siri ya kumvutia mumeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

siri ya kumvutia mumeo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Sep 20, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  ukipenda chukua ukinuna achana nazo
  [​IMG]SIRI YA KUMVUTIA MUME MUDA WOTE:
  Ni kweli upo kwenye mahusiano na katika mahusiano yako mwanaume uliyenaye ni wa uhakika, safi kabisa na hongera sana.
  hata hivyo linakuja wazo kwamba hivi inawezekana huyu mwanaume akaendelea kunipenda kama hivi?
  Je, atakuwa yupo interested na mimi muda wote?


  Haijalishi mnapendana kiasi gani ukweli ni kwamba mahusiano huhitaji kazi, huhitaji efforts, inahitaji kuwekeza jitihada kidogo ili kuvuna mambo makubwa.
  Kama unapenda mume uliyenaye awe anavutiwa na wewe wakati wote kuna tips na siri nyingi unahitaji kuzifahamu vingenevyo unaweza kujikutana anakukwepa na kukuona huna lolote (huna jipya, unachosha)

  Jambo la kwanza ni kweli mahusiano ni kitu cha ajabu sana huweza kupanda na kushuka kwa kiwango cha kutisha hata hivyo siri kubwa ya mahusiano unatakiwa usiwe mtu ambaye mpenzi wako anaweza kujua au kutabiri au kutarajia mara zote utasema nini au utafanya kitu gani, unahitaji kuwa na vitu vizuri ambavyo hawezi kutegemea, waingereza wanaita unakuwa spontaneous and fun na unakuwa na adventure ambazo hategemei.

  Hakuna kitu mwanaume hapendi kama mwanamke aliye na usumbufu wa uhitaji (too needy). Kumtaka mume kila kitu hadi anajiona usumbufu huweza kuua mwanamke kumvutia mwanaume, ninachozungumzia hapa si ile hali ya kuonesha unamuhitaji bali ile hali inayoonesha unasumbua kwani hata kile ambacho kipo kwenye uwezo wako bado unataka mume akutimizie.
  Kama anataka kutoka na rafike zake wa kiume mruhusu siyo kulalamika tu hadi anajiona mkosaji.
  Kwani ukimruhusu naye akaenda kufurahi na rafiki zake na wewe ukatumia muda huo na rafiki zako kuna tatizo gani, wewe unataka kumganda all the time hadi anashindwa kupumua, kwa mwanaume hiyo ni dalili kwamba wewe mwanamke hupo huru bali upo desparate na maisha.

  Pia si vizuri kumpigia simu au kumtumia sms kila dakika kutaka kujua yupo wapi anafanya nini na yupo na nani as if wewe ni auditor wa mienendo yake.
  Ukiona message au simu haipokelewi ujua unamsumbua badala ya kuonesha upo caring.
  Pia angalia usiwe ni mwanamke ambaye anatuma sms kwa mume au kumpigia simu mara moja kwa mwaka, this is too much!

  Jambo lingine na la msingi sana mwanamke lazima ukumbuke kwamba wanaume wanasoma magazeti huwa hawasomi mawazo ya kwenye akili yako (mind) hivyo basi ni muhimu sana kumwambia mume wako kila unajisikia pale mkijadili suala lolote na siyo kukubaliana tu na kila kitu ukiamini kwamba unamfurahisha na unataka avutiwe na wewe.
  Mwanaume mwenye akili timamu anafahamu fika kwamba mwanamke mwema na mwenye busara kichwani mwake ana ubongo hivyo huwezi kukubaliana na kila kitu na kusema ndiyo, ndiyo ndiyo ….
  Mwanaume anahitaji mwanamke ambaye naye anaweza kupendekeza wazo jipya na kwa njia hiyo huonekana ni mwanamke strong na wanaume hupenda strong woman ambaye anaonesha uwezo hivyo kuvutia zaidi.

  Hakikisha mume wako anasoma kitu kipya kuhusu wewe baada ya muda fulani na hiyo itasaidia kukuangalia kwa upya zaidi na maana yake unamvutia. Kama ulishaonesha kila kitu basi unahitaji kuwa mbunifu kwani mwanaume huhitaji kitu kipya kutoka kwa mwanamke baada ya muda fulani katika maisha.

  Pia ni muhimu sana kuachana na imani potofu kama vile
  "The key to a man's heart is through his stomach"
  Ni kweli wanaume huwasifia sana wanawake wanaokaangiza vizuri hata hivyo si misosi mizuri tu ndiyo ticket ya mume kuvutiwa na wewe.
  Pia wapo wanaoamini kwamba ili mume avutiwe na mke ni pale mke anapotoa sex kwa kwenda mbele, ni kweli mwanaume akipewa hiyo offer hawezi kulazia damu hata hivyo mwanaume anaweza kufanya sex na asiwe amevutiwa na wewe kwani kwa mwanaume sex na love ni vitu viwili tofauti.

  Je, kama si chakula kitamu au sex kila siku ni kitu gani muhimu ili kumvutia mwanaume?
  Jibu ni rahisi mno mwanaume anahitaji heshima, kumjali, kutukuzwa, kuenziwa, kusifiwa, thaminiwa na kunyenyekewa, kuhusudiwa (respect, admire).
  Hakuna hitaji kubwa kwa mwanaume kama lile la kwamba anahitajiwa (needed) na mke wake.

  Weekend njema!

  God Bless you!
  Dieu vous bénisse!

  Mungu akubariki!
   
 2. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je, kama si chakula kitamu au sex kila siku ni kitu gani muhimu ili kumvutia mwanaume?
  Jibu ni rahisi mno mwanaume anahitaji heshima, kumjali, kutukuzwa, kuenziwa, kusifiwa, thaminiwa na kunyenyekewa, kuhusudiwa (respect, admire). Hakuna hitaji kubwa kwa mwanaume kama lile la kwamba anahitajiwa (needed) na mke wake.


  hapo kwenye red hapo
   
 3. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  thanx pdidy
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Sep 21, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hivi hamnaga nakala za jinsi ya kumfurahisha au mvutia mwanamke?. Aksante Pdidy kwa makala nzuri. Ubarikiwe
   
 5. c

  charndams JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kama vile ulikuwa akilini mwangu. mimi pia jidume lakini nahisi wanaume wanajifanya miungu midogo. let us focus our attention to our ladies. ndio nakala yenyewe nzuri lakini wanaume wengine bwana ni kama paka mapepe, umpe japo steki huyoo paka atakushukuru lakini akimuona panya anakutoroka
   
 6. N

  Nsagali Member

  #6
  Sep 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa sms
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  kwa niaba ya jf wewe na blackberry nawatunukia degree ye heshima ya kuthaminiwa na waume zenu
   
 8. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Senkyu
   
Loading...