Siri ya ushindi wa CCM!

Viva forever

Member
Feb 28, 2017
18
14
224993d081aba66cddd0f0017c1fd39b.jpg

Kwa muda mrefu chama cha mapinduzi (ccm) kimeonekana kuiongoza hii nchi kwa ushindi wa kupigiwa kelele. Chama hiki kilicho zeeka, kimeendelea kuishika nchi kwa mitindo na mbinu mbalimbali za panya na kuwaacha wapinzani midomo wazi wasijue wameibiwa wapi au wapi wamepigwa. Kila kitu kina mwisho na mwisho wa ccm ndio huu, kaa mkao wa kula!

Mbinu wanazo tumia ccm ni za kisayansi sana, huwezi jua Kama poyoyo! Tangu uhuru wa vyama vingi ulipoanza, ccm haikuwahi kushinda mpaka leo hii. Mbinu ni kali na vita ni kubwa na vitisho hata ikibidi kuua. Wanalinda kubaki madarakani zaidi na wanavyolinda mipaka ya nchi.

SIRI YA KADI YA MPIGA KURA!
Juzi nilipokea taarifa za kiintelijensia toka kwa mwananchi mmoja jijini, akilalamika kuwa kuna watu wanaosemekana ni watu wa ccm. Watu hao walikuwa na kazi ya kuwashawishi wananchi wawauzie vitambulisho vya kupigia kura kwa sh 5000 za kitanzania! Inasemekana watu hao wanachohitaji ni namba tu ya kitambulisho cha Mpigaji kura kwa dau la tsh 5000!

Wana ukawa na wapenda demokrasia na amani kwa ujumla, hii ishu chafu! Ukiona kiongozi ana muelekeo wa kiimla, tambua hakushinda kidemokrasia bali kwa mkono wa chuma.

MBINU MPYA NINI CHA KUFANYA??
1.Kuwa makini na wasajili wa laini za simu -watu hawa wengine wamewekwa spacial kwa kazi za ccm na huwezi kuwajua. Wanachofanya ni kuhitaji kitambulisho chako chochote zaidi ni kile cha kupigia kura. Wanachukua na kukopi jina na namba maalumu ya kitambulisho na kuondoka nazo. Hizo ndizo kura feki za watanzania zinazoipa jeuri ccm!! Jeuri kuwatesa watu, jeuri ya kufanya wanachotaka bila kuogopa yeyote katika hii nchi.

Kiongozi wa nchi anaposimama madhabahuni na kusema MFE TU SINA UWEZO WA KUWALISHA au KUWAJENGEA NYUMBA! Just imagine anaoongea nao ni wale wale walio muwezesha kuiyona ikulu na kula bata na familia yake miguu juu! Hii ni jeuri ya goli la mkono!

Mkono wa chuma! Kesho tena atapanda ktk madhabahu na kuwaomba watu haohao wamuwezeshe. Zipo mbinu nyingi za ccm kuing'ang'ania nchi ila hii, itakusaidia kukuweka makini. CCM imeanza kampeni jamani, tena mchana kweupe pee! Wameanza tabia chafu mapema hadi watoto wanaona! Watu wa UKAWA, mtalia sana hata msiiyone kesho Kama hamtotoa boriti machoni mwenu.

Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano siku hiyo, kuliko ccm kushinda uchaguzi ujao!! AMINI NAKUAMBIA, CCM ILISHA KUFA ILA UHAI BANDIA UNAIFANYA ITAMBE LEO HII KWA JEURI.
 
Sioni kama Kuna mbinu mpya uliyoifichua, yote uliyoandika hapo ni ya kizamani Sana.
CCM kuiba ni kweli wanaiba tena 2015 walizidiwa kete na Ukawa tena walibanwa kweli kweli kwa kila njia, wakaona wakomae na IT pamoja na vijana wa Ukawa waliokua wanakusanya matokeo Kitaifa ndiyo ikawa pona pona Yao.
 
224993d081aba66cddd0f0017c1fd39b.jpg

Kwa muda mrefu chama cha mapinduzi (ccm) kimeonekana kuiongoza hii nchi kwa ushindi wa kupigiwa kelele. Chama hiki kilicho zeeka, kimeendelea kuishika nchi kwa mitindo na mbinu mbalimbali za panya na kuwaacha wapinzani midomo wazi wasijue wameibiwa wapi au wapi wamepigwa. Kila kitu kina mwisho na mwisho wa ccm ndio huu, kaa mkao wa kula!

Mbinu wanazo tumia ccm ni za kisayansi sana, huwezi jua Kama poyoyo! Tangu uhuru wa vyama vingi ulipoanza, ccm haikuwahi kushinda mpaka leo hii. Mbinu ni kali na vita ni kubwa na vitisho hata ikibidi kuua. Wanalinda kubaki madarakani zaidi na wanavyolinda mipaka ya nchi.

SIRI YA KADI YA MPIGA KURA!
Juzi nilipokea taarifa za kiintelijensia toka kwa mwananchi mmoja jijini, akilalamika kuwa kuna watu wanaosemekana ni watu wa ccm. Watu hao walikuwa na kazi ya kuwashawishi wananchi wawauzie vitambulisho vya kupigia kura kwa sh 5000 za kitanzania! Inasemekana watu hao wanachohitaji ni namba tu ya kitambulisho cha Mpigaji kura kwa dau la tsh 5000!

Wana ukawa na wapenda demokrasia na amani kwa ujumla, hii ishu chafu! Ukiona kiongozi ana muelekeo wa kiimla, tambua hakushinda kidemokrasia bali kwa mkono wa chuma.

MBINU MPYA NINI CHA KUFANYA??
1.Kuwa makini na wasajili wa laini za simu -watu hawa wengine wamewekwa spacial kwa kazi za ccm na huwezi kuwajua. Wanachofanya ni kuhitaji kitambulisho chako chochote zaidi ni kile cha kupigia kura. Wanachukua na kukopi jina na namba maalumu ya kitambulisho na kuondoka nazo. Hizo ndizo kura feki za watanzania zinazoipa jeuri ccm!! Jeuri kuwatesa watu, jeuri ya kufanya wanachotaka bila kuogopa yeyote katika hii nchi.

Kiongozi wa nchi anaposimama madhabahuni na kusema MFE TU SINA UWEZO WA KUWALISHA au KUWAJENGEA NYUMBA! Just imagine anaoongea nao ni wale wale walio muwezesha kuiyona ikulu na kula bata na familia yake miguu juu! Hii ni jeuri ya goli la mkono!

Mkono wa chuma! Kesho tena atapanda ktk madhabahu na kuwaomba watu haohao wamuwezeshe. Zipo mbinu nyingi za ccm kuing'ang'ania nchi ila hii, itakusaidia kukuweka makini. CCM imeanza kampeni jamani, tena mchana kweupe pee! Wameanza tabia chafu mapema hadi watoto wanaona! Watu wa UKAWA, mtalia sana hata msiiyone kesho Kama hamtotoa boriti machoni mwenu.

Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano siku hiyo, kuliko ccm kushinda uchaguzi ujao!! AMINI NAKUAMBIA, CCM ILISHA KUFA ILA UHAI BANDIA UNAIFANYA ITAMBE LEO HII KWA JEURI.
Wacha watawale tuu, maana wananchi wenyewe bado hawajachoka.Ila siku wananchi wakichoka, hakuna cha ccm wala cha lumumba.Kwa sasa ccm ipo madarakani kwa sababu wananchi wamekubali iwepo!!
 
Back
Top Bottom