Peter Agostino
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 105
- 226
Mafanikio katika jambo lolote lile maishani mwanadamu analolenga kufanya hutokea nje ya uwanja wake wa faraja, kwa kimombo wanasema, “outside of your comfort zone”,. Unataka kuwahi kazini, shuleni au kwenye biashara zako kwa lengo la kuzidisha mafanikio, ufanisi au kipato zaidi, ni lazima ukubaliane na kuachia shuka, kukatisha usingizi wako mtamu wa alfajiri na kupambana na umande wa asubuhiasubuhi kwenye nyasi katika uchochoro unaotoka nyumbani kwako kabla hujafika stendi kupanda basi.
Unataka mwili wako kuwa imara(fiti), ni lazima kwanza uvuje jasho jingi kwa mazoezi nk. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa katika biashara au sekta nyingine zozote zile za kimaisha. Mafanikio yanamtaka mtu kuchukua hatua ambazo mara nyingi haziwezi kumpendeza hata kidogo, na hali hiyo ya kutokupendezwa ndiyo tunayopigana nayo kila siku ndani ya fikra zetu, na ili tufanikiwe basi ni lazima tushinde vita hiyo ya kifikra kabla hatujaanza kusaka njia kuu za mafanikio katika maisha.
Binadamu mara nyingi tumekuwa tukisaka siri za mafanikio katika mambo mbalimbali tunayoyafanya kama vile, jinsi ya kufanikiwa kibiashara, jinsi ya kupata pesa, kufanikiwa katika masomo, au katika maeneo mengine yeyote yale kwenye maisha. Ukweli ni kwamba majibu ya swali hilo wala siyo magumu hata kidogo kwani siri kuu za mafanikio hujidhihirisha zenyewe katika mifano ya vitu, watu na hata mambo mbalimbali yanayotokea kwenye mazingira yetu ya kawaida kabisa.
Mifano hiyo katika maisha ya kawaida ndiyo leo nataka nikutajie katika makala hii, hivyo karibu sana tujifunze pamoja, hakikisha unaisoma makala hii mpaka mwisho kupata manufaa yote yaliyokusudiwa. Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho kuisoma makala hiyo yote katika blogu ya jifunzeujasiriamali.
SIRI NYINGI ZA MAFANIKIO HUJIFICHA KWENYE VITU VIDOGOVIDOGO KAMA HIVI...