Hili vazi linashangaza kweli!
Dukani linauzwa hadharani.
Wakati wa kununuliwa linanunuliwa kwa siri.
Wakati wa kuvaliwa linavaliwa kwa siri na linavaliwa sirini.
Linaficha siri.
Linafuliwa na kuanikwa kwa siri.
Linapochakaa linatupwa kwa siri.
Kwa nini limekuwa la siri kiasi hiki?