Siri nzito TANESCO zafichuka!

Siri nzito TANESCO zafichuka!

Mkuu Njaare,

nashukuru kama nawe umeona udhaifu wa hii article na inadhoofisha gazeti zima la Tanzania Daima.

Wiki hii yote Stori ya Tanesco hiyo hiyo ndiyo lead story kwenye Tanzania Daima, mnafanya kugeuza paragraph tu za juu zinakuwa chini,hakuna jipya huko? content za ajabu ajabu tu, cant you go further than that? Yaani nyie na article yenu ndiyo mnathibitisha kuwa mnatumiwa tu kama taulo tu,na mnawaaibisha waandishi wengine, kwa kuandika mambo msiyoyajua. Mathalan, mnapoandika "maombi ya Tanesco kupandisha ushuru," ushuru gani Tanesco wanapandisha?

Hebu fanyeni hata analysis ya madeni ya Tanesco yamekuwaje hadi kufikia hapo, wadaiwa ni akina nani, umeme unazalishwa kiasi gani, unanunuliwa kwa gharama gani na Tanesco wanatuuzia kwa kiasi gani? Chambueni hata operational costs za Tanesco,mfano, wanatumia sh ngapi kukanusha kwenye matangazo ghali kuwa hakuna mgao ilhali upo? Au kwa sababu mnafaidika na hayomatangazo basi mnafumba macho?
 
Imba:

Nchi ya kitu kidogo; nchi ya watu wadogo
Inasonga mbele hatua mbili na kurudi nyuma hatua saba.
Wananchi wameacha nchi mikononi mwa wasanii
Wananchi wanawaita wasanii wanasiasa
Viongozi waso maono zaidi ya matumbo
Nchi hiyo ni hii hiiii hiii hapa
Wa hapa hapa wapo kama hawapo
Wapo kama wanapita njia ili hali ndo kwao
Nchi hiyo ni hii ya kwangu yenye mito na mabonde
Imesheeni madini lukuki na wananchi waganga njaa
Viongozi tumbo nao waganga njaaa
Nani ainusuri nchi hiyooooooo


Tafakari
 
Mkapa, Mwinyi, Kikwete na wote waliowahi kuwa Mawaziri katika Wizara hiyo tangu wakati wa RUKHSA wamechangia sana katika kuiangamiza TANESCO.
 
Mi nasikia kutapika haki

Mramba wa Tanesco hana undugu na aliyekuwa waziri. Tena huyu ni mzee wa Kanisa la TAG pale ubungo. Ni mtumishi mzuri wa Mungu, na wakati mwingine huwa anahubiri.
 
Tanesco., Shirika pekee linalogawa umeme, limeweka luku, watanzania wanalipa, linapataje hasara? kama kuna watu wana daiwa kwanini lisiwakatie? Hasara ya bilioni 90 jamani hebu wana JF kila mmoja arudi aangalie bajeti ya Serikali kuna Wizara ngapi zinapewa Fesha kidogo sana kuliko Ruzuku ya Bilioni 231 zinzotumiwa na Tanesco kutengeneza Dairy na Kalenda, kutolea matangazo ya kukanusha mgawo hata kama tunaona nchi ipo gizani, Hongera gazeti la Tanzania Daima, kwa kueleza kwa ufasaha mambo ambayo magazeti mengine yanaogopa. Watanzania wanatoka nyumbani hawajanyoosha nguo, nyimbani giza, lakini magazeti yanaletewa tangazo kuwa hakuna mgawo yanaleta kwa wananchi
Mambo gani ya ufasaha limeeleza zaidi ya kutumiwa na watu furani kwa manufaa yao ku-discredit kazi ya Waziri wa Nishati na Madini na Katibu Mkuu wa Wizara.

Kinachoandikwa hapa kinafaa kwa watu wasiojua kile kinachoendelea TANESCO.

Kama kweli Tanzania Daima ni waandishi mahili, wakokotoe basi mapato na matumizi ya TANESCO. Manunuzi ya umeme na gharama zake, mauzo kwa wateja n.k

Kila mara, Wanakuja na heading kubwa, zero contents.
 
Tanesco VUMILIENI gesi ikija matatizo yataisha. Sie tunasikilizia umeme ushuke, nyie mnataka kupandisha? Hebu vutavuta subira kidogo.
 
Mgao huu unathibitisha Tanesco na washauri wetu wote wa nishati ni wajinga na mambumbu
Hawafanyi kazi zao kitaalamu bali waoo tu kazi yao kubwa ni washa na zima .
Tulioo anza kuzalisha gas tulijigamba sana kuwa suala la mgao litapubgua kwa sababu vyanzo vya kuzalisha umeme vimeongezeka
Leo tunaambiwa wenye gesi yao wanata kusafisha mitambo yao ! Hatuna cha kufanya hatuna gesi ya kuzalishia umeme kwa nini?
Wenyewe mlisema mlikua na taarifa miezi 2 kabla. Hivi gas si inasafirishwa kama petroli? Si inauzwa kila kona ya dunia? Gesi hii si inawekwa katika storage tanks kwa akiba na matumizi ya dharura?
Ina maana gesi yetu ni hand to mouth?
Kwa nini walipo ambiwa kutakuwa na service wasiweke akiba ya gesi kuzalisha umeme bila ya mgao?
Jee hizi mbio za mabomba ya mchina ya mtwara nayo stori si itakua hiyo hiyo?
Jee siku songo songo ikipata mafuriko au natural disaster si ndio tumekwisha?
Jamani gesi nayo inajengewa storage tanks na depots kama disel na petrol
Tanesco wao wanaleta gesi kutoka songas moja kwa moja hadi kwenye genereta!!! Kwa nini msiwe na akiba ?
Huu tanesco ni ujinga na hamlifanyii wema taifa bali mnaliangamiza
Garama ya kujenga deport ya kuweka gesi kwa matumizi ya mwezi mmoja haizidi 10bilion
Hata mkimpa mtu ajenge na nyie mkodi hio sehemu wapo watu watajenga

Jengine la ujinga na kuikomoa nchi si mliambiwa miezi 2 kabla kuhusu matengenezo? Kwanini msikae na hao symbion kuona kipindi hichi mnaagiza gesi kutoka nje?
Mambo yenu ya kuudhi kama vile mmepata hivo vyeti kwa kukopia tu
Hamuoneshi kama ni wataalam walobobea waliosoma sawa sawa na kujua mnachokifanya
Mnatuvuruga
Afadhali hili shirika liuzwe tu na hawa jamaa wapewe jembe wakalime
 
tangu kufanyika mabadiliko ya uongozi katika wizara angalau umeme umekuwa wa uhakika kidogo serikali haina budi kuboresha huduma ya upatikanaji wa umeme wa kutosha hasa katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi.
 
Hili shamba la mh.lowasa namh rostam wavuna tu. Kweli dhambi kubwa sana binadam hawa wanchuma cjui wataishi miaka mingapi
 
Back
Top Bottom