makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Katika gazeti la Mwananchi leo limetanabaisha kuwa Moshi mjini pamoja na kuwa chini ya upinzani kwa zaidi ya mwongo mmoja bado haijatetereka kiutulivu.
Kulingana na utafiti uliofanyawa na Waandishi wa Mwananchi ni kuwa elimu na uelewa wa Wananchi wa Moshi mjini uko kwenye asilimia 95(95%), ikifuatiwa na miji ya Arusha, Mbeya na Mwanza! Elimu na kujitambua kumbe ni siri kubwa ya maeneo yote ya upinzani.
Hii maana yake ni nini? Kuwa unapokuwa na watu wenye Elimu na ufahamu wa kutosha kususu maswala ya Demokrasia,Sheria na Katiba wanafanya vizuri sana kwenye swala la Utulivu na Amani.
Tatizo linakuja pale kunapokuwa na kiongozi mwendawazimu wa Serikali kama ilivyo kwa Mikoa ya Arusha na Mwanza ambako Ma-DC ma-RC wanapoamua kupambana na wapinzani kwa chuki zao binafsi kama ilivyo kwa Mrisho Gambo kwa Arusha mjini.
Mrisho Gambo au Paul Makonda huwezi kuwalinganisha na RC wa Kilimanjaro Mhe. Merck Sadik. RC mstahafu Bwana Muhogo Mulongo alikuwa ni aina yakina Gambo watu wanaopenda fujo na vurugu ili wajulikane wapo kwenye Utawala. Nina uhakika leo hii ukimleta Mrisho Gambo kuwa RC au DC wa Moshi Mjini zitaanza vurugu za kisiasa sasa hivi. Kama JPM anabisha na afanye hilo zoezi!!!
Namshauri Rais JPM awepeleke kina Paulo Makonda(Dar), Mrisho Gambo(Arusha) na Mnyeti(Arumeru) wakapate kitchen party kwa Mhe. Sadiki ili waache fujo za kijinga na utoto!
ADVERTISEMENT
By Daniel Mjema,Mwananchi;dmjema@mwananchi.co.tz
Moshi. Licha ya kuwa chini ya ngome ya upinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro imetajwa kuongoza kwa utulivu wa kisiasa.
Kwa miaka 20 mfululizo sasa, Moshi Mjini imekuwa ikiangukia chini ya upinzani. Mwaka 1995-2000 ilikuwa chini ya NCCR-Mageuzi na tangu mwaka 2000 mpaka sasa imekuwa chini ya Chadema.
Moshi haijawahi kushuhudiwa vurugu kubwa za kisiasa yakiwamo maandamano yasiyo na kibali kama miji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mwenyekiti wa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, wanatokea Mkoa wa Kilimanjaro, lakini ndiyo mkoa wenye utulivu wa kisiasa licha ya upinzani kushika maeneo mengi.
Uchunguzi wa Mwananchi Digital umebaini kuwa mambo yanayosababisha Jimbo liwe na utulivu wa kisiasa ni kiwango cha juu cha kujua kusoma na kuandika (literacy) kuliko jimbo lolote nchini.