Siri za kufanikiwa chochote unachotaka

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KWANINI katika maisha kuna watu wengine hawafanikiwa na wengine wanafanikiwa? Ni swali ambalo limekuwa likiumiza vichwa vya wengi.

Wapo ambao wanawianisha mafanikio ya mtu na elimu, lakini hiyo haina ukweli sana, japo kuna watu ambao mafanikio yao yametokana na elimu waliyonayo. Kusoma au kutosoma kwa maana ya kupata elimu ya kutosha siyo ile ya kufuta ujinga haina maana kwamba mtu atakuwa na maisha mazuri au atafanikiwa katika maisha au laa.

Tunasisitiza kuwa elimu ni muhimu sana katika masiaha ya sasa. Lakini hiyo unaitumia vipi hilo ndilo suala au jambo la msingi sana ambalo wengi wanashindwa kulitambua. Kutokana na kushindwa kujua hilo wengi huishia kutoa wasifu wa viwango vya elimu.

Aah! Unajua mimi nimesoma na Rais wenu… alikuwa kilaza sana, mara oooh usinione hivi nimesoma sana, nimetembelea nchi nyingi sana hapa duniani au aaah… nimeonana na wakubwa wengi katika dunia hii na mengine kama hayo.

Kila mtu anapenda kufanikiwa, anapenda maisha mazuri, lakini si wengi wanatimiza azma hiyo. Kwanini? Kuna sababu nyingi, lakini kubwa ni woga wa kuthubutu kujaribu kufanya jambo fulani.

Je wewe una shauku ya kufanya nini? Yawezekana unataka kuwa na biashara kubwa, unataka kujiajiri na hata uajiri wengine, basi acha woga.

Wengi wanaishi katika hofu na kuamini kuwa maisha bofra yako katika ajira ya mshahara pekee. Siyo kweli. Thubutu utaona jinsi unavyoweza kupiga hatua kubwa na tena ya ajabu. Usichelewe.

Kushindwa kuthubutu kunaashiri mwisho mbaya wa maisha yako hapa duniani na hasa kama hutakuwa na mradi wowote wa kukuongezea kipato zaidi ya mshahara wako.

Watafiti wengi duniani wanabainisha kuwa yeyote ambaye anaishi kwa kutegemea ajira pekee, lazima atakuwa na hali ngumu, kwani baada kustaafu atapata mafao yake na kukaa nyumbani akicheza na wajukuu au kukaa tu tofauti na aliyekuwa na mradi baada ya kustaafu ataendelea na biashara yake na kipata hakitabadilika sana.

Msingi wa kuwa na mafanikio kwa chochote unachotaka ni kuthubutu, ni lazima kutafakari namna ya kujiajiri. Ni lazima ujiulize kama wengine wameweza kuniajiri, kwanini siku moja na wewe usiajiri watu wa kukufanyia kazi? Kwani wao ni akina nani hadi waweze na wewe ushindwe? Tafakari, chukua hatua.

Ukweli ni kwamba msingi wa mafanikio yetu kwa asilimia 99 unatokana na kufanya kazi kwa bidii, na asilimia 1 ni bahati. Ndio kusema usitegemee kufanikiwa kwa misingi ya bahati, fanyakazi kwa bidii na umakini.

Je kuwa na fedha ndio msingi wa mafanikio? Hapana, huo ni uongo. Fedha, si ufunguo wa mafanikio, ingawa ni kigezo muhimu sana katika uanzishwaji wa biashara na mambo mengine.

Hapa tunajifunza kitu kingine kwamba kuzaliwa kwenye familia maskini au tajiri, haina maana kwamba utakuwa tajiri au maskini. Kuna watu wamerithi fedha au mali lukuki lakini wakaishia kuwa masikini wa kutupwa kwa kjukosa maarifa ya kuzisimamia.

Ni ujinga mkubwa kwa mtu hasa kijana kuringia mali za wazazi wake, badala yake anapaswa kujifunza namna ya kutafuta zake.

Je kuwa na uzoefu na jambo fulani ndio huleta mafanikio? Hapana. Lakini pia ni kweli uzoefu unaweza kumfanya mtu kufanya kazi kwa mafanikiotofauti na asiyekuwa na uzoefu.

Uzoefu ni siagi kwenye mkate!
Kufanya kazi kwa bidii ni muhimu kwa mafanikio? Jibu ni NDIYO. Hakuna mafanikio pasipo kufanya kazi kwa bidii.

Mafanikio yoyote ni matokeo ya moja kwa moja ya masuala mengi lakini lililo kubwa ni ile ya kufanya kazi kwa bidii, umakini na kutumia fedha kwa uangalifu wakati wote.

Pamoja na kufanyakazi kwa bidii, kazi lazima ifanywe kwa kushirikiana na wengine kwani tunaishi kwa kutegemeana, usimdharau mtu kutokana na hali yake unaweza kupata kitu ambacho wewe huna.

Kila mara jibidiishe na kupata elimu mpya. Elimu haina mwisho. Tafuta elimu wakati wote itasaidia kukuweka sawa katika kuendesha shughuli zako kisasa na kwa mafanikio zaidi.

Ili kufanikiwa ni lazima uwe na kiu ya kujifunza, uwe na kiu ya kusoma vitabu vinavyohusiana na ujasiriamali na siri za mafanikio.

Kwa ushauri zaidi piga 0653777700,http://dismaslyassa.com
 
Mkuu Kilimasera, first impression is the deepest!
Pamoja na contribution yako , avatar yako inakuonyesha kama mtu asiye serious on anything!!
 
Kila mtu anapenda kufanikiwa, anapenda maisha mazuri, lakini si wengi wanatimiza azma hiyo. Kwanini? Kuna sababu nyingi, lakini kubwa ni woga wa kuthubutu kujaribu kufanya jambo fulani.

Je wewe una shauku ya kufanya nini? Yawezekana unataka kuwa na biashara kubwa, unataka kujiajiri na hata uajiri wengine, basi acha woga.

Wengi wanaishi katika hofu na kuamini kuwa maisha bofra yako katika ajira ya mshahara pekee. Siyo kweli. Thubutu utaona jinsi unavyoweza kupiga hatua kubwa na tena ya ajabu. Usichelewe.

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.
Tatizo kubwa ni mtu kukosa uelekeo wa kimaisha na kufikiri kuwa ili kufanikiwa ni lazima kuajiriwa katika sehemu yenye mshahara mzuri.
Wengi wanakosa ujasiri wa kuanzisha mradi kwa kujitoa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Kwa walio ajiriwa serikalini na mashirika ya umma mtido wa kujiongezea kipato ni njia za ujanja ujanja na ambazo si halali eg visafari visivyo na ulazima, warsha na makongamano etc.
Ukijiajiri jipe muda wa sana sana miaka mitano ya kazi ngumu na baada ya hapo ni lazima mafanikio yatajitokeza.
 
Katika jamii yetu watu wengi wanakuwa na mawazo kuwa kuajiriwa ndio mwisho wa kila kitu wakati si kweli, na pia nakubaliana kuwa mafanikio ya mtu hayatokani na elimu aliyonayo...
 
elimu hata siku moja sio kigezo cha maendeleo watu wengu hawakusoma lakini wameweza kujitajilisha kutokana na mbinu zao tu kiakili na uwezo binafsi wa kufikiri tofauti na elimu ila tatizo la tanzania kwamba misingi yetu sehemu kubwa upande wa elimu tumeelekeza zaidi kwenye kuajiliwa na ndio maana kila anaemaliza chuo anaanza kutafuta kazi badala ya kutafuta namna ya kujiajili!!kumekua na utitiri wa taasisi nyingi za fedha kwa sasa ambazo hutoa mikopo ya fedha kwa raia wengi wa tanzania lakini wamekua wakishindwa kuziendeleza capital hizo na kuishia kudaiwa madeni tu kutokana na kutokua na ujanja wa kubuni mambo mbadala ambayo yangesaidia kuwainua kimaisha mie nadhani cha muhimu na kukubwa hapa serikali nayo iangalie system nzima ya elimu ilenge zaidi kwenye kujitegemea na sio kutegemea kupata ajira!
 
Kivipi mkuu?? mbona ilikuwa haina noma au kwa vile alikuwa ni .......:tape:

Sasa ile nyengine ulimi umetokeza kama mjusi bana, huoni alikua amekaa ki....! Anyways ngoja nichangie kwenye mada!!

Kwa binafsi nilikuwa katika ajira karibia miaka saba, nikaamua kununua biashara iliyo kwenye fani yangu...kwa malengo ya kujiajiri na kuajiri watu...nilifanya biashara hii kwa miaka miwili lakini matokeo hayakua mazuri...mtaji umekufa, na madeni yamenikaba...sina budi kurudi kwenye ajira...ila tu nisema nitajaribu tena mambo yakiwa mazuri....

Muhimu ni kwamba unapoamua kujiajiri ni vizuri kufanya kautafiti kidogo, usikurupuke!!!
 
kingwendu ngwendulile
Sasa ile nyengine ulimi umetokeza kama mjusi bana, huoni alikua amekaa ki....! Anyways ngoja nichangie kwenye mada!!

Kwa binafsi nilikuwa katika ajira karibia miaka saba, nikaamua kununua biashara iliyo kwenye fani yangu...kwa malengo ya kujiajiri na kuajiri watu...nilifanya biashara hii kwa miaka miwili lakini matokeo hayakua mazuri...mtaji umekufa, na madeni yamenikaba...sina budi kurudi kwenye ajira...ila tu nisema nitajaribu tena mambo yakiwa mazuri....

Muhimu ni kwamba unapoamua kujiajiri ni vizuri kufanya kautafiti kidogo, usikurupuke!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom