Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,939
*JE,WAZIJUA SIRI KUMI ZA NDOA*
1. *KILA UNAEMUOA AU KUOLEWA NAE ANA UDHAIFU WAKE*
*Mungu* pekee ndiye hana udhaifu, Kila ua waridi unaloliona lina chimbuko lake.
2. *KILA UNAEMUOA AU KUOLEWA NAE ANA HISTORIA YAKE MBAYA*
Hakuna mtu ambae ni malaika,epuka kuchunguza mambo ya mtu ya nyuma samehe, usahau na songa mbele.
3. *KILA NDOA INA CHANGAMOTO ZAKE*
Ndoa sio kitanda cha maua yanayomeremeta kila muda, ndoa zote zenye mafanikio zimepitia misukosuko mingi.
4. *KILA NDOA INA HATUA ZAKE KATIKA MAFANIKIO*
Hatuwezi kuwa sawa, kuna watakaokuwa mbele kidogo na watakaokuwa nyuma kidogo. Kupunguza stress, kuwa mtulivu, fanya kazi kwa bidii na kwa muda muafaka ndoto za ndoa yako zitatimia.
5. *KUOA AU KUOLEWA NI KUTANGAZA VITA*
Ukishaoa au kuolewa ni kuingia katika uwanja wa mapambano,Kuwa tayari kupambana kuulinda ukanda wa ndoa yako.
6. *HAKUNA NDOA ILIYOKAMILIKA*
Hakuna ndoa ambayo imetimilika,Ndoa ni kazi ngumu,jitolee mwenyewe na ufanye kazi ya kuijenga ndoa yako iwe kamilifu.
7. *MUNGU HAWEZI KUKUPA MTU KAMILI UNAYEMTAKA*
Mungu atakupa mtu ili wewe umtengeneze jinsi wewe unavyohitaji yeye awe.
8. *KUOA NI KUJIINGIZA KATIKA HATARI*
Huwezi jua nini kitatokea baada ya ndoa, hali inaweza badilika,hivyo achia nafasi ya marekebisho.
9. *NDOA SIO MKATABA WA MUDA BALI NI MKATABA WA KUDUMU*
Ndoa inahitaji ahadi ya kudumu,mapenzi ni gundi ambayo huwafanya wanandoa kuwa pamoja daima..Talaka huanza katika mawazo.
10. *KILA NDOA HUHITAJI KUJITOA*
Hakuna mapenzi rahisi katika ndoa,huwezi kupenda au kupendwa bila kujitoa nafsi yako kwa dhati.
Sent from my HUAWEI P6-U06 using JamiiForums mobile app