Sisi au wao?

Sisi au wao?

harunimaiga

Member
Joined
Nov 13, 2022
Posts
26
Reaction score
47
NAWASALIMU KWA JINA LA JAMAHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,HEKIMA NI UHURU!

Awali ya yote nipende kumshukuru mwenyezi Mungu,kwa kutujalia uhai,amani na utulivu katika Taifa letu,Tanzania.

Utangulizi;
Mwandishi wa makala hii,ni Mimi mwanafunzi wa Chuo kikuu Cha Dar es salaam(Udsm) kutoka kozi ya Sayansi ya Siasa na utawala wa Umma katika ndaki ya Sayansi ya jamii.

Katika kuhakikisha utoaji wa elimu na mafunzo Bora katika chuo kikuu Cha Dar es salaam kwa kuzingatia uhifadhi wa utamaduni,maadili na tunu za Taifa letu,Chuo kikuu(Udsm),kwa kuzingatia miongozo na kanuni za MAVAZI, chuo kimeweka baadhi ya Sheria ambazo ni nzuri na sahihi zihusuzo MAVAZI, kwa kubainisha aina ya mavazi yanayofaa na yasiyofaa kuvaliwa katika mazingira,au maeneo yote ndani ya chuo.

Baadhi ya Mavazi yasiyoruhusiwa kwa jinsia zote,NI suruali(kwa lugha ya mtaani vijana tunaziita crazy) zinazoonyesha mwili,mfano magoti mapaja n.k. Pia mashati hususani yaoneshayo au yasiyofunika mabega(vest) kwa jinsia zote mbili Yaani, kike na kiume.

Kaptura/pensi pia haziruhusiwi,vazi Kama kofia haliruhusiwi,na hili sijajua sababu ya kuzuia uvaaji wa Kofia,hapa napata sintofahamu,kwani msimu huu wa kiangazi,jua ni kali Sana,ambapo hata maeneo ya kuzunguka chuo tunamopita sio mote mna vivuli,hivyo jua lituwakialo ni la utosi.

MKANGANYIKO WA SHERIA ZA MAVAZI

Chuo kikuu cha Dar es salaam kinajumhisha wanafunzi wazawa na wa mataifa tofauti na wakiwa hapa Tanzania,basi tunaishi nao Kama jamii moja.

Wanafunzi wazawa (watanzania) ndio tumekua tukizitii Sheria za mavazi,jambo ambalo kwa wanafunzi wa kigeni ni tofauti kabisa,kwani utaona wao wakivaa hata hayo mavazi yasiyoruhusiwa katika mazingira ya ndani ya chuo pasi na kuulizwa na mtu yeyote.

Mfano, ni kawaida kwa mwanafunzi wa kitanzania kuzuiliwa kuingia ndani ya chuo akiwa ameufunika utosi wake kwa kofia. Lakini pia ni kawaida kuona Mzungu akiingia hata kwenye vipindi na Kaptura Bila hata kuulizwa na mtu yeyote.

Jambo hili linaleta sintofahamu,kwani Chuo hiki kinazo Sheria za mavazi Tena zikiwa na usaidizi wa Picha katika mabango mbalimbali ikiwemo njia zote za kuingia ndani ya maeneo ya chuo.Kama nilivotangulia kusema hapo mwanzo,picha katika mabango hayo,zinaonesha mavavi yafaayo na yasiyofaa ndani ya Chuo ili kulinda maadili na utamaduni wetu sisi Watanzania.

MAMBO YA KUJIULIZA!!!?
1. Je, Hawa wanafunzi wa kigeni hususani wazungu wanazo Sheria au miongozo tofauti ya Mavazi tofauti na wanafunzi Watanzania?

2. Kama jibu katika Mambo ya kujiuliza namba (1) ni NDIYO, Je miongozo hiyo ipo wapi na inawaruhusu kuvaa hivo kinyume na maadili yetu sisi watanzania?

3. Kama sisi Watanzania tunazuiliwa hata kufunika utosi kwa kuvaa kofia,na hawa wanafunzi wa kigeni wanavaa hata Kaptura ndani ya chuo,je huo sio utumwa wa sheria ndani ya nchi yetu,au hizi Sheria ni za sisi Watanzania pekee?

4. Tunaweza kusema labda Hali ya hewa(joto ndio inachangia wanafunzi wa kigeni(wazungu) kuvaa mavazi ya aina hii.Tukijibu NDIYO, Mbona haohao wazungu baadhi yao huvaa Kila siku mavazi Kama yetu sisi(Watanzania)?.Je Hawa wao sio Kama hao(wazungu) wanaovaa kaptura na nguo zisizofunika mabega?

5. Kama jibu sio Hali ya hewa(joto); Je Udsm imeshindwa kulinda utamaduni na maadili ya nchi yetu?

6. Uvaaji wa Kofia unatafsirika kwa namna gani?

7. Jambo hili litatuhusu wote,NI kweli nguo zinazoonyesha mwili(crazy haziruhusiwi) kwani huwa na matundu au uwazi unaoonyesha mwili,Lakini zile light skin trousers zinazovaliwa na wadada wengi na kuwachora karibu maungo yote na miili yao zinaruhusiwa!!!!!!!!!!.

Je, ipi Bora, suruali (crazy) yenye kitundu kidogo mfano kwenye sehemu ya goti la mguu au light skin trouser inayochora na kulemba kwa uzuri kabisa maungo yote ya Hawa ndugu zetu??!

MAPENDEKEZO
Ningeomba Chuo kikuu( Udsm) kiangalie upya na kuboresha sheria za mavazi Sheria zake hususani katika mavazi ili kulinda utamaduni na maadili yetu sisi Watanzania,kwani inauma kuona wenye nchi yao wakizuiwa kuvaa kufunika utosi huku wakuja wakipeta na Kaptura. Taasisi Kama hii ndio inaaminika katika kuleta mabadiliko chanya yenye tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Asante.
HEKIMA NI UHURU
 
Fact
 
Huna exposure tu , umetoka kishimundu huko hujui lolote kwenye jamii ya kimataifa ,unasema kulinda utamaduni wetu halafu unataka huo utamaduni wawafunze wazungu ambao nao wanao utamaduni wao ,

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom