Siri kubwa ya mafanikio ni hii hapa

Siri kubwa ya mafanikio ni hii hapa

Pia usitoe siri zako juu ya chochote utakacho fanya hadi angalau kifikie angalau asilimia 90 kufanikiwa ndipo unaweza waambia watu. Ukiwambia mipango yako kabla ujafanikiwa chance ya kutofanikiwa ni kubwa
Kwanini hii hutokea!?
 
Kwanini hii hutokea!?
Mafanikio yeyeto ya mwanadamu yanaanza katika ulimwengu wa kiroho so likely mipango YAKO kabla kufikia mikononi mwa watu wabaya negative people kupitia nguvu zao hasi ni rahisi kuharibika.
Umeshawahi muona mtu yeyeto mropokaji asiwe na siri au muongeaji Sana amefanikiwa? Kufanikiwa sio kupata hela ya kula tu
 
Ushuhuda
Mimi ni baharia,,nipo melini Saud Arabia,
Kipindi fulani nyuma,,mambo yangu yalikuwa hayaendi,,
nilikaa nyumbani kama mwaka mzima bila kazi,

Kila nikijitahidi kuomba kurudi kazini ikawa ni ngumu Sana,,
Emails hazijibiwi wala watsap hazijibiwi ,
Nilihuzunika Sana.,,

Siku nipo kitandani kabla ya kulala,,
nilikaa na mawazo sana,,
nilikuwa kwenye deep feelings.
Sina hata cent ya kula,,njaa kali sana,

Nikawa naongea mwenyewe Kwa uchungu,,Ee mwenyeziMungu.
--Mimi nimekosa nn?
--Hivi Mimi nimefanya dhambi ipi kubwa hata leo naadhirika hivi?
--Mbona Mimi sio mlevi,,,
--Sina mambo ya kichawi,,
-- Nafanya ibada japo mara 1 Kwa week.

--Ila mimi nina nini haswa kwann siitwi kazini?
--Ee Mungu najuwa upo,,
--najuwa unanisikia ,
--Naomba nipelele kazini.
_Naomba unisitiri na dhiki

Niliongea maneno hayo nipo peke yangu ,,chumbani.
niliongea Kwa uchungu hata kutokwa na machozi na kulia Kwa kwikwi nikiwa peke yangu kitandani.

Baada ya muda nikapitiwa na usingizi,,
Nikashtuka saa 05;30 Am mlio wa simu yangu inaita whtsp call.
Kupokea kumbe ni coordinator wangu wa company yetu,,, ananiomba niingie kwenye email,, nijibu email nirudi kazini..

Haikupita week 2 nikaletewa viza Ili nirudi Saudi Arabia.

Ikiwa bado nasubiri ticket nikapata email tena kwamba nimekuwa rejected na company kujiunga nao sababu sina vigezo.

Nilishangaa sana,,iweje Mimi ni x crew nimepigiwa simu nijiunge na ofisi,
halafu wanitumie kila kitu ila ticket iwe shida,
mwishowe waseme nimekuwa rejected?
yaani Sina sifa za kuwa onboard.
Nilikata tamaa ya kurudi tena kazini..

Miezi 2 imepita nikiwa bado nahangaika ,,Sina matumaini tena kurudi kazini.

Siku Moja usiku kabla ya kulala,,
niliomba Mungu nikasema kwamba --ewe Mungu,,
--Najuwa unajuwa yaliyo wazi na yaliyo fichika.
--Naomba unionyeshe nimekosea wapi?
--Nionyeshe hatma ya safari yangu,,

--Naomba nipeleke kazini,,hakika kwako hakuna kubwa.,
--Wewe ndy mmiliki wa Ardhi na mbingu.
--Usemalo kuwa linakuwa,,Basi iwe Leo nirudi kazini..
Nikapitiwa na usingizi,,

Usiku huo nliota ndoto nipo melini na nimevaa coverall za company yangu.
Nilipoamka asubuhi 07Am,. niliitafakari Ile ndoto lakini nikaipuuza..

11Am napokea whtsp call kutoka office kwamba nimetumiwa ticket nirudi kazini,,
nahitaji ni confirm date of travel..
Nifunguwe email nijibu nataka kuondoka ln?

Hakika baada ya week nikarudi kazini..

Mtoa mada upo sahihi sometimes inapaswa uongee na Muumba wako utapata majibu yote yanayokusumbuwa..

Dunia imejaa kila aina ya uovu,, sometimes kuna watu waovu wanavuruga mipango ya watu kiroho,, kichawi bila kujuwa..
Utahangaika Kwa waganga wote bila mafanikio..

True story
Nakazia hapo
 
Back
Top Bottom