Siri ya mafanikio katika maisha

Siri ya mafanikio katika maisha

steveson manumbu

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
887
Reaction score
178
Wanadamu wote tumeumbwa na kupewa akili ambayo inabidi tuitumie vizuri ili kuweza kuishi vyema katika ulimwengu huu. Kinachoshangaza ni kwamba wapo watu wachache tu ambao wamekuwa wakitumia akili vizuri na kufanya vitu vikubwa vinavyo wapatia mafanikio makubwa, huku wengi wetu tukiwa tumebaki kusema kuwa wao wamebahatika.

Hakuna watu waliozaliwa na bahati au mikosi, wanadamu wote wanauwezo wakutumia akili vizuri na kujipatia kipato kikubwa sana. Yapo mambo kadha wa kadha ambayo inabidi tuweze kuyafanya ili kuhakikisha kuwa tunasonga mbele na kuwa na maisha mazuri.

Kwanza kabisa, lazima mtu uwe na nidhamu katika kila kitu ambacho unakifanya. nidhamu inachukua sehemu kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria. Hakikisha unakuwa na ratiba inayoeleweka ambayo itakuwa inakuongoza katika shughuli zako za kila siku.

Hii itaongeza ufanisi, lakini pia nidhamu humfanya mtu aheshimike na kuoneka ana thamani katika jamii, kitu kinachoweza kufanya watu wakupatie kazi mbalimbali kwakuwa wanaamini hauta waaibisha.

Uwe mwaminifu katika maisha yako. uaminifu umekuwa adimu sana kwa watu wengi, jambo linalopelekea watu kukosa nafasi mbalimbali kwakuhofiwa kufanya ubadhilifu.

Ukiwa mwaminifu ni rahisi kupata fursa nyingi na kazi nzuri zenye maslahi mazuri. uaminifu ni silaha kubawa sana katika maisha.

Watu waliofanikiwa walikuwa waaminifu kwa sehemu kubwa, hawakuwa na tamaa ndogondogo zisizo nafaida. hakuna haja ya kuiba fedha kidogo ambazo zitachafua jina lako na kufanya heshima yako ipotee. Kumbuka kuwa ni rahisi sana kupoteza heshima kuliko kuijenga.

Usiwe na matumizi yasiyo na msingi. Watu wengi hawafanikiwi kwasababu wanatamani maisha ya wenzao, wanapenda waonekane wana maisha ya juu wakati sio kweli. Hakuna haja ya kutafuta sifa mbele za watu wakati ukirudi kwako unaanza kujuta kwa matumizi uliyoyafanya.

Weka akiba kwa kile unachokipata, achana na starehe zisizo za msingi. unywaji wa pombe unafilisi sana na unakwamisha sana maendeleo ya watu wengi. ishi maisha yaliyo ndani ya uwezo wako, ukiwaza kupiga hatua na si kudumaa hapohapo ulipo.

Fanya kazi kwa bidii na kwa malengo ili uwe na maisha mazuri. uvivu wa kufikiri na wa kufanya kazi unakwamisha maendeleo.

Tazama watu wote waliofanikiwa wanafanya sana kazi kwa bidii. Mwenyezi Mungu alisema kuwa asiyefanya kazi na asile, usichague kazi ya kufanya ilimradi isiwe inavunja sheria. Tuache ubishoo wakuona kuwa kuna kazi ambazo hazikustahili wakati huna kazi ya kufanya.

Kuwa mbunifu, lakini pia tumia kipaji chako kujipatia kipato. usijilinganishe maisha yako na yawatu wengine, usiangalie watu waliofanikiwa bali angalia watu walio chini yako. Mshukuru Mungu kwa uhai na uzima ulio nao. Fanya kazi kwa bidii ukimtanguliza Mungu utafanikiwa tu.
 
Kwenye mambo muhimu kama haya awachangii, lakini kwenye siasa , wanajaa kibao. ASANTE MLETA MADA.
 
Imekaa poa sana hiyo, ifanye editing kidogo...!!!
 
Eti tutumie akili vizuri. Je mfumo wa nchi unaruhusu matumizi ya akili au ujanja ujanja? Mnafanikiwa kwa ujanja ujanja alafu mnajifanya weledi wa maisha na kutuandikia tumakala mlitotutafsiri toka mbele ili muendelee kutuibia. Tumewashtukia
 
Mpumbavu hata ukimtwanga kwenye kinu pamoja na ngano upumbavu wake hautamtoka. Usibishane na mpumbavu usije kufanana naye. Mtoa mada katoa mawazo mazuri kufundisha mchangiaji anaanzisha matusi. Changia,ping a au boresha. Matusi faida yake nini ?
 
Kwenye mambo muhimu kama haya awachangii, lakini kwenye siasa , wanajaa kibao. ASANTE MLETA MADA.

Hujui siasa bora ndo mafanikio yako pia?!
Chukulia mikataba feki ya madini na gesi. Au uko darasa na ngapi?
 
kweli mkuu umeongea uwazi inabidi tubadilike tupo kwa ajiri ya kujifubza vitu muhimu . ni mbaya zaidi kila mtu kuwa mwanasiasa
 
Eti tutumie akili vizuri. Je mfumo wa nchi unaruhusu matumizi ya akili au ujanja ujanja? Mnafanikiwa kwa ujanja ujanja alafu mnajifanya weledi wa maisha na kutuandikia tumakala mlitotutafsiri toka mbele ili muendelee kutuibia. Tumewashtukia

mkuu badilika lengo ni kuwekana sana na kujifunza mambo tofauti tofauti usiongee kwa hasira sababu ya kukosa cha kufanya nasoma makala na vitabu mabalimbali ili kuweza kunitengeneza niwe tifauti hii ni karne ya 21 kila mtu anajua kusoma na kuandika lakini ni karne ya watu wachache wasiopenda kujifunza mambo mapya badilika maana ya jf hujaitambua. samahani lakini.
 
Mpumbavu hata ukimtwanga kwenye kinu pamoja na ngano upumbavu wake hautamtoka. Usibishane na mpumbavu usije kufanana naye. Mtoa mada katoa mawazo mazuri kufundisha mchangiaji anaanzisha matusi. Changia,ping a au boresha. Matusi faida yake nini ?

mkuu ninachojifunza ni kuwa dunia ya leo si ya mbumbumbu wasiojua kusoma na kuandika but ni dunia ya watu wasiopenda kujifunza mambo mapya na kubadili mfumo wa kufikiri.
binadamu wote tupo sawa na unaemcheka leo ni kwa sababu ya fikra zake hivyo ukimtengenezea mazingira ya kumbadili fikra atakuwa mtu mzuri hivyo basi hiyo ni kazi yangu mm na ww mkuu .
 
Hujui siasa bora ndo mafanikio yako pia?!
Chukulia mikataba feki ya madini na gesi. Au uko darasa na ngapi?

Dogo michango yako humu ni ya ki-facebook Facebook hivi, majukwaa mengine ya naona usilete pumba zako bwana. Tulia angalia wakubwa zako wanachangia nini ndio uchangie
 
Unamwita "dogo" nadhani amekuzidi uelewa dogo yuko sahihi siasa bora ni kiini cha maendeleo.
 
Ubarikiwe mleta maada inshaalah Mungu akuongezee maarifa.
 
Dogo michango yako humu ni ya ki-facebook Facebook hivi, majukwaa mengine ya naona usilete pumba zako bwana. Tulia angalia wakubwa zako wanachangia nini ndio uchangie

Aisee usirudie kuniita dogo wewe mtoto, Mi sipo apa kusubiri matokeo na usijipendekeze kwangu.

Join Date : 11th March 2014
 
mkuu badilika lengo ni kuwekana sana na kujifunza mambo tofauti tofauti usiongee kwa hasira sababu ya kukosa cha kufanya nasoma makala na vitabu mabalimbali ili kuweza kunitengeneza niwe tifauti hii ni karne ya 21 kila mtu anajua kusoma na kuandika lakini ni karne ya watu wachache wasiopenda kujifunza mambo mapya badilika maana ya jf hujaitambua. samahani lakini.

Bila samahani mkuu! hapa najenga hoja kuwa % kubwa ya watz waliotoka kimaisha kwa maana ya kufanikiwa ni kweli ni waaminifu, wanafanya kazi kwa bidii nk km ulivyotushirikisha katika mada yako lakini silaha yao kubwa ni UJANJA UJANJA ambapo ndani yake kuna wivu, fitina, unafiki, na bila kusahau the rushwa. huwa wana msemo wao kuwa nilipata deal/mchongo ambapo ukijaribu kumdadisi mdomo unakuwa mzito kuelezea hayo mafanikio.
 
ongera kwa threat nzuri kiongozi me binafsi nime note some issue, hizi ndiyo mada tunazosubiri vijana,
usisite kutupa mambo mazuri kama haya kwa siku nyingine, ubarikiwe

wito;watanzania tujitahidi kufikiri chanya unapotoa mada mada ni vizuri iwe na mtazamo mzuri na lengo zuri piah
 
Wanadamu wote tumeumbwa na kupewa akili ambayo inabidi tuitumie vizuri ili kuweza kuishi vyema katika ulimwengu huu. Kinachoshangaza ni kwamba wapo watu wachache tu ambao wamekuwa wakitumia akili vizuri na kufanya vitu vikubwa vinavyo wapatia mafanikio makubwa, huku wengi wetu tukiwa tumebaki kusema kuwa wao wamebahatika.

Hakuna watu waliozaliwa na bahati au mikosi, wanadamu wote wanauwezo wakutumia akili vizuri na kujipatia kipato kikubwa sana. Yapo mambo kadha wa kadha ambayo inabidi tuweze kuyafanya ili kuhakikisha kuwa tunasonga mbele na kuwa na maisha mazuri.

Kwanza kabisa, lazima mtu uwe na nidhamu katika kila kitu ambacho unakifanya. nidhamu inachukua sehemu kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria. Hakikisha unakuwa na ratiba inayoeleweka ambayo itakuwa inakuongoza katika shughuli zako za kila siku.

Hii itaongeza ufanisi, lakini pia nidhamu humfanya mtu aheshimike na kuoneka ana thamani katika jamii, kitu kinachoweza kufanya watu wakupatie kazi mbalimbali kwakuwa wanaamini hauta waaibisha.

Uwe mwaminifu katika maisha yako. uaminifu umekuwa adimu sana kwa watu wengi, jambo linalopelekea watu kukosa nafasi mbalimbali kwakuhofiwa kufanya ubadhilifu.

Ukiwa mwaminifu ni rahisi kupata fursa nyingi na kazi nzuri zenye maslahi mazuri. uaminifu ni silaha kubawa sana katika maisha.

Watu waliofanikiwa walikuwa waaminifu kwa sehemu kubwa, hawakuwa na tamaa ndogondogo zisizo nafaida. hakuna haja ya kuiba fedha kidogo ambazo zitachafua jina lako na kufanya heshima yako ipotee. Kumbuka kuwa ni rahisi sana kupoteza heshima kuliko kuijenga.

Usiwe na matumizi yasiyo na msingi. Watu wengi hawafanikiwi kwasababu wanatamani maisha ya wenzao, wanapenda waonekane wana maisha ya juu wakati sio kweli. Hakuna haja ya kutafuta sifa mbele za watu wakati ukirudi kwako unaanza kujuta kwa matumizi uliyoyafanya.

Weka akiba kwa kile unachokipata, achana na starehe zisizo za msingi. unywaji wa pombe unafilisi sana na unakwamisha sana maendeleo ya watu wengi. ishi maisha yaliyo ndani ya uwezo wako, ukiwaza kupiga hatua na si kudumaa hapohapo ulipo.

Fanya kazi kwa bidii na kwa malengo ili uwe na maisha mazuri. uvivu wa kufikiri na wa kufanya kazi unakwamisha maendeleo.

Tazama watu wote waliofanikiwa wanafanya sana kazi kwa bidii. Mwenyezi Mungu alisema kuwa asiyefanya kazi na asile, usichague kazi ya kufanya ilimradi isiwe inavunja sheria. Tuache ubishoo wakuona kuwa kuna kazi ambazo hazikustahili wakati huna kazi ya kufanya.

Kuwa mbunifu, lakini pia tumia kipaji chako kujipatia kipato. usijilinganishe maisha yako na yawatu wengine, usiangalie watu waliofanikiwa bali angalia watu walio chini yako. Mshukuru Mungu kwa uhai na uzima ulio nao. Fanya kazi kwa bidii ukimtanguliza Mungu utafanikiwa tu.

Shukrani kwa kutukumbusha mambo ya muhimu.:thumbup:
 
Back
Top Bottom