Siri ya kuvumbuliwa simu

Jan 15, 2013
77
27
Binafsi nimekuwa nikijiuliza; waliovumbua simu na vyombo ya kisasa vya mawasiliano walikuwa na malengo gani?

Mashaka haya katika fikra zangu yalizidi kuota mizizi baada ya kuangila movie/series kadhaa, miongoni mwazo; The 100 season ya 3 kuhusu CHIP, Jason Bourney ya mwaka 2016 kuhusu FREE INTERNET, Kingsman - The secret service kuhusu FREE SIM CARD, FREE INTERNET, FOR EVERYONE FOREVER, the matrix kwa waliozielewa.

Kupitia movie na series kadhaa zilizohusu technolojia na mambo ya ujasusi;

Sidhani waliotengeneza simu walikuwa na lengo la kufanya biashara kama tufikiriavyo,
Sidhani walikuwa na lengo la kufanya wepesi katika mawasiliano kama tufikiriavyo,
Sidhani tufikiriavyo ni sahihi, nifikiriavyo; kuna siri?

Kuna ungojwa unaitwa nomophobia, nimesoma makala fulani humuhumu JF, iliokuwa na kichwa kama hichi (UNAWEZA KUKAA MUDA GANI BILA KUISHIKA SIMU), kwa mujibu wa makala hiyo, muathirika wa ugojwa huo hukosa raha pindi akosapo kuwa na uwezo wa kutumia simu yake, eidha kwa kukatazwa kutumia simu, simu kuisha chaji, kuipoteza na nyinginezo.

Mie nadhani SIRI YA KUVUMBULIWA SIMU ni kukuza vita ya kifikra (THE WAR ON MIND CONTROL), je wewe unafikiriaje?
 
hata chips wanasema zinamadhara lkn watu wanakula tu,sufuria zinamadhara lkn bado tunapikia sasa alietengeneza sufuria alikuwa na malengo gani..?
lengo linaweza kuwa zuri lkn kukawa na zara ndani yake ila lengo kuu litabaki palepale... endapo ni vizuri kuhoji pia
 
Umeathiliwa sana na series.....
Hakuwa na lengo baya siyo kila unacho kiona kwenye series kina reflect ukweli japo kunaweza kuwa na ukweli ndani yake...
 
Back
Top Bottom