Siri kubwa ya Ruge Mutahaba

.

By Sangu J

Wakati taifa hususani sisi vijana tukiwa kwenye huzuni kubwa kupotelewa kwa ndugu yetu #Ruge Mutahaba mimi napendelea kumuita ( KING OF YOUTH) kwa uhodari wa kuhakikisha anajitoa kwa ajili ya sisi vijana wa kitanzania ili tuweze kuleta mabadiliko chanya kwenye Taifa letu.

Inawezekana nimechelewa kwa sababu wakati naandika haya Boss Ruge hatunaye tena kwenye uso wa dunia na hawezi kujibu chochote kwa sababu tunayemsimulia ni mwili ambao mzee wangu Mengi aliuita jina la Kasha.

Nilibahatika kukutana naye mara chache lakini nilishuhudia kupokelewa kwa mwili wake na kikubwa nilichokigundua Boss Ruge aliwekeza zaidi kwa vijana, karibia 85% walikuwa ni vijana ambao ndiyo idadi kubwa ya watu tulijitokeza kumlaki Boss Ruge.

Somo pekee alilothibitisha na ametufunza Boss Ruge ukihitaji kufanikiwa kwenye jambo wahamasishe kwa kugusa maisha ya vijana na kuwajaza uzalendo juu ya TZ na ndiyo jambo kubwa lilimfanya Boss Ruge kutuunganisha vijana na kutambua thamani ya nchi, kulinda raslimali, kujua vijana ndiyo tunaotegemewa na kuivusha nchi hii kutoka tulipo ili kufikia uchumi wa kati.
.
#KijanaMzalendo #IloveTz #PumzikaRuge #SanguJoseph

Sent using Jamii Forums mobile app
Uzalendo ni nini wakuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom