikiiangalia CCM kusema kweli hawana anaeweza kumrisi Magufuli ,hamna nikiwaangalia naona hawaiwezi kazi ambayo Mheshimiwa anaendana nayo, Sasa hata kule kwa wavaa makoti wala bata na pilau nako ndio yaleyale maji ya futi kwa nyayo...
Nilijua kumrithi, kumbe ni 'KUMRISI' basi sawa.
 
Hapa naona neno milele limetumika visivyo. Neno sahihi ni "wa maisha". Rais hawezi kuwa wa milele kwani itafika kipindi atakufa na hivyo anatafutwa mwingine kushika nafasi yake. Huyo Rais mnayetaka awatawale hadi kifo kiwatenganishe ni wa maisha SI wa milele.
Sasa sawa ,ila inapendeza kusema milele kama vile kusema zidumu fikra za mwalimu.

Unajua wengi tumeanza kuona mwelekeo ,hata viongozi anaowaongoza wamepata nguvu za ziada wanamkabili yeyote wakiamini Mkuu wao yupamoja ,kwa ufupi wanawajibika kikamilifu na kwenye utata wanamueleza na anawasikiliza.

Wapi alitokea Raisi namna hio tokea tupate uhuru ? Mengine jiongezeeni,angalia ,kuna maraisi waliopita wengine walifanya Ikulu ofisi za biashara binafsi ,huyu katuletea paa simba yaani ,ana nia ya kuipendezesha nchi yetu na kuitangaza.
nani kama Magu acheni chuki za kuchonga.
 
Fikra za Mwalimu ziliondoka naye. Mwenyewe alikiri, kuzungumzia Azimio la Arusha inakupasa uwe na akili ya kiuendawazimu.
 
Wandugu hasira hazitawasaidia au kuonyesha wapo wengi ndani ya CCM wakati sio kweli,Magu imetokea kama bahati au tumeletewa atusimamie,na kama kazi basi ameiweza kuliko yeyote yule aliepita...
taarabu nyingi huna hoja!..
 
Sasa mnakuwa kama malimbukeni,halafu mnafananisha na mambo ambayo sio kigezo cha utendaji wa kazi, mtu aseme tu anitajie kiongozi aliethubutu kufanya na kusimamia waliochini yake kama Magufuli,mtaje,walau kukemea tu,nani ?...
Msukuma bana!
 
Nina wasiwasi unawazimu au marelia ipo mgongoni,inakuwaje unauliza ,mala sijui kuandika,sa dada nikuulize vipi umefahamu kama sijui kuandika ukaunganisha na tabia.
Mzee malaria sio marelia....

Mzee ni mara na sio mala..

Hanza kujifunza na vitu vidogo vidogo.. Afu ndio uje kuandaa uzi...

Haya sasa... Ulikuwa unasema magufuli afanyaje ???
 
Yaani kila nikiiangalia CCM kusema kweli hawana anaeweza kumrisi Magufuli ,hamna nikiwaangalia naona hawaiwezi kazi ambayo Mheshimiwa anaendana nayo, Sasa hata kule kwa wavaa makoti wala bata na pilau nako ndio yaleyale maji ya futi kwa nyayo.

WaTanzania walio wngi sasa wameanza kuona matunda sio ya CCM maana CCM wamepita wengi ,matunda ya Magufuli ukianzia kwenye usalama ,leo Tanzania unatembea mida wowote ule ,hakuna mwenye habari na yeye,leo kila mtu alie na simu basi hakosi net live,hayo ni maendeleo na yalikuwa hayapo,wengi sasa wanamiliki vitu ambavyo wakiviona ni ndoto kwenye maisha yao.

Sasa ikiwa mitano iliyopita tumefarijika kiasi hiki je mitano mingine tuseme mpaka aridhike kuwa amewafikisha waTanzania sehemu ambayo hawatajuta milele.
Na wala sio vibaya kuna nchi nyingi maraisi wao ni wamilele ,haitokuwa ajabu kwa Tanzania.
....hawana anaeweza kumrisi....
Sentensi hiyo tu inatosha kuonesha uwezo wako wa kufikiri.
 
Elimu elimu elimu... Ni kitu muhimu sana kwa kila mtanzania...

Wakati unaandika huu uzi... Ulishirikisha ubongo ??
Yaani kila nikiiangalia CCM kusema kweli hawana anaeweza kumrisi Magufuli ,hamna nikiwaangalia naona hawaiwezi kazi ambayo Mheshimiwa anaendana nayo, Sasa hata kule kwa wavaa makoti wala bata na pilau nako ndio yaleyale maji ya futi kwa nyayo.

WaTanzania walio wngi sasa wameanza kuona matunda sio ya CCM maana CCM wamepita wengi ,matunda ya Magufuli ukianzia kwenye usalama ,leo Tanzania unatembea mida wowote ule ,hakuna mwenye habari na yeye,leo kila mtu alie na simu basi hakosi net live,hayo ni maendeleo na yalikuwa hayapo,wengi sasa wanamiliki vitu ambavyo wakiviona ni ndoto kwenye maisha yao.

Sasa ikiwa mitano iliyopita tumefarijika kiasi hiki je mitano mingine tuseme mpaka aridhike kuwa amewafikisha waTanzania sehemu ambayo hawatajuta milele.
Na wala sio vibaya kuna nchi nyingi maraisi wao ni wamilele ,haitokuwa ajabu kwa Tanzania.
 
Ugumu upo katika ufahamu wenu,hivi nyie mtaweza kusomeshwa na maprofesa ? mmebumaa vibaya mno ! Nawashangaa ikiwa mna macho lakini hamuoni,eti mna akili lakini hamfahamu,masikio dizaini za ungo lakini hamsikii .

Mnabwabwaja sana lakini bado sijaona wala hamjamuonyesha angalau mkasema huyu na huyu na yule wanaweza kuendeleza mkazo wa JPM,hamna CCM hawana kifaa wala speya inayoweza kukidhi vigezo vya Mheshimiwa Raisi Magufuli.

jamaa zangu wanaovaa makoti kama makobe huko ni utitiri wa mihemko utadhani wanatangaza mnada,hamna kitu wala sifa ndio kabisa hawana,Naachana nao.

Huku aliko JPM hakuna mwengine wa kuweza kuwafunga mapaka makengele,Leo hii mnaona nchi inavyochemka hakuna kuvumiliana tena,hufai unawekwa pembeni,na hadi leo tumepiga hatua ya kupigiwa mfano na sasa kila nchi wananchi wake wanasema wanatamani wawe na kiongozi jasiri kama Mheshimiwa Magufuli.

Mabezo yenu hayana mashiko,mara sijui kuandika,mara hufahamiki,mara huna hoja,ndio nikasema hamna elimu ya uelewa waulizenu wanaofundishwa na maprofesa.

Ila kwa huu ungumbaro mnaouonesha ni wazi mmekamatwa pabaya na ndio nikasema na kudai ni huyu huyu kwa miaka mingi ijayo,hatutaki mbadala.

Magufuli Ameanza kuijenga Tanzania ndio hivyohivyo ilianza kujengwa Roma.
 
Back
Top Bottom