Siri za utajiri (secrets of the rich)

Aug 3, 2018
19
16
hakika hizi ndizo siri za utajiri matajiri wamekuwa wakizificha toka mda mrefu ambapo Mimi toka nikiwa na miaka Tisa(9)nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu sana na kujiuliza maswali mengi kuwa kwanini duniani watu wote si matajiri? kwanini watu wote duniani si masikini? basi kutokana na maswali yote hayo mda wote nilikua nikimuuliza baba kwanini inakuwa hivyo inapokuja kwenye maswala ya kifedha? kwanza cha kwanza alichoweza kusema baada ya kumuuliza maswali mengi nikuwa" usiniamini kwa kile ninachokwambia hata sikumoja"nilishtuka baada ya kuskia neno hilo nikamuuliza kwanini nisikuamini akati wewe ndo unanifundisha? baada ya hapo alinigusa kichwani kisha akasema "tumia hiki" akimaanisha nitumie kichwa changu kupambanua mambo yote ya kifedha! baada ya kusema hvyo akaendelea kusema "pesa ni moja kati ya nguvu lakini chenye nguvu zaidi ni elimu ya pesa,pesa huja na huondoka,lakini kama unaelimu jinsi pesa inavyo Fanya kazi,utakuwa na uwezo juu yake na ndipo unapoweza ukaanza kujenga utajiri wako".baba aliishia hapo wakati huo nikiwa na umri mdogo sana.lakini pia baada ya kufatilia kwa kina za kupitia uchunguzi wa karibu sana nikaja nikagundua kuwa watu wote katika ulimwengu wa kifedha wamegawanyika katika makundi matatu ambayo ni tabaka la juu(rich people),tabaka la kati(middle class) na tabaka la chini(poor people),ambapo tabaka la chini limeonekana kuwa na namba mkubwa ya watu likifuatiwa na tabaka la kati ,wakati la juu likichukua namba ya mwisho.sasa leo nawaleteeni kile ambacho matajiri wakiona nimekiweka hapa wazi lazima wanitafute na kunihoji kwanini nimeamua kuwatolea siri zao wasizopenda wengine wazijue! lakini lengo langu Mimi nikuhakikisha watu wote Tanzania tunafikia kile kinachotajwa kuwa uchumi huru (economic freedom).
kwanza kabla sijakuafanya tajiri naomba niseme kuwa "usiamini kwa asilimia mia kile ninacho kuambia" ila kichukue ukachanganye na akili yako ya kuzaliwa (common sense)ili tuweze kuichangia dunia
zifuatazo ni siri kumi za utajiri duniani kote hebu tumia hizi umiliki pesa isiyo potea kwa muda mfupi.

1.wanaelimu ya fedha(financial education)
niseme hivi hii ndio siri kubwa sana ambayo mtu akiikosa hawezi kuwa tajiri hata siku moja zaidizaidi atapata pesa alafu zitamuishia tu, kwanza naomba nitoe maana ya neno utajiri,utajiri siyo kuwa napesa nyingi au magari mengi ama vitu vingi kumiliki hapana Bali tunaposema "utajiri ni uwezo wa Mali za mtu kuweza kuwepo kwa mda mrefu(vizazi na vizazi)kama yeye mwenyewe ataacha kufanya kazi Leo(retire)" nikisema kuacha kumfanya kazi Leo kifedha namaanisha kuiacha pesa ijizalishe bila kuhusisha nguvu yoyote ya mwenye pesa hyo,hiyo ndyo maana kamili ya neno utajiri.lakini tunaposema elimu ya kifedha pia hiki ni kipengele kipana sana ambacho hata hakifundishwi popote hata shuleni hakuna anaefundisha aina hii ya elimu bali ni mtu anapokua amejitolea kuifundisha jamii kama Mimi navojitolea kutoa elimu hii ambayo haipatikani kokote nchini. elimu ya kifedha ina vitu vingi ndani yake na hivi ndvyo vitakavyo kuweka katika gari la kusafiri kuelekea kule utajiri ulipo kwanza ili uweze kuwa tajiri lazima ufuate yafutayo vinginevyo hautakuja kutajiri kamwe.
lazima uwe na mambo haya.

*matamanio(desire)
kwanza kabisa ili uweze kuwa na elimu ya kifedha lazima uwe matamnio ya kuweza kuwa tajiri,nasema hivi kama hauna matamnio yakuwa tajiri nibora usiendelee kusoma siri hizi kwani utahisi kama kazi ngumu.matajiri wote duniani waritamani kuwa matajiri ndo maana wakaanza kutafuta sasa nitawezaje kutimiza ndoto zangu kuwa tajiri!?nazidi kukupa siri hizi ili wewe na vizazi vijavyo vipate kuwa matajiri wakubwa.

*Fanya kwa moyo wako(make your own choice).
katika ulimwengu wa pesa na uwekezaji hutakiwi kuingia kwa kulazimishwa au kumfata mtu frani bali ingia ukiwa na ndoto zako mwenyewe ukishajua kama una ndoto za kuwa tajiri twende hatua ya tatu.

*tafuta sababu kubwa kuliko uhalisia(find a reason greater than reality).
ili uweze kupambana na kupanda Mara kushuka kwa mabadiliko ya ulimwengu wa biashara ni lazima uwe na sababu ambayo siyo kirahisi utakuja kukata tamaa kwenye ndoto zako ulizo nazo.sababu ni muunganiko wa kwanini "nataka" baasi lazima utafute kwanza za kwanini nataka kuwa tajiri? nataka kuwa tajiri nisifanye kazi maisha yangu yote,nisiajiriwe,napate mda wa kutulia na familia yangu,niwe huru ,na baada nichangie chochote katika ulimwengu huu Mimi kama Mimi.kama tayari uko na sababu mkubwa kama hizo twende hatua nyingine.

*kuwa na utamvulisho(have an identity)

katika ulimwengu wa biashara na utajiri mtu yeyote lazima awe na utambulisho ambao utamfanya atambulike kama mwekezaji au mfanya biashara katika ulimwengu huo,ifahamike kuwa tunapo sema utambulisho ni kwamba wewe unafanya biashara gani au wewe unafani gani je wewe ni mwanamuziki,je unaimba nini bongo freva au hiphop?je wewe ni mkulima unalima nini ?je wewe ni mwandishi unaandka nini?yaani kile unacho kifanya katika uwanda wa biashara ndicho tunasema utambulisho wako,yaani jamii inakutambua kwa kipi hasa hasa jamii tunayoizungumzia hapa ni jamii katika ulimwengu wa biashara je inakutambua kwa kipi hicho ndicho tunasema utambulisho wako wewe katika ulimwengu wa biashara je tayari unautambulisho katika ulimwengu huu tusonge mbele!? ok naendelea kukufanya tajiri!

*mipango(combined plans)

lazima ili uweze kuwa tajiri uwe na muunganiko wa mipango katika kile unacho kifanya, hakikisha mipango yako inafata kile ulicho kipendekeza kuwa ndicho utakitumia kukutambulisha kwenye ulimwengu wa kifedha weka mipango yako ukilenga kufikia sehemu pakubwa kwa kile unacho kifanya kama tayari umeweka mipango yako naomba unifuate hata hadi hatua nikupeleke kwenye mafanikio.

*onyesha vitendo(action)

sasa hii ndio hata muhimu matajiri wengi huificha kwa nguvu zote,unajua Mara nyingi watu wamekua wakitamani kuwa matajiri lakini inapofikia sehemu ya kuweka mipango yao katika vitendo wanafeli sasa Leo hii ndio mwisho wa hilo tatizo kwa wa Tanzania wote watakao ipata hii nasema hivi, kama umekua na mipango isiyo kuwa na vitendo hautokuja kuwa tajiri kamwe na hautopenda kusoma elimu hii tena maishaini lakini wewe usikate tamaa.ili uweze kuweka mipango yako katika vitendo na uanze kuingiza pesa hebu Fanya kile unachokipenda toka moyoni mwako na usimwamini yeyote katika hicho na ujue kuwa changmoto zipo ila utakabiliana nazo kulingana naulivyo andaa mipango yako. Aitambulike kuwa matajiri wote duniani wanafanya kwa vitendo kile walicho kipanga kiwe na kwa kuwa wanaamini akili zao basis nakweri kinakuwa.kama umeshaweka mipango yako kwenye vitendo naamini sasa uanaingiza kipato chako na hata kama bado basis unategemea kuanza kuingiza pesa zako vizuri kutoka vitega uchumi ilivyo vianzisha basi nakukaribisha katika ulimwengu huu wa mabillionare wala ucjari acha tuendelee.

*jua pesa mini(know what is money).

baada ya we we kuwa rasimi uko na utambulisho au kitega uchumi chako sasa naanza rasmi kukufundisha kuhusu pesa inavofanya kazi kwanza lazima ujue kuwa pesa nini?watu wengi sana duniani wamekuwa wakijiuliza ivi pesa nini ? na wamekosa mjibu hatimaye wameingia kwenye kudanganyana kuwa pesa eti ni" noti au sarafu iliyo kubalika ktk jamii ya nchi Fulani itumike ktk mbadilishano wa kibiashara" huu ni uongo na siku zote nitaupinga Mimi ,ndugu yangu Mimi nakwambia Leo kuwa matajiri peke yako ndio wanao jua maana halisi ya neno "pesa"nataka niseme hivi duniani kila mtu amezaliwa na pesa kichwani ila bado hajapewa macho ya kuziona ambayo ni elimu ya kifedha,nasema hivi pesa ni kitu kisicho shikika na hakionekani kwa macho ya kawaida(necked eyes)Bali pesa ni wazo (ideal).hivyo basi mtu yeyote atakae chagua kuwa tajiri naye atakuwa na yule atakaye chagua kuwa masikini naye atakuwa.kwa sababu mtu anaweza kuwa professor mkubwa lakini akawa kilaza bila ya yeye kujua kama ni kilaza kwenye ulimwengu wa pesa ndo maana utakua anang'ang'ania mdaraka au wadhifa frani kwa sababu hajui jinsi pesa zinavyo Fanya kazi ili kutengeneza pesa lakini matajiri ndio watu pekee wanaojua pesa nini na inafanya kazi vipi kuzalisha pesa zaidi nazaidi kama tayari umepata uelewa kuhusu pesa nini acha nikupe hii inayo fata.

*tengeneza pesa(create money)

hii ni sehemu ambayo kila MTU hujikita pasipo kujua anachokitengeza ni pesa au yeye ndo anatengenezwa pesa na wanaotengeneza pesa!!.sasa epuka kutengeneza kitu usichokijua kwanza kijue alafu ndo kutengeneza ndipo utaweza kukitengeneza.kuna watu wameleta misemo isiyo na maana katika jamii ya ulimwengu wa biashara moja kati ya misemo hiyo ni "fursa haiji Mara mbili" katika ulimwengu wa biashara tunasema hivi fursa hutengenezwa kwahyo kama fursa inaweza kutengenezw basi inaweza kuja Mara mia zaidi kadri mtu anavyoitengeneza mwenyewe hata tukija kwa upande wa pesa nayo pia hutenezwa na MTU mwenyewe. kwanza ifanye pesa yako itiririke(flow) iruhusu kuflow na kamwe usiizuie kokote iendako ila ile maelekezo na uijurishe kuwa ikienda ikakuletee kiasi frani kuna watu wanafanya biashara lakn pesa zao wanziogopa kuzituma badala take zenyewe zinawatuma kwenda kifanya kazin pahala ili waongezee zingine Hakka nasema hautaweza kuzifanya ziwe nyingi kwa mfumo huo kwani utakua haupo huru na pesa zako ili uweze kutengeneza pesanyingi zaidi lazima uzitwale kwanza hizi ulizonazo lakini usizitawale kwa kuzituma zikafanye maovu no Bali zitawale kwa kuzifanya zikakuletee pesa wenzake kupitia utambulisho wako au kitega uchumi chako ulichojichagulia Mara zote buni miradi mingi zaidi ili kujipanulia uwanda wa wewe kuingiza pesa nyingi zaidi kumzidi mwingine.

*chagua marafiki wa aina yako(choose friends of your favour)

Mara nyingi marafiki wanamchango mkubwa katika mafanikio yako jitahidi uwe na marafiki ambayo wanweza kukushauri kitu kizuri au basi nao wawe kama wewe ulivyo yaani wawe wafanya biashara wenzio usijaribu kumchagua MTU ambayo so wa aina yako akawa lafiki yako hamtafikia mbali kifedha,matajiri Mara nying huchugua marafiki ambayo hufanya nao kazi au biadhara na hvyo wanashauliana kuhusu maswala ya pesa.kama tayari zko pia ni wafanyabiashara basi nyote nawapelekeni kwenye ulimwengu wa pesa kupitia siri hizi

*pata pesa bure(get money for free)

matajiri walio duniani wanitumia njia hii ya kujipatia pesa bure pasipo na kutoa chochote kwa mfano wanatangaza kamali kama vile mkekabet,mzuka jackpot na kamali nyingine nyingi lakini pia wanatumia miamala kama inayo Fanya na kampuni la voda (m.pesa),Airtel(airtelmoney),tigo(t.pesa)pamoja na halotel(halopesa) hawa wanakijua kitu kinaitwa "get money for free" kila wewe unapofanya muamala wanapata pesa he wap wamekupa nini jiulize hapo au unapo bet wap wanapata pesa wewe uanpata nini basis nawewe tumia njia zile zile za kupata pesa pasipo na chochote kikubwa tumia akili yako kubuni njia za kuapta pesa bila kutoa chochote kwa kuanzisha vitega uchumi vitakavyo hitaji watu watoe pesa bila ya wewe kuwapa chochote.

*tafuta mawazo mapya(look for new ideas)

Mara zote matajiri wanayajua mapungufu yao na kugundua kuwa wasipo kuwa na mawazo mengi na mapya huenda wakaupoteza utajiri wao kutoka na mabadiliko mengi yanayoendelea kutokea katika masoko wanako uza bidhaa zao lakini pia mawazo nayo kibiashara huwa yanaishiwa muda wake ndo maana ni lazima ubadilishe badilishe mawazo kutoka kwawafanya biashara wenzio au huzuria seminar zinazofundishwa maeneo karibu ulipo au soma vitabu vya kifedha ili upate zaidi.

*fikiria kikubwa(think big)

matajiri walio wengi duniani hufikiria pakubwa sana na kuwa na maono ya mbali katika maisha yako kama kweri unahitaji kuwa tajiri basis lazima ufikirie kitu kikubwa kitakachokuja milikiwa na wewe au kufikiwa kulingana na ndoto zako pamoja na juhudi zako mwenyewe.hata kama ulichonacho nikidogo lakini amini kuwa siku moja utakuja kuwa nacho kikubwa Mara nyingi wanaofikiria kdogo hupata kdogo wakati wanaofikiria kikubwa hupata kikubwa kulingana na juhudi zako.

*tumia asset kununua vitu vingine(liability)

matajiri wote duniani hawachukui pesa zao kununulia magari ya kutembelea,vitu vya ndani,nyumba,pamoja na vitu ne visivyo tengeneza pesa Bali wanachokifanya ni kuanziasha kitega uchumi alafu ndo kikisha Alisha pesa yeye ndo anachukua zile pesa ananunua vitu hvyo (luxury) ilikuepuka anguko la biashara zake sasa sisi huku tulip wengi tunaenda kukopa benk alafu tunanunua magari at kutembelea jarafu wakija Benji kudai hela yako wankuta MTU hana hata mia ndo wanchukua nyumban mwisho wake MTU anarudi tens katika haali yake ya umasikini kwa sababu ajui pesa zinafanyeje kazin kumletea pesa nyingi zaidi kwahyo epuka hili.

*hudhuria semina,mafundisho na soma majrida ya kifedha.
yawezekana ikakuchujua mda kujifunza kupitia smina mbalimbali za kifedha lakini hakika utajifunza vingi vitakavyo nunua maisha yako kwa mabilion ya pesa.

*toa nawe utapata(give and you shall receive)
matajiri walio wengi huamini kuwa ukitoa basi lazima utapata kama uantaka pesa to a pesa kwanza nawe utapata hizo,kama unataka huduma basis to a kwanza huduma nawe utapata hiyo,na kama unataka tabasamu basis tabasamu kwanza wewe ndio utapata matabasamu mengi zaidi kutoka kwa watu wanao kuzunguka basi we we kama kwer unandoto za kuwa billionaire usiahau kutoa ili upate kikubwa zaidi.

ikumbukwe kuwa kwa Leo nimewaletea siri namba moja ya utajiri ambayo matajiri wote dunia mzima wanayo na wanaitumia je wewe pia nataka kuwa tajiri!??basi ndelea kunifatilia kwa umakini mkubwa upate kuwa mmoja kati ya wale wamiliki pesa..ewe kijana dunia inakusubiri hebu Fanya kitu kwaajili ya dunia yetu usisubiri tu dunia ikufanyie,endelea kunifatilia nikufundishe mambo adimu na baada ya hapo itafuata siri naomba mbili.............................(64+56)
 
Sijaisoma nasubir nipate lunch kabisa ndo nianze neno kwa neno
 
Jaribu kuzingatia matumizi ya R na L naona yanakushinda kabisa.
Pili jaribu kuweka vituo. Andiko ni zuri ila nimesoma kwa shida sana hadi kichwa kinauma.
 
Back
Top Bottom