TAI DUME
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 11,462
- 31,608
Habari rafiki.
Kama mnavojua huku umasaini kuna ng'ombe wetu amepotea. Inasemekana alikuwa anafukuzwa na madubu wakali. Huyu ng'ombe ana sauti ya pekee, akilia "MOOOOO" kila mtu anafurai na sauti yake inafika mbali Sana. Tumeulizia kote hata askari wetu morani hawajui msitu alikopotelea.
Sisi wamasai ng'ombe akipotea tunatafuta kwa siku Tano tu zikizidi kama hajaoneka tunahesabia ameliwa na wanyama au amezama kwenye maji kwa hiyo hatumtafuti tena na akionekana hata damu yake hatuitaki
Bado siku Moja tu iliyobaki kumtafuta ng'ombe wetu ila tunaamini tutampata. Morani wetu wanahangaika maporini na wamasai wengine tumebaki kuomboleza. Kama ameliwa na wanyama wakali Ni bora wale mpaka mifupa maana uchungu utakuwa mwingi sana tukiona mzoga wake.
Tunasikia huko mpakani karibu na maji mengi Kuna wanyama wengine ila sio ng'ombe hawajaonekana mpaka Leo baada ya kupotea. Ila wengine tunasikia waliopatikana baada ya siku tatu. Sasa sisi huku ikizidi siku tano hatumtaki tena ng'ombe huyu maana tunauhakika atakuwa kibudu.
Jamani wamasai tumechanganyikiwa. Maana tuna ng'ombe wengine wachache wakubwa Kama huyo aliyepotea wamebaki, Sasa hawa madubu yenye uchu yasije yakanogewa huko yakaanza kuwawinda na hawa..
Shime jamani sisi wamasai hususani tunaovaa mashuka mekundu hali yetu itakuwa mbaya sana kama ng'ombe huyu asipopatikana kwani maziwa yake ni matamu sana hasa mtindi.
Morani bado wapo kazini