Siri mgogoro wa gesi yafichuka

Siri mgogoro wa gesi yafichuka

Obesity

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
111
Reaction score
46
Siri mgogoro wa gesi yafichuka
MOJA ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa nishati hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.

Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.

Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, Januari 25 na 26 mwaka huu na kufanikiwa kuzima mgogoro huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya wadau wa gesi mkoani humo.
"Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa siyo kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja," alisema Pinda na kuongeza:

"Pamoja na hayo nikachukua maelezo kuhusu matatizo yao mengine na nikawaahidi kwamba nitayafikisha katika mamlaka husika ili waweze kuona namna ya kufanya."

Madai kwamba gesi hiyo inapelekwa Bagamoyo yalikuwa moja ya ujumbe mkuu uliokuwa umeandikwa kwenye baadhi ya mabango wakati wa maandamano ya Desemba 27 mwaka jana yaliyofanyika Mtwara Mjini, yakiratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani.

Pinda alisema viongozi wa kisiasa mkoani Mtwara wakiwamo wabunge, wameonekana kuwa na mpasuko unaosababisha uchochezi kwa makundi ya watu.

Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Waziri Mkuu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Alhaji Masoud Mbengula alikiri chama hicho kumeguka na akataja sababu kuwa ni makundi yaliyotokana na uchaguzi wa ndani uliofanyika mwaka jana.

"Tusiwe wanafiki, ni kweli kuna makundi ndani ya chama… wabunge hawako pamoja na ndiyo hali iliyotufikisha hapa… suala hili lipo wazi kabisa," alisema Alhaji Mbengula.

Kamati ya Spika hatihati
Akizungumzia Kamati ya Bunge iliyotarajiwa kuundwa na Spika kwenda Mtwara kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi wa huko, Pinda alisema hawezi kuingilia mhimili huo wa Dola isipokuwa atatoa taarifa bungeni na kama Spika ataona wabunge wameelewa, basi ataamua lolote.

"Nitakuwa na nafasi ya kuzungumzia jambo hili ndani ya Bunge na Spika akiona wabunge wamenielewa bila shaka atasitisha lakini akiona bado inafaa ataamua yeye," alisema.

Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari jana, kiongozi huyo alifanya mazungumzo na Mawaziri wanaotoka Mkoa wa Mtwara ambao ni George Mkuchika (Utawala Bora) na Hawa Ghasia (Tamisemi) pamoja na wawekezaji wa kutoka China ambayo alisema yalilenga kuwapa halihalisi ya huko.

Nchimbi afunguka
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema vurugu hizo zimefikia mwisho na Serikali haitavumilia tena machafuko ya aina hiyo.

Dk Nchimbi alisema timu ya wataalamu ipo Mtwara kuweka mambo sawa na kusema Serikali itatimiza majukumu yake pasi na shaka yoyote na kusisitiza kuwa haiwezi kukubali Tanzania ikawa vipande.
Alisema Serikali inafanya tathmini kujua hali ilivyo Mtwara na ikibidi itasitisha shughuli zote za kisiasa mkoani humo.

source:gazeti la mwananchi
 
Pinda hakuzima vurugu za Mtwara...waseme amefanikiwa kutuliza munkali wa wanamtwara. Wanamtwara wanasubiri waone ahadi walizopewa na Pinda na hao Mwaziri waliokwenda huko. Kama mambo yatakuwa ndivyo isivyo upo uwezekano wa kuibuka tena vurugu maana wanamtwara wame-test kina cha maji na wametambua kumbe inawezekana kudai haki zao za msingi na wakazipata. wamefanikiwa kuipigisha magoti serikali .
 
Viongozi wa ccm ni mbulula kweli kweli ya Nchimbi na phd yake ya kuforge anataka kusitisha shughuli za kisiasa Mtwara apeleke udictator wake huko nyamba.......
 
uandishi wa mwananchi uko kishabiki zaidi ili kupoteza uhalisi wa nia na lengo la kupinga gesi. wananchi wanahoji stake yao nipi kwenye utajiri huu wa gesi. kupelekwa bgamoyo ilikuwa ni chachandu za maandamano. kweli magamba hawana akili. hawa watu ni mediocres kuanzia kwa mkiti hadi kwa mwanachama.

watanzania hebu tupumzishe hii mibakaji ya utajiri wa nchi yetu maana nahisi yatakujatokea ya Niger Delta huko Nigeria. Mijitu ya Afrika haina uwezo wa kuplan, magamba yanataka qwik fixes ili mradi yeyewe ymeshaona mgao wao huku yakisahau kuwa ile ndo defining resource kati ya ufukara na neema.

tukirudi kwa waandishi wa habari na vombo vya habari, sijaona sijaona ujuzi wowote katika swala la ges isipokuwa propaganda mfu kama iliyoandikwa na mwananchi. sijaona hata documentary moja kwenye vi-tv vya kishamba vya bongo japo kuonesha nchi zingine zenye gesi zilipofikia kimaendeleo,zaidi ya kuonesha chereko, woman of steel na ze comedy. hopeless in fwact nasikia uchungu sana......Aargh!!!!
 
Siri mgogoro wa gesi yafichuka

pinda.jpg

[TD="align: right"] Submit Cancel
[/TD]

MOJA ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa nishati hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.

Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.

Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, Januari 25 na 26 mwaka huu na kufanikiwa kuzima mgogoro huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya wadau wa gesi mkoani humo.
"Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa siyo kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja," alisema Pinda na kuongeza:

"Pamoja na hayo nikachukua maelezo kuhusu matatizo yao mengine na nikawaahidi kwamba nitayafikisha katika mamlaka husika ili waweze kuona namna ya kufanya."

Madai kwamba gesi hiyo inapelekwa Bagamoyo yalikuwa moja ya ujumbe mkuu uliokuwa umeandikwa kwenye baadhi ya mabango wakati wa maandamano ya Desemba 27 mwaka jana yaliyofanyika Mtwara Mjini, yakiratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani.

Pinda alisema viongozi wa kisiasa mkoani Mtwara wakiwamo wabunge, wameonekana kuwa na mpasuko unaosababisha uchochezi kwa makundi ya watu.

Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Waziri Mkuu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Alhaji Masoud Mbengula alikiri chama hicho kumeguka na akataja sababu kuwa ni makundi yaliyotokana na uchaguzi wa ndani uliofanyika mwaka jana.

"Tusiwe wanafiki, ni kweli kuna makundi ndani ya chama… wabunge hawako pamoja na ndiyo hali iliyotufikisha hapa… suala hili lipo wazi kabisa," alisema Alhaji Mbengula.

Kamati ya Spika hatihati
Akizungumzia Kamati ya Bunge iliyotarajiwa kuundwa na Spika kwenda Mtwara kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi wa huko, Pinda alisema hawezi kuingilia mhimili huo wa Dola isipokuwa atatoa taarifa bungeni na kama Spika ataona wabunge wameelewa, basi ataamua lolote.

"Nitakuwa na nafasi ya kuzungumzia jambo hili ndani ya Bunge na Spika akiona wabunge wamenielewa bila shaka atasitisha lakini akiona bado inafaa ataamua yeye," alisema.

Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari jana, kiongozi huyo alifanya mazungumzo na Mawaziri wanaotoka Mkoa wa Mtwara ambao ni George Mkuchika (Utawala Bora) na Hawa Ghasia (Tamisemi) pamoja na wawekezaji wa kutoka China ambayo alisema yalilenga kuwapa halihalisi ya huko.

Nchimbi afunguka
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema vurugu hizo zimefikia mwisho na Serikali haitavumilia tena machafuko ya aina hiyo.

Dk Nchimbi alisema timu ya wataalamu ipo Mtwara kuweka mambo sawa na kusema Serikali itatimiza majukumu yake pasi na shaka yoyote na kusisitiza kuwa haiwezi kukubali Tanzania ikawa vipande.
Alisema Serikali inafanya tathmini kujua hali ilivyo Mtwara na ikibidi itasitisha shughuli zote za kisiasa mkoani humo.

source:gazeti la mwananchi
mpasuko hauwezi kuzibika kwa kauli na mtazamo wa kitaahira kama wa kutishia kuzuia shughuli halali za kisisa mtwara

au kutisha wananchi kwa mitutu ya bunduki waliyoinunua wenyewe kwa michango ya kodi zao

au kwa kudhani kudai haki ya msingi ni kuligawa taifa tofauti na hoja ilivyo.

mbona maelezo ya waziri mkuu yako wazi yakionyesha udhaifu ulipo?
 
Mhh-haya sasa makubwa. WM anaamini katika hilo na hata kuwambia waandishi wa habari (umma wa TZ hivyo)? Mbona mabango mengine hakuyazungumzia? Aliona hilo tu? hayo yalikuwa maneno ya watu waliochoka na kukata tamaa dhidi ya maendeleo katika eneo lako. Mbona la Barabara ya kusini miaka 51 bado, bomba la gesi kwenda Dar miezi 18 hakulisema? AAche unafiki na undumilakuwili =akue kama bado anahisi anaweza kudanganya watu wakakubali. Ukweli uko wazi, kama wananchi hawakushirikishwa kama alivyokiri aliatarajia wananchi wabuni au waote? matokeo yake ndo hayo-lack of information or poorly informed- Badilika WM-wewe ndo serikali ati-hatutegemei tena kusikia uupuuzi kama huu kutoka kwako
 
Haya yeye aendelee kujifanya hafahamu wanaMtwara wanataka nini! dalili za mvua amekwisha ziona ila ana taka kuendelea kutembea bila mwanvuli...... Kama anaweza kuzuia moshi kwa mikono haya kila la kheri!
 
lini pinda aliwahi kufanya jambo remarkable zaidi ya kulia bungeni?
 
Huyu mbona anafahamika bingwa wa kuhairisha migogoro mizengo kayanza peter pinda!!!!!!!!!!!!!!
 
kwahiyo Pinda anaamini amemaliza mgogoro wa gesi..!? Let we see, time will tell!
 
Pinda hakuzima vurugu za Mtwara...waseme amefanikiwa kutuliza munkali wa wanamtwara. Wanamtwara wanasubiri waone ahadi walizopewa na Pinda na hao Mwaziri waliokwenda huko. Kama mambo yatakuwa ndivyo isivyo upo uwezekano wa kuibuka tena vurugu maana wanamtwara wame-test kina cha maji na wametambua kumbe inawezekana kudai haki zao za msingi na wakazipata. wamefanikiwa kuipigisha magoti serikali .
tatizo la baadhi ya wakuu serikalini wanadhani watz na hasa wanamtwara ni wajinga na wanaweza kuwapoza na mambo yakaendelea kama kawaida lakini ukiangalia kiundani mengi yanasemwa ila wanamtwara wanajua wanachohitaji na wanaonekana wameshaamua, jibu ni kukipata na wala sio porojo.
Serikali ikilazimisha hili inabidi liibuke la gharama halisi za mradi, mkilazimisha mwishowe itajulikana tu kama RICHMOND!

Mhh-haya sasa makubwa. WM anaamini katika hilo na hata kuwambia waandishi wa habari (umma wa TZ hivyo)? Mbona mabango mengine hakuyazungumzia? Aliona hilo tu? hayo yalikuwa maneno ya watu waliochoka na kukata tamaa dhidi ya maendeleo katika eneo lako. Mbona la Barabara ya kusini miaka 51 bado, bomba la gesi kwenda Dar miezi 18 hakulisema? AAche unafiki na undumilakuwili =akue kama bado anahisi anaweza kudanganya watu wakakubali. Ukweli uko wazi, kama wananchi hawakushirikishwa kama alivyokiri aliatarajia wananchi wabuni au waote? matokeo yake ndo hayo-lack of information or poorly informed- Badilika WM-wewe ndo serikali ati-hatutegemei tena kusikia uupuuzi kama huu kutoka kwako

Hapo umenena mkuu....
 
urasimu wa kuwaibia gesi wanamtwara ingefanyika mwaka 1972 wakati ule watz wengi walikua black kichwani na sauti ya rais iliheshimiwa zaidi ya Mungu, kwa sasa its oo late...
 
Mbona simuoni bigshow,au alikua miongoni wa casualt za fujo?
 
Mie cijaona hata hiyo ciri hapo.. Naomba anijuze hili.. Ni kwanini alimuamrisha Mkuu wa Mkoa kuomba radhi wananchi wa Mtwara..? Kwa nini kwenye ziara zake hizo hakuongozana na Mkuchika na Ghasia..?
 
wanaharakati walioitwa wachochezi na walifanikisha azma zao.
1.nyerere
2.kenyata
3.kwame nkuruma
4.nelson mandela
5.mahlangu
6.steve biko
7.indira gandhi.
8.martin ruther king
na hawa wote waliitwa wachochezi wavunja amani na nchi zao zote zilifanikiwa kupata uhuru kutoka mikononi mwa wezi wachache watawala wa wakati huo.
sasa dr slaa nayeye atafanikiwa kuirejesha nchi mikononi mwa wananchi, kutoka mikononi mwa watawala wachache wezi wa rasilimali za taifa (ccm)mapambano ndio yanaanza ccm fungeni mikanda hakuna kulala lazima tuwaondoe tu.
 
Siri mgogoro wa gesi yafichuka

Dk Nchimbi alisema timu ya wataalamu ipo Mtwara kuweka mambo sawa na kusema Serikali itatimiza majukumu yake pasi na shaka yoyote na kusisitiza kuwa haiwezi kukubali Tanzania ikawa vipande.
Alisema Serikali inafanya tathmini kujua hali ilivyo Mtwara na ikibidi itasitisha shughuli zote za kisiasa mkoani humo.

Huku ndiko kusema bila kufikir,i yenye ni kama nani kusitisha shughuli za kisiasa.
Ana sahau kuwa hata yeye anafanya shughuli za kisiasa .Labda aanze yeye kuachia ngazi na hii itasaidia kuwa hafanyi shughuli za kisiasa kwa upendeleo.

Kauli kama hizi mara nyingi ndiyo mwanzo /vichocheo vya vurugu!
 
Unapokuwa unachezea Yanga kumbe wewe ni Simba na ukajitahidi kuficha ukweli huo kwa muda usifikiri unafiki huo utadumu milele. Serikali yetu inapanda bangi huku ikidanganya watu wake kuwa haikuwa imepanda bangi,bali maharage ya Mbeya! Watu hawawezi kurubuniwa wakijua wazi kuwa wanaghiribiwa na wakakaa kimya;sasa serikali hii inavuna ilichopanda halafu wanakimbilia kumlaumu Dr Slaa.
 
Back
Top Bottom