Siri ya Ulegelege wa CCM

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Mimi ni mwana harakati ambaye daima napenda kuwa mkweli, kwa namna fulani nilitokea kuwakubali baadhi ya wabunge wa chama tawala, kwa kuwataja wachache ni pamoja na Ester Bulaya, Januari Makamba, James Lembeli , Deo Filikunjombe, Mwigulu Nchemba na wengine wengi ambao wapo kwaajili ya kutetea masilahi ya taifa hili.

Kwa lililotokea leo bungeni kwa Mwigulu Nchemba na mh. Komba nimegundua kuwa ccm imekuwa legelege kwa kipindi kirefu kulingana na watu walioaminiwa kukiongoza chama hicho kuwa na upeo mdogo sana, Leo hii Nchemba anajieleza yeye kuwa ni mchumi wa daraja A, lakini mambo anayoongea hata mtu asiyefika fomu IV awezi akaongea mambo kama yale.
Nchemba unadiriki kuudanganya umma kuwa to invest in human capital is a part of project investment, kilichomo kwenye mpango wa miaka mitano wa taifa ni kwamba angalau kila mwaka itengwe asilimia 35 kwaajili ya investment projects, wewe unatuambia tunasomesha watu ni sehemu ya lengo la kufikia asilimia 35 ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo.

Wewe kweli ni mchumi wa daraja A na mwandamizi wa BoT nchi hii na ccm mnaipeleka wapi ? mbona hatuwaelewi na nyinyi ndo mnaaminiwa kwenye chama kama vijana wasomi, huo kweli ndo uchumi wa daraja A ?

Ulegelege wa ccm umesababishwa na viongozi na wabunge wasioelewa kama Nchemba , naomba kuwasilisha
 
Bunge hili na Bajeti hii is another SILLY SEASON. Tundu Lisu ni Jembe na hekima kusifiwa na si Kujisifia nani kampa Daraja A tena bila aibu eti BOT ambako Ufisadi mkubwa umeikumba taasisi nyeti ktk nchi, Nchemba awe na haya! na abakishe ma neno ccm ndo hio iko ICU inapumua kwa msaada wa mashine 2015 lazima mashine itolewe kieleweke
 
Bunge hili na Bajeti hii is another SILLY SEASON. Tundu Lisu ni Jembe na hekima kusifiwa na si Kujisifia nani kampa Daraja A tena bila aibu eti BOT ambako Ufisadi mkubwa umeikumba taasisi nyeti ktk nchi, Nchemba awe na haya! na abakishe ma neno ccm ndo hio iko ICU inapumua kwa msaada wa mashine 2015 lazima mashine itolewe kieleweke

Nimeipenda hiyo kuwa 2015 mashine lazima itolewe ili jamaa aliyeko ICU a RIP
 
Aibu kijana kama yeye Mh M Nchemba kuaminiwa na CCM kuwa katibu wa Uchumi na Mipango....!
Bana Bongo yaan ktk CCM kila mtu kalala kisa Dola ipo 24 hr inawalindaaa...! daah Govt yote ipo goigoi imelala usingizi,
Wallaah 2015 mbona haufiki mapema...?
 
Kilichotokea leo Bungeni naomba rafiki na jamaa wa karibu wa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba wamwambie anawaibisha watanzania.Nilidhani ana akili timamu kumbe zilishakwisha.Mh aibu hata kwa nchi jirani kama walimsikia alivyoongea na kama wasomi wetu wako hivyo basi tumekwisha.
 
Hata mwenyekiti wao wa taifa ambaye anadai kasomea uchumi, alipoulizwa kwa nini Tanzania ni maskini, alisema hajui!! Huyu ndiye mzizi mkuuu wa ulegelege wa CCM.
 
Hakuna lolote na ccm na wamejisahau sana wanaona hakuna wakuwatoa hapo walipo milele na milele na pesa wanazochata zinawapa kiburi sana manake wanajua uchaguzi ukikaribia ili kurudisha imani kwa wananchi WANAWAONGA KWA PESA ,KOFIA,KANGA PAMOJA NA PROPAGANDA NYINGI NA AHADI ZA KUWALAGAI NA KUWASAULISHA MATATIZO YAO WALIYONAYO.
 
CHAMA LEGELEGE HUZAA SERIKALI LEGELEGE=NYERERE NA NDIO HII SERKALI YA AKINA MWIGULU POLENI SANA MNATOKWA NA MAPOVU WAKATI MECHI HAIJAANZA:decision:
 
Tz watu wenye vyeti pasipo elimu wanatamba sana, Mwigullu ni mmoja wapo. Shame on him and his party. Hata cheti bila elimu ni aibu ya CCM pia.
 
Ccm inatudhalilisha watanzania na
Hawa kina nchemba wanaongea utumbo
Mbele ya watanzania nasisi tunawaangalia tu
Hebu tuwachenchie siku moja huku
Mtaani watatia adabu mafisadi wakubwa hawa.
 
Yaan Nchemba anajisifia Kuwa ni mchumi wa daraja A????? tena eti wa BOT???? NDIO MAANA SIKU HIZI BOT IPO KAMA MICROFINANCE coz kama wafanyakaz wenyewe ni kama Nchemba kaziiii kwelikweli. Alete hoja sio A, mbona hata Bana ni Dr, lakini inatusaidia nn wananchi.
 
Back
Top Bottom