Siri ya Wanawake kuficha mateso ndani ya ndoa

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,883
5,188
Manyanyaso kwenye ndoa limekuwa jambo la miaka mingi, kiasi kama limeonekana ni kawaida. Na muhanga mara nyingi huwa ni mwanamke, sababu kuu ni kuwa Unyanyasaji huusisha nguvu za kimwili na kiuchumi, ambazo zote ziko mikononi mwa mwanaume. Na Unyanyasaji uko wa namna mbili, wa kihisia na kimwili.

Wengi tunazungumzia zaidi Unyanyasaji wa kimwili(Physical abuse), lakini wapo wanawake ambao hawapigwi, lakini wanateswa sana kihisia—matusi, kejeli, udhalilishaji n.k! Suluhu la yote ni mwanamke kuwa na nguvu kiuchumi na kielimu na kuacha dhana kuwa yeye ndiye mwenye wajibu wa kuvumilia manyanyaso ili ndoa idumu. Ndoa ni taasisi muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu, lakini si jambo la lazima.

Muhimu: wapo pia wanaume wanaoteswa na wake zao.

================

AdobeStock_178622128.jpg
Elizabeth Edward
“Jamii yetu inatakiwa kuacha kuwalaumu wanawake pale ndoa inapovunjika na kwa nini wanawake walaumiwe. Hatumsaidii mtu kwa kumdhihaki pale ndoa yake inapofikia mwisho, na ndiyo sababu wapo wanaoendelea kuwapo kwenye ndoa zenye machungu, ukatili na maumivu.’’

Hiyo ni sehemu ya ujumbe uliotikisa mtandao wa kijamii wa Instagram wiki iliyopita kutoka kwa mwanamitindo, Flaviana Matata.

Flaviana, alifunga ndoa Julai 16, 2015 , hata hivyo ndoa hiyo ilidumu kwa miaka michache kabla ya kusambaratika.

Novemba 16, mwaka huu mwanamitindo huyo alivunja ukimya na kueleza kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake, baada ya kusikiliza mahojiano ya mwanamuziki Adele wa Marekani na mtangazaji Ophrah Winfrey.

Katika mahojiano hayo Adele alieleza kuhusu ndoa yake kuvunjika huku akiweka wazi kuwa ilivunjika ndani ya mwaka baada ya kuolewa, hali iliyomfanya kujisikia vibaya.

Kupitia ukurasa wa Instagram Flaviana alieleza kuguswa na namna Adele alivyofunguka kuhusu ndoa yake na alikwenda mbali zaidi na kueleza masikitiko yake kwa namna wanawake wanavyolaumiwa na kubebeshwa mzigo pale ndoa inapovunjika.

image001.jpg
Aliandika: “Kabla ya kumdhihaki mtu kwa ndoa yake kuvunjika tafadhali jaribu kumhurumia. Hakuna anayefunga ndoa ili baadaye ikavunjika. Nikizungumzia kwa upande wangu, tulitalikiana mwaka 2019 na mitandao haikunipa nafasi ya kupumua, ilikuwa ni kama nimeua mtu.

“Nipo katika nafasi nzuri kwa sasa naweza kupumua. Nashukuru kwa watu wangu wa karibu kuwa pamoja na mimi. Ni wengi kati yetu tunachagua kuficha maumivu.

‘‘Watu wa mtandaoni wanaweza kuwa wakatili na hii ndiyo sababu wengi wanashindwa kuweka wazi wanayoyapitia isipokuwa wachache wenye werevu.”

Kauli ya Flaviana iliungwa mkono na mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Noela Godfrey, ambaye alieleza ugumu aliopitia baada ya kuachana na mume wake na kupata talaka.

“Kuna shida kubwa kwenye jamii yetu, hii dhana ya kwamba ndoa ikivunjika basi anashambuliwa mwanamke tutaendelea kushuhudia mauaji ya kikatili kila kukicha.

Binafsi naamini ndoa ni makubaliano ya wawili, pale inapofikia hatua unaona hamuwezi tena kuwa pamoja, ni vyema kuachana.

Sasa inapotokea hivyo lawama zinashushwa kwa mwanamke kwamba sio mvumilivu mara hawezi kumtunza mume, utamlazimisha mtu avumilie unajua anapitia nini huko ndani? Wanawake wengi wanateseka kwenye ndoa kwa kuhofia maneno ya watu au watawaacha vipi watoto,” alisema Noela.

Wanasaikolojia

Mshauri wa masuala ya uhusiano, Deogratius Sukambi alieleza kuwa licha ya ukweli kwamba, jamii huwalaumu wanawake pale ndoa inapovunjika, lawama hizo huanzia kwao wenyewe kutokana na namna walivyotengenezwa na kuaminishwa kuwa wana dhamana kubwa kwenye ndoa.

Alisema suala la wanawake wenyewe kujiona wana hatia, ni tatizo kubwa kuliko lawama zinazotoka kwenye jamii.

“Sababu kubwa inayowafanya wanawake wajione wanalaumiwa ni kutokana na ukweli kuwa wao wenyewe wanajilaumu kwa yale yanayotokea kwenye ndoa. Hili lipo hadi kwenye masuala ya kiimani; mwanamke anaonekana kubebeshwa jukumu la uhusiano na kuonekana kwamba ana dhamana kubwa kuhakikisha ndoa inakuwa na hatima njema zaidi.

“Tamaduni nyingi pia zinamuona mwanamke kama mtu anayeshikilia hatma ya familia na ndoa, huku mwanaume nguvu yake ikiwa kwenye eneo la kiuchumi,’’ anasema.

Anaongeza: ‘‘Kwa hiyo tamaduni zinamtazama mwanamke hivyo. Sababu nyingine ni malezi; wanawake wengi wanalelewa kuhakikisha wanaubeba kwa uzito mkubwa mustakabali mwema wa uhusiano.

Kwa upande wake, mwanasaikolojia Saldeen Kimangale, anabainisha kuwa kinachowaathiri wanawake kushindwa kusonga mbele, ni maana wanayoijenga juu ya ndoa na talaka kwa kuzingatia mtazamo wa watu na jamii.

Alishauri mafundisho kuhusu ndoa na yatazamwe upya au yafanywe na watu weledi zaidi wenye kumzingatia mwanadamu kama kiumbe huru mwenye mwili na roho na kwamba ndoa ni kukamilishana na wala sio kushindana.

“Wanandoa wanapoachana mwanamke hubebeshwa jukumu na lawama zote kwa sababu jamii yetu imemuandaa hivyo; uvumilivu, subira, unyenyekevu, ni mahubiri atakayopewa mwanamke, kuvunjika kwa ndoa maana yake mwanamke ameshindwa kufanyia kazi mahubiri hayo hivyo, anastahiki lawama zote,’’ alisema.

MWANANCHI.

Screenshot_20211122-093613.jpg
 
Tatizo kubwa kwa sasa hasa mijini ni pale ndani ya ndoa kila mtu anataka kuwa juu.. tunasahau kuwa kila mtu ana nafasi yake.. mwanaume ni kupenda mke na mwanamke ni kumtii mume.. kila mtu atimize wajibu wake bila kuangalia hali ama kipato kati yenu...sasa linapokuja hili suala la haki sawa ndio linaharibu kabisa..
 
Tatizo kubwa kwa sasa hasa mijini ni pale ndani ya ndoa kila mtu anataka kuwa juu.. tunasahau kuwa kila mtu ana nafasi yake.. mwanaume ni kupenda mke na mwanamke ni kumtii mume.. kila mtu atimize wajibu wake bila kuangalia hali ama kipato kati yenu...sasa linapokuja hili suala la haki sawa ndio linaharibu kabisa..
Kwani kaka inaposemwa haki sawa kwenye ndoa kwako lina maanisha nini?
 
Manyanyaso kwenye ndoa limekuwa jambo la miaka mingi, kiasi kama limeonekana ni kawaida. Na muhanga mara nyingi huwa ni mwanamke, sababu kuu ni kuwa Unyanyasaji huusisha nguvu za kimwili na kiuchumi, ambazo zote ziko mikononi mwa mwanaume. Na Unyanyasaji uko wa namna mbili, wa kihisia na kimwili. Wengi tunazungumzia zaidi Unyanyasaji wa kimwili(Physical abuse), lakini wapo wanawake ambao hawapigwi, lakini wanateswa sana kihisia—matusi, kejeli, udhalilishaji n.k! Suluhu la yote ni mwanamke kuwa na nguvu kiuchumi na kielimu na kuacha dhana kuwa yeye ndiye
Hao celebrities wanaishi kwenye ndoa za utopian life, ndoa ni mapambano baina ya pande mbili, huwezi kupata na kuishi kwenye ndoa on a sliverplate, akili ya mtu yoyote hupimwa kwa uwezo wake wa kutunza ndoa yake, au kutoka peacefully kwenye ndoa yenye mgogoro bila kuumizana. Women are not easy to handle hao viumbe hawaeleweki kabisa
 
Hiyo picha ya mwishoni ndoa yao yenyewe nimepitia misukosuko sana hapo mwanamke anavumilia ili heshima kwenye jamii isishuke.
 
Hao celebrities wanaishi kwenye ndoa za utopian life, ndoa ni mapambano baina ya pande mbili, huwezi kupata na kuishi kwenye ndoa on a sliverplate, akili ya mtu yoyote hupimwa kwa uwezo wake wa kutunza ndoa yake, au kutoka peacefully kwenye ndoa yenye mgogoro bila kuumizana. Women are not easy to handle hao viumbe hawaeleweki kabisa
 
Ilikuwa ni mvumilivu hula mbivu but now imekuwa mvumilivu huambulia kifo
 
Back
Top Bottom