Priest_
Member
- Jun 17, 2021
- 11
- 25
“Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini walioumbwa na Mwenyezi-Mungu. Basi, nyoka akamwambia huyo mwanamke, “Ati Mungu alisema msile matunda ya mti wowote bustanini?” 2Mwanamke akamjibu huyo nyoka, “Twaweza kula matunda ya mti wowote bustanini; 3lakini Mungu alisema, ‘Msile matunda ya mti ulio katikati ya bustani, wala msiuguse, msije mkafa” Huu ni mstari ambayo watu wengi tumekuwa tunaufahamu na bila shaka kujiuliza kwamba ilikuwaje Nyoka kuwa na uwezo wa kuzungumza? Je, Adam alikula tunda au tunda lilikuwa na maana nyingine iliyo fichika ?
Nitajaribu kuchambua huu mstari na kujaribu kuangalia maana halisi au siri iliyo fichika. Hii itakuwa imegawanyia kwenye sehemu kuu tatu
SEHEMU YA KWANZA
Serpent (Swahili: Nyoka/Joka) anajulikana kwenye Biblia, Quran, na Hinduism. Alama ya nyoka inamaana kubwa sana kwenye haya madhehebu na tamaduni ya watu wakale. Pia neno “Nyoka” limekuwa au nilimetumika kuwa na maana moja kwenye haya madhehebu.
Neno nyoka kwenye biblia, limetumika kuwakilisha Shetani/Ibilisi. Kulingana na Ufunuo wa Yohana 12:7-8 inaeleza kwamba kulikuwa na vita mbinguni, Mikaeli na malaika wake waki pigana na hilo joka. Yohana 12:9 Inaeleza kwamba nyoka alikuwa naitwa Ibilisi/Shetani, adanganyaye watu wote ulimwenguni. Alitupwa chini ardhini, yeye pamoja na malaika wake”.
Pia Isaya 27:1 inaeleza kwamba Mungu atautwaa upanga na kuliadhibu joka danganyifu liishilo baharini.
Pia historia kama hii imetajwa kwenye Quran takatifu. Kulingana na Quran Surah Al-A'raf 7:19 inaeleza Adam na mke wake walikuwa wanaishi kwenye bustani ambayo inapendeza kama paradiso. Kwenye hii bustani waliambiwa wanaweza kula matunda yeyote isipokuwa mti mmoja. Surah Al-A'raf 7:20–22 inaeleza Shetani/Ibilisi aliwashawishi Adam na mke wake kuonja ule mti.
Pia kwenye hadithi ya Fakhr al-Mulk Radwan. Imemtaja Ridwan(Riswan) kama mlinzi wa mbinguni kwenye Qisas Al-Anbiya, ambayo kazi yake ilikuwa kumzuia Ibilisi/Shetani kuingia kwenye bustani ya Adam. Lakini Riswan alidanganywa na “nyoka” amabye alikuwa amemficha Ibilisi kwenye mdomo.
Kwenye vitabu vya Hindu, kuna hadithi sambamba na Adam. Hindu wanaamini kwamba kulikuwa na mtu anaitwa Adama alikuwa anishi na mke wake kwenye msitu mkubwa ambao waliwekwa na Mungu. Kama ilivyo hapo juu, walikatazwa kula matunda ya mti. Lakini, Kali Purusha alijibadilisha kuwa Nyoka na kuwarubuni Adama na mkewe kula matunda ya mti walio katazwa.
Kwenye dini ya Hindu Kali Purusha ni mtoto wa jinni, Krodha(Hasira) na Himsha (wivu).
Maana halisi ya Nyoka
Kama ambavyo tumeona hapo juu ni kwamba Serpent(Nyoka) inamaana ya Shetani/Ibilisi. Lakini nyakati za kale, kabla ya biblia, Quran au Hindi. Neno Serpent(Nyoka) lilikuwa na maana ya Hekima na Uzazi. Mathayo 10:16 Yesu alisema “kuweni na Hekima kama nyoka”.
Kuhusu Uzazi, anamaana ya kufanya upya na kuzaliwa mara ya pili. Hii imethibitishwa Yohana 3:3 Yesu alisema lazima kuzaliwa mara ya pili. Watu wa kale walikuwa wanatumia picha ya nyoka kung'ata mkia wake. Hii Ilikuwa inaonyesha uwezo wa nyoka kujifanya upya, ambao ni uwezo halisi wa nyoka kuondoa ngozi za zamani na kutengeneza ngozi mpya.
Hitimisho sehemu ya kwanza:
Kama ilivyo nyoka kutambaa na kuishi kwenye mapango/mashimo aridhini, inamaana nyoka anawakilisha Kuzimu(underworld) Unaweza kuangalia Isaya 14:9-14
Kwahiyo tumeona kwamba Nyoka alitumika kuwakilisha Hekima au kuzaliwa kwa Hekima/Ufahamu. Pia hii Hekima haina kikomo, ndio maana inawakilishwa na alama ya nyoka kula/kung'ata mkia wake.
Itaendelea......

- Maana ya neno Nyoka na maana halisi ya nyoka
- Neno tunda na maana halisi ya neno tunda
- Mwisho, tutaweka maana halisi kwenye mstari mzima ili kuweza kuangalia kama kutakuwa na siri au ujumbe ulio fichika kwenye Mwanzo 3:1-3.