Siri mgogoro wa gesi yafichuka

Siri mgogoro wa gesi yafichuka

Sidhani kama suala la gesi limeisha. Kuna maswali mengi kuliko majibu. Kama wananchi walipotoshwa na hawakupewa taarifa sahihi naye aliyepaswa kutoa taarifa sahihi? Kwanini kunakuwa na ombwe la taarifa sahihi katika nchi hii? Lakini kwa hali halisi kuna mantiki gani kusafirisha gesi hadi Dar ili kuzalisha umeme badala ya kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha hadi Dar? hebu watoe gharama za kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha hadi Dar ilizilinganishwe na kujenga bomba la gesi hadi Dar.
 
wanaharakati walioitwa wachochezi na walifanikisha azma zao.
1.nyerere
2.kenyata
3.kwame nkuruma
4.nelson mandela
5.mahlangu
6.steve biko
7.indira gandhi.
8.martin ruther king
na hawa wote waliitwa wachochezi wavunja amani na nchi zao zote zilifanikiwa kupata uhuru kutoka mikononi mwa wezi wachache watawala wa wakati huo.
sasa dr slaa nayeye atafanikiwa kuirejesha nchi mikononi mwa wananchi, kutoka mikononi mwa watawala wachache wezi wa rasilimali za taifa (ccm)mapambano ndio yanaanza ccm fungeni mikanda hakuna kulala lazima tuwaondoe tu.

Mkuu,

kwa Quotation haya maneno ni mengi ila nimeyapenda sana. Wewe GT, keep it up!
 
Kwann nchmbi anakimbilia kusitisha shughuri za kisiasa? Anaogopa nn? Anatetea chama gani ? Hivi ni waziri wa ccm au wa watanzania? Ss nimeamini wanakwenda kukabidhi nchi Havana pa kushika utelezi kila pahala kweli kifo cha nyani, chezea Dr. Slaa ww? Mbona alisema nikikosa urahisi nitabaki kukijenga chama ? Hamkuelewa ss mnajuta.
 
Sidhani kama suala la gesi limeisha. Kuna maswali mengi kuliko majibu. Kama wananchi walipotoshwa na hawakupewa taarifa sahihi naye aliyepaswa kutoa taarifa sahihi? Kwanini kunakuwa na ombwe la taarifa sahihi katika nchi hii? Lakini kwa hali halisi kuna mantiki gani kusafirisha gesi hadi Dar ili kuzalisha umeme badala ya kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha hadi Dar? hebu watoe gharama za kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha hadi Dar ilizilinganishwe na kujenga bomba la gesi hadi Dar.
Hapo umenena,kwa mtu aliyeangalia taarifa aliyoitoa Dr.Nchi kwa waandishi wa habari inaonyesha mgogoro haujaisha ila umetulizwa kwa sababu amesema ulinzi umeimarishwa na vyombo vya usalama.sasa kama suala hili limeisha kwa nini ulinzi umeimarishwa?Ungekuwa umeisha tulitegemea tuona akina na Hawa ghasia wakipeana mikono na wananchi wa mtwara kama ishara ya amani na kusahau yaliyotokea.Kinachoigharimu serikali ya ccm ni uongo wa wazi ambao badala ya kumaliza tatizo unaongeza hasira za watu.
 
Huyu mbona anafahamika bingwa wa kuhairisha migogoro mizengo kayanza peter pinda!!!!!!!!!!!!!!

Kweli kabisa.
Hata mgogoro wa madaktari aliuahirisha na matokeo yake ni suala la Ulimboka.
Kwa hili la gesi nadhani hali itakuwa mbaya kwa kuwa Pinda hana mamlaka ya kutekeleza alichoongea au kuahidi
 
He Jamani huyu Dr wa ajabu ajabu, Nchimbi anasema ikibidi watasitisha harakati zote za Kisiasa Mkoani, Mtwara. Jamani hivi hawa viongozi wa Tanzania wakoje???? Hivi huyu chimbi anajua kuwa moto wa Kisiasa ni mkali na hatari kuliko huo wa Gesi?? Jamani, hiki kinchi Tanzania kikoje? Hivi tutaongozwa na viongozi wa sampuli hii mpaka lini jamani? Kweli inakatisha tamaa du...
 
Nahisi ngoma bado

hata mimi naona kama jamaa wamepumzika huku wakiipasha ngoma moto ili watakapoanza tena ivume vizuri, sijajua viongozi wetu huwa wanafikiri nini hasa khs wananchi wanaowaongoza? natamani nijue.
 
Back
Top Bottom