Siri nzito TANESCO zafichuka!

Siri nzito TANESCO zafichuka!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,574
Reaction score
164,454
WAKATI Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) likitangaza kutoingiliwa kiutendaji na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, siri zaidi za kuzama kwake zimefichuka.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na Tanzania Daima Jumamosi, umebaini TANESCO imekuwa ikiangushwa kutokana na uamuzi mbaya wa kisiasa unaodaiwa kutolewa na viongozi wa juu wa wizara hiyo.

Jumatano wiki hii gazeti hili liliandika kuwa hali ya TANESCO ni mbaya na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakimu Maswi, wanatajwa kuwa chanzo cha kudhohofika kiuchumi shirika hilo kwa madai ya kuingilia shughuli za kiutendaji kwa maslahi ya kisiasa.

Hata hivyo, siku moja baada ya habari hiyo, TANESCO inayoendeshwa kwa hasara ya sh bilioni 90 kwa mwezi, ilitangaza katika vyombo vya habari kuwa habari hiyo haina ukweli wowote wala mashiko, na kueleza umma kuwa hakuna msuguano wala kukinzana kati ya menejimenti ya TANESCO na wizara.

Lakini nyaraka za mawasiliano baina ya shirika hilo na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) zimebainisha namna TANESCO ilivyolalamika kuingiliwa kiutendaji na wakubwa hao wa wizara.

Katika nyaraka hizo, TANESCO walisema bayana kutopenda kabisa uamuzi wa wizara ambao unafanywa kisiasa, bila kuzingatia utaalamu wakati wa sakata la kutaka kupandisha bei ya umeme.

Ushauri wa kitaalamu ambao ulizingatia sababu za TANESCO kutopendezwa na uamuzi wa kisiasa ulifikishwa kwa maandishi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu Jan, 16, mwaka huu.

TANESCO katika mawasiliano yake na Ewura iliweka wazi namna "isivyopendezwa hata kidogo na uamuzi wa serikali, na inaona hakuna uwezekano wa kusikilizwa kila inapopeleka suala hili na kuelezea madhara yatakayopatikana baada ya kuondoa maombi ya dharura ya kupandisha ushuru".

TANESCO katika maelezo yake, ilitoa sababu nne; kwanza ikisema kiwango cha ruzuku kinachopangwa na Ewura kilionesha kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya kupanda na kushuka kwa thamani ya fedha, kwa mantiki hiyo hata kama ushuru huo ungetumika usingeisaidia TANESCO.

"Hali ya hewa pia siyo nzuri, kuna upungufu wa mvua unaosababisha upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, hivyo zitahitajika pesa nyingi sana ili kuwezesha ununuzi mafuta au umeme katika mwaka 2013.

"Mtiririko wa fedha kutoka serikalini haupo sanjari na mahitaji ya uendeshaji wa TANESCO, na mara nyingi serikali huchelewa kutoa pesa," ilisema sehemu ya mawasiliano baina ya pande hizo mbili.

Shirika hilo liliongeza kuwa, mkopo kutoka Benki ya Dunia utatumika kulipa madeni tu wala sio kuisadia TANESCO, hivyo kwa mtazamo huo, utaratibu wa serikali wa kutoa ruzuku inayotosheleza mwaka mzima, unaweza kufanyika bila kupandisha bei ya umeme, lakini ubuniwe utaratibu mwingine utakaofanya TANESCO iendelee kuonekana kwa macho ya watu kama vile bei imepandishwa, lakini bila kuondoa maombi ya kutopandisha ambako kutazidisha shaka kwa wadau wengine mfano wawekezaji na wabia wa maendeleo.

Wiki hii gazeti hili lilimnukuu Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Felchesmi Mramba, akisema kuwa hakuna mgawo wa umeme kwa sasa, na kwamba ikitokea serikali itatangaza.

Hata hivyo, kukatika kwa umeme kwa siku nzima katika baadhi ya sehemu kunadhihirisha uwepo wa mgawo wa siri unaoendelea.

Pamoja na kukanusha kuwepo kwa mgawo, Mramba alikiri kuwa hali ya umeme haijarejea katika uhalisia wake wa kawaida kiasi cha kuondoka katika hali ya dharura.

"Bado mitambo ya dharura tuliyokodi kupambana na hali ya umeme inaendelea kuhitajika, lakini pia mabwawa hayana maji ya kutosha kukidhi mahitaji ya umeme bila kuhitaji mitambo ya matufa," alisema.

Mramba alibainisha kuwa tangu Julai mwaka 2012 hadi Februari 2013, serikali imetumia jumla ya sh bilioni 231.2 kama ruzuku kwa TANESCO kwa ajili ya kununua mafuta ya mitambo.

"TANESCO kutoka kwenye mapato yake imetumia jumla ya sh bilioni 423.3 katika kipindi hicho kununulia mafuta, hivyo fedha yote iliyotumika kununulia mafuta ndani ya kipindi hicho ni sh bilioni 654.5," alisema Mramba.

Kauli ya Mramba inaonesha kuwa hata kama TANESCO ingeamua isilipe mishahara wala isifanye matengenezo ya mitambo, isinunue vifaa vya kuunganishia wateja, au isiingie gharama nyingine zozote, bado ingepata hasara ya karibu sh bilioni 90 kila mwezi.

Chanzo chetu kutoka Ewura kimesema kuwa walishangazwa na uamuzi wa TANESCO wa kujitoa katika mazungumzo ya kupanda kwa bei ya umeme kwa kiasi kidogo na kwenye upungufu ruzuku ya serikali iweze kufidia, kwa madai ya kutekeleza maelekezo kutoka wizarani.

Chanzo hicho, kimekiri wazi kuwa kuna mgawo wa umeme ingawa haujatangazwa rasmi.

"Mgawo upo ingawa haupo katika ratiba, ila tukiwauliza TANESCO ambao ndio wasemaji wanadai ni tatizo la miundombinu, au maji hayatoshi na kweli kwa sasa maji hayatoshi Mtera na kama hali ikiendelea hivi hivi Mtera itafungwa.

"Kwa sababu mvua za Januari hadi Machi zinazotegemewa hazikunyesha vizuri, na bado maji machache tunayopata toka Mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo tunagawana na wakulima wa mpunga walio katika bonde la Usangi, hapo ndiyo tunajiuliza tutoe maji kwa ajili ya mpunga au kwa ajili ya umeme?" kilisema chanzo chetu.


CHANZO:TANZANIA DAIMA
 
Tanesco ni chakula cha wakubwa hivyo shirika hilo halitaendeshwa kwa ufanisi hata siku moja. Kama kweli wange kuwa na huruma wangekaribisha wawekezaji ili kuwe na ushindani.
 
Nikiona jina Mramba sehemu yoyote huwa nahisi harufu kali ya ufisadi............
 
Shirika limejaa ufisadi kama nini,
Wanatangaza survey ndan ya siku 14 ukifika pale leo unaambiwa survey mwezi wa 7.
Shame on you Tanesco, Bora shirika libinafsishwe tu tumechozwa na udhalimu wenu ama kama ni kufa life kabisa tujue moja.
Mnakera sana.
 
Kauli mbiu ya Tanesco- Tanesco-Inaunguza Maisha yako! Usiguse nyaya zilizodondoka ( wakati hazina umeme)!
 
Hilo ni shamba la watu fulani ambao kazi yao ni kushinda kwenye mitandao kuzusha upuuzi lkn ipo siku siri itavuja kwamba kuna taasisi ambayo kila mwezi inavuna fedha tanesco
 
[QUOTE=Tatizo la Tanesco utendaji wake unaendeshwa kisiasa sana bila kuangalia hali hali ya uchumi wa nchi na matatizo yanayokumba shirika hilo.Tanesco sasa ni chombo cha kuchafuana na kupanda chart.Moja Tanesco imekuwa na mipango mibovu jinsi ya upatikanaji wa nishati mbadala pindi inapotokea mabadiliko ya tabia nchi.Kutegemea chanzo cha maji kufua umeme kumeleta majanga kwa sasa.Baada ya kutokea ukame na mabwawa kukauka nchi iliamua kukodisha mitambo ya zarura ya kufua umeme ambayo kwa kiasi kikubwa inatumia mafuta na gesi kujiendesha(emergency Power Purchasing Aggreement).Pamoja na mchakato huu kusaidia nchi isiingie gizani pia harufu za kukiuka taratibu za manunuzi zilikiukwa na kuleta mtafaruku kisiasa.Kwa kuwa mafuta ya mitambo yanaagizwa kutoka nje ya nchi na kushuka kwa thamani ya shilingi na kuyumba uchumi ulimwenguni gharama kubwa ya uzalishaji umeme ni kubwa.Ukubwa huo unamrudia mtumiaji kwa sababu Tanesco lazima iongeze bei ya umeme au serikali iongoze ruzuku bila hivyo Tanesco lazma ife.PILI , Tanesco sasa angalau mfumo wa madeni makubwa ya Bills umepungua baada ya kufunga Mita za Luku kwa watu binafsi,Ofsi za Serikali,Mawizara,Viwandani nk.Tatizo lilopo ni mfumo wa kukusanya pesa kutoka Shirika la umeme Znzbar.Hili deni ni kubwa na hawawezi kukatiwa.TATU Tanesco ina matatizo ya ndani Vishoka,Rushwa,matumizi mabaya ya rasilimali za kampuni zikiwamo pesa na watu,taratibu za kuunganisha umeme, miundo mbinu imechakaa (dilapidated infrastructure), washukuru REA/EWURA zinawapiga bega pamoja na upotevu wa umeme kutokana na uchakavu wa miundo mbinu.Kidogo majuisho hayo yanasababisha uendeshaji wa Tanesco ni gharama kubwa hivyo serikali lazima itoe ruzuku kubwa Our top most leaders shouldtell the people the truth,instead of giving them false hopes.Siasa isiongoze Tanesco.Wape wataalam waliokabidhiwa shirika hilo wafanye kazi bila shinikizo.Mramba,Mgonja kaza buti.Kwa matatizo yaliyopo Tanesco hata akija mwekezaji hakuna ufanisi.MPAHO
:crying:
 
Wakuu wa TANESCO wanalalamika kitu gani wakati miezi michache iliyopita waliungana na uongozi wa Wizara kuufitini uongozi wa Mhando na kuwaaminisha Watanganyika kwamba hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme itakua shwari baada ya kuondoka wahujumu akina Mhando!!!
 
Hizo ni siasa tu, bila msaada wa serikali Tanesco haiwezi simama yenyewe
 
Naona gazei hili linataka kuanza kutumiwa na wafanyabiashara mafisadi ili kuishinikiza serikali ipandishe bili za umeme na wao waanze kufanya biashara na Tanesco. Nasema hivyo kwa sababu;
1. Tanesco inataka ijiendeshe kibiashara wakati haina plan ya kutafuta mtaji. Tanesco inategemea mtaji wao uwe wananchi kwa kuwakamua. Iiombe serikali iwadhamini wakope.
2. Tanesco haina mpango wa kupanua vyanzo vya umeme wa bei nafuu. Inangangania kupanua matumizi ya mafuta ambayo ni ghali
3. Tanesco haionyeshi dalili ya kuachana na mikataba ya kifisadi. Toka mwaka 2005 mpaka leo tanesco inazalisha umeme wa dharura. Ni dharura gani ya miaka 8?
4. Tanesco haina mipango mikakati ndiyo maana inafuata mipango mikakati ya wanasiasa.

Kwa mantiki hiyo, hata kama EWURA itapandisha bill za umeme kitakachofanyika ni kuingia tena mkataba mwingine wa dharura na makampuni ya kifisadi mojawapo likiwa hilo linalomfadhili mwandishi wa habari hii.
 
Mramba!!! Jamani samaki mmoja akioza sii kweli kuwa wote wameoza!

Yawezekana hana harufu ya ufisadi!
 
inasikitisha mali za umma zinavyohujumiwa. hivi kweli imeshindikana kupata suluhisho la matatizo ya tanesco?
 
TANNESCO ni kicha na sehemu ya kuvuna hela kwa ccm huwezi sema unafanya biashara isyo na faida huku unang'ang'ania si wabinafisishe kama limeshawashinda
 
Hivi kumbe bado kuna hii kitu inaitwa TANESCO na bado kinatoa huduma za umeme!!.. alafu huyu Mramba si mtakula majani?
 
WAKATI Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) likitangaza kutoingiliwa kiutendaji na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, siri zaidi za kuzama kwake zimefichuka. Uchunguzi wa kina uliofanywa na Tanzania Daima Jumamosi, umebaini TANESCO imekuwa ikiangushwa kutokana na uamuzi mbaya wa kisiasa unaodaiwa kutolewa na viongozi wa juu wa wizara hiyo. Jumatano wiki hii gazeti hili liliandika kuwa hali ya TANESCO ni mbaya na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakimu Maswi, wanatajwa kuwa chanzo cha kudhohofika kiuchumi shirika hilo kwa madai ya kuingilia shughuli za kiutendaji kwa maslahi ya kisiasa. Hata hivyo, siku moja baada ya habari hiyo, TANESCO inayoendeshwa kwa hasara ya sh bilioni 90 kwa mwezi, ilitangaza katika vyombo vya habari kuwa habari hiyo haina ukweli wowote wala mashiko, na kueleza umma kuwa hakuna msuguano wala kukinzana kati ya menejimenti ya TANESCO na wizara. Lakini nyaraka za mawasiliano baina ya shirika hilo na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) zimebainisha namna TANESCO ilivyolalamika kuingiliwa kiutendaji na wakubwa hao wa wizara. Katika nyaraka hizo, TANESCO walisema bayana kutopenda kabisa uamuzi wa wizara ambao unafanywa kisiasa, bila kuzingatia utaalamu wakati wa sakata la kutaka kupandisha bei ya umeme. Ushauri wa kitaalamu ambao ulizingatia sababu za TANESCO kutopendezwa na uamuzi wa kisiasa ulifikishwa kwa maandishi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu Jan, 16, mwaka huu. TANESCO katika mawasiliano yake na Ewura iliweka wazi namna “isivyopendezwa hata kidogo na uamuzi wa serikali, na inaona hakuna uwezekano wa kusikilizwa kila inapopeleka suala hili na kuelezea madhara yatakayopatikana baada ya kuondoa maombi ya dharura ya kupandisha ushuru”. TANESCO katika maelezo yake, ilitoa sababu nne; kwanza ikisema kiwango cha ruzuku kinachopangwa na Ewura kilionesha kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya kupanda na kushuka kwa thamani ya fedha, kwa mantiki hiyo hata kama ushuru huo ungetumika usingeisaidia TANESCO. “Hali ya hewa pia siyo nzuri, kuna upungufu wa mvua unaosababisha upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, hivyo zitahitajika pesa nyingi sana ili kuwezesha ununuzi mafuta au umeme katika mwaka 2013. “Mtiririko wa fedha kutoka serikalini haupo sanjari na mahitaji ya uendeshaji wa TANESCO, na mara nyingi serikali huchelewa kutoa pesa,” ilisema sehemu ya mawasiliano baina ya pande hizo mbili. Shirika hilo liliongeza kuwa, mkopo kutoka Benki ya Dunia utatumika kulipa madeni tu wala sio kuisadia TANESCO, hivyo kwa mtazamo huo, utaratibu wa serikali wa kutoa ruzuku inayotosheleza mwaka mzima, unaweza kufanyika bila kupandisha bei ya umeme, lakini ubuniwe utaratibu mwingine utakaofanya TANESCO iendelee kuonekana kwa macho ya watu kama vile bei imepandishwa, lakini bila kuondoa maombi ya kutopandisha ambako kutazidisha shaka kwa wadau wengine mfano wawekezaji na wabia wa maendeleo. Wiki hii gazeti hili lilimnukuu Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Felchesmi Mramba, akisema kuwa hakuna mgawo wa umeme kwa sasa, na kwamba ikitokea serikali itatangaza. Hata hivyo, kukatika kwa umeme kwa siku nzima katika baadhi ya sehemu kunadhihirisha uwepo wa mgawo wa siri unaoendelea. Pamoja na kukanusha kuwepo kwa mgawo, Mramba alikiri kuwa hali ya umeme haijarejea katika uhalisia wake wa kawaida kiasi cha kuondoka katika hali ya dharura. “Bado mitambo ya dharura tuliyokodi kupambana na hali ya umeme inaendelea kuhitajika, lakini pia mabwawa hayana maji ya kutosha kukidhi mahitaji ya umeme bila kuhitaji mitambo ya matufa,” alisema. Mramba alibainisha kuwa tangu Julai mwaka 2012 hadi Februari 2013, serikali imetumia jumla ya sh bilioni 231.2 kama ruzuku kwa TANESCO kwa ajili ya kununua mafuta ya mitambo. “TANESCO kutoka kwenye mapato yake imetumia jumla ya sh bilioni 423.3 katika kipindi hicho kununulia mafuta, hivyo fedha yote iliyotumika kununulia mafuta ndani ya kipindi hicho ni sh bilioni 654.5,” alisema Mramba. Kauli ya Mramba inaonesha kuwa hata kama TANESCO ingeamua isilipe mishahara wala isifanye matengenezo ya mitambo, isinunue vifaa vya kuunganishia wateja, au isiingie gharama nyingine zozote, bado ingepata hasara ya karibu sh bilioni 90 kila mwezi. Chanzo chetu kutoka Ewura kimesema kuwa walishangazwa na uamuzi wa TANESCO wa kujitoa katika mazungumzo ya kupanda kwa bei ya umeme kwa kiasi kidogo na kwenye upungufu ruzuku ya serikali iweze kufidia, kwa madai ya kutekeleza maelekezo kutoka wizarani. Chanzo hicho, kimekiri wazi kuwa kuna mgawo wa umeme ingawa haujatangazwa rasmi. “Mgawo upo ingawa haupo katika ratiba, ila tukiwauliza TANESCO ambao ndio wasemaji wanadai ni tatizo la miundombinu, au maji hayatoshi na kweli kwa sasa maji hayatoshi Mtera na kama hali ikiendelea hivi hivi Mtera itafungwa. “Kwa sababu mvua za Januari hadi Machi zinazotegemewa hazikunyesha vizuri, na bado maji machache tunayopata toka Mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo tunagawana na wakulima wa mpunga walio katika bonde la Usangi, hapo ndiyo tunajiuliza tutoe maji kwa ajili ya mpunga au kwa ajili ya umeme?” kilisema chanzo chetu. CHANZO:TANZANIA DAIMA
Tanesco., Shirika pekee linalogawa umeme, limeweka luku, watanzania wanalipa, linapataje hasara? kama kuna watu wana daiwa kwanini lisiwakatie? Hasara ya bilioni 90 jamani hebu wana JF kila mmoja arudi aangalie bajeti ya Serikali kuna Wizara ngapi zinapewa Fesha kidogo sana kuliko Ruzuku ya Bilioni 231 zinzotumiwa na Tanesco kutengeneza Dairy na Kalenda, kutolea matangazo ya kukanusha mgawo hata kama tunaona nchi ipo gizani, Hongera gazeti la Tanzania Daima, kwa kueleza kwa ufasaha mambo ambayo magazeti mengine yanaogopa. Watanzania wanatoka nyumbani hawajanyoosha nguo, nyimbani giza, lakini magazeti yanaletewa tangazo kuwa hakuna mgawo yanaleta kwa wananchi
 
TANNESCO ni kicha na sehemu ya kuvuna hela kwa ccm huwezi sema unafanya biashara isyo na faida huku unang'ang'ania si wabinafisishe kama limeshawashinda

Huwa najiuliza sana kwamba mr Clean alibinafsisha mashirka yoooote, hili aliliacha kwanini????
 
Kwanini ilo Shirika wasiwape wawekezeja hata kama tukiuziwa umeme kwa sh. 2,000 kwa kila unit liwalo na liwe!
 
Ishu ni nzito,hawa wakubwa niakina nani?wakiruhusu ushindani,mie nitafwetua invetors za kufua umeme kwa wingi kwa gharama nafuu.au!
 
Back
Top Bottom