Siri ya Rais Magufuli kuhusu uteuzi yabainika

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,251
2,000
Imeelezwa kuwa siri ya Rais John Magufuli kufanya uteuzi wa Watanzania wataalamu wa ndani badala ya kuchukua wanaofanya kazi nje ya nchi, ni pamoja na msimamo wake wa kutolipa mishahara mikubwa lakini pia kuwatia moyo wasomi waliamua kubaki nyumbani.

Katika kipindi cha mwaka mmoja, Rais Magufuli ameonekana kuteua wataalamu na wasomi kutoka sekta binafsi na taasisi za umma ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), tofauti na mtangulizi wake Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliyeonekana wakati mwingine akichukua Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi.

Hata hivyo, wachambuzi wameeleza kuwa licha ya Watanzania wote kuwa na haki ya kufanya kazi nchini kwa sifa na vigezo vinavyohitajika, kinachotakiwa kuangaliwa ni uwezo na vipaumbele vya wataalamu wanapopatikana.

Miongoni mwa wachambuzi waliozungumzia mazingira hayo, Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa Repoa, Dk Abel Kinyondo aliyesema licha ya muda mfupi ambao amekaa madarakani, ni vyema Rais Magufuli kuchukua tahadhari katika uteuzi wake.
 

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,518
2,000
wasomi "madayasipora" ktk awamu ya JK,mkwere alijitahidi kuwapa mashavu,lakini mwishowe waligeuka kuwa wapigaji.

rejea historia ya alikoibuliwa pro.muhongo na kashfa kadhaa zilizo ibuka wizara ya nishati na madini wakati yeye akiwa waziri wa wizara hiyo.

kuna mmoja aliibuliwa toka marekani,akakabidhiwa wizara ya maliasili na utalii....inasemekana yeye ndio muhusika mkuu aliyehusika "kumpiga" faru john.
 

Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Wanayo practical experience? Kubana matumizi yapi? Je! Zile ndege bajeti yake imepitishwa na nani? Cost analysis ya uwanja wa ndege nyumbani ili fanyika? Tusidanganyane
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,713
2,000
Anaua UDSM na taasisi zingine za taaluma kwa kuchukua wanataaluma huko na kuwapa nafasi za kiutendaji kwenye mashirika ya umma ilihali tayari kuna uhaba wa academicians nchini.
 

J C

JF-Expert Member
Dec 12, 2013
2,636
2,000
Tunataka chanel zile za bure zirudishwe la sivyo waturudishie analogia yetu maana antena bado tunazo. Hii ni laana na unyonyaji mkubwa kwa kutaka kuwakamua maskini wa nchi hii kila walichonacho.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,132
2,000
Wanayo practical experience? Kubana matumizi yapi? Je! Zile ndege bajeti yake imepitishwa na nani? Cost analysis ya uwanja wa ndege nyumbani ili fanyika? Tusidanganyane
Kasome kitabu cha bajeti ya wizara ya ujenzi,mawasiliano na uchukuzi 2015/2016
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom