Siri iliyojificha katika kujivua gamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri iliyojificha katika kujivua gamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chibidula, May 27, 2011.

 1. c

  chibidula Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Badala ya kujivua gamba kumbe mwenyekiti alikuwa anaandaa mbinu ya kutafuta mrithi wake ambaye anatakuwa wa ‘type yake’.
  Pamoja na kubadili safu ya uongozi mjini Dodoma, CCM pia ilitangaza kwamba wanachama wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe la sivyo wataondolewa kwa nguvu. Wanachama hao wanatajwa kuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, na wabunge wawili, Andrew Chenge na Rostam Aziz. Ni kweli matajiri hawa hawapendwi na Watanzania wengi isipokuwa wa majimboni mwao tu.
  Lakini pia watu hawa watatu wana sifa nyingine: kwamba ndio tishio pekee na la kweli dhidi ya mpango wa Kikwete wa kusaka Mwislamu wa kumrithi. Watu hawa nia yao kubwa si udini; bali ni ulaji. Wanataka kumweka Lowasa kwenye urais mwaka 2015, mtu ambaye pengine hatalazimika kumheshimu Kikwete na kumlinda. Lakini tatizo kwa Kikwete ni kwamba Lowassa si Mwislamu.
  Kundi hili lina urafiki wa karibu na Makamba ambaye inadaiwa kuwa ndoto yake kubwa haikuwa udini kwa mwaka 2015, licha ya kuwa naye amesikika mara nyingi akijiingiza kwenye siasa za udini; bali anaota mwanae aje kuachiwa urais mwaka 2025 na kundi hili. Makamba hutamba kwamba mwanae anafaa kuwa kiongozi na hakuna ubishi kwamba alihakikisha mwanae anapata ubunge, uenyekiti wa kamati ya Bunge, na kisha kuingia kwenye Sekretarieti ya CCM.
  Aidha, mtoto wa Makamba pia anaelezwa kuwemo kwenye kundi linalowaunga mkono watuhumiwa hawa wa ufisadi ambalo lina idadi kubwa ya wabunge na viongozi wa CCM wa ngazi za wilaya, mikoa na taifa. Hii ndiyo sababu tangu CCM ilipoanza kushambulia mafisadi hadharani, yeye amepotea jukwaani!
  Kimsingi kuna kutofautiana kati ya Makamba na Kikwete kuhusiana na nani awe rais mwaka 2015 na hawa watuhumiwa wa ufisadi wafanyejwe. Hivyo, tangazo la kujivua gamba pamoja na kutajwa kwa watuhumiwa hao ambao Kikwete mwenyewe aliwapigia kampeni mwaka jana kwenye uchaguzi wa wabunge, ni geresha tu. Kikwete alikuwa anaunda timu itakayomrithi mwaka 2015.

  Kimsingi, hadi sasa Kikwete ameshawaacha wabaya wake wote nje ya Kamati Kuu ambao ‘dhambi’ yao kuu ni kuutaka urais wa mwaka 2015. Watu hawa ni Membe, na hili kundi la mafisadi pamoja na Prof. Mark Mwandosya ambaye licha ya kushindwa mwaka 2005 na umri kumtupa mkono, inadaiwa bado anataka kujaribu tena 2015.
  Njama hizi za Mwenyekiti Kikwete ambazo zinaelezwa kwamba ni zoezi la CCM kujisafisha, ingawa upo ukweli pia kutokana na kuigopa CHADEMA, ndizo chanzo na mwisho wa zoezi la kujivua gamba. Hakuna cha zaidi.

  Hivyo basi, hakuna ushujaa wala maamuzi magumu yaliyofanyika Dodoma. Ulikuwa ni ‘usanii’ tu, na ndiyo sababu hakuna kiongozi wa CCM anayepigia kelele mafisadi zaidi ya kijana Nnauye ambaye anaganga njaa na kulipa fadhila za kupewa ukuu wa wilaya na cheo kwenye chama. Hata Chiligati aliyejitokeza mwanzoni sasa ameingia mitini.
  Makamba mdogo naye amekaa mbali; kwani mafisadi hao ndiyo wafadhili wake wakuu kisiasa na maswahiba wa baba yake. Hofu yake ni kwamba, akiwachafua leo na wao watamwacha huko mbeleni au watamng’oa kwenye siasa.

  Malalamiko ya Joseph Butiku hivi juzi kwamba viongozi wa CCM wamemwachia Mwenyekiti mzigo wa kupambana na mafisadi, yamekuja bila kujua ukweli wa mambo. CCM haiko kwenye mapambano na mafisadi; bali Mwenyekiti ndiye anapambana na maadui zake ila tu amepata bahati kwamba watu hao hao ndio wanaolalamikiwa kwa ufisadi. Ni bahati tu ya mtende iliyotoa nafasi ya fitna hii kuchezwa!
  Source (Raiamwema, 25-31, Mei 2011)
   
 2. oba

  oba JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ukweli ukipambanishwa na uongo ukweli hushinda, tutawagundua tu , njia ya mwongo ni fupi!Wapangao hila wajue tuko macho na kwamba watashindana lkn hawatashinda.
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kuna mkeka umewekwa hapa jamvini.....ni bora tuusome wote bila ku-edit, coz kila mstari una maana yake
   
 4. c

  chitage Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  tz ina makubwa,watu wanaota vyeo tu badala ya maendeleo.!
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Pumba za kufikirika!
   
 6. c

  chibidula Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Faizafoxy, ili uweze kuwa great thinker unatakiwa usome yale yanayotokea na kufanya analysis, na kama huna hoja ni bora ukatulia na kusoma kile ambacho watu wanachangia.
   
 7. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Acheni ujinga wenu wa kujadili CDM/CCM hivi hatuwezi jadili mambo ya maendeleo ya nchi yetu? Inakuaje unaleta upupu kama huu?
   
 8. c

  chibidula Member

  #8
  May 28, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kuwepo kwa CDM ndiko kunakosaidi CCM ijirekebishe na kuwaletea maendeleo wananchi otherwise km isingekuwa CDM 'check and balance and not domination of power', je issue ya EPA ingejulikana? Hoja iliopo inaonyesha mpango uliojificha nyuma ya panzia ambao watanzania tuuangalie kwa makini ili tusiweze kujikuta tumetumbukia kwenye tatizo lingine ' its like TAHADHALI' . kwa hiyo mchango wako unasaidia katika kufumbua macho wale waliolala
   
 9. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @Mlengo wa kati, elewa ili ni jukwaa la siasa na CCM &CDM ni vyama vya siasa tena vikubwa apa nchini kwetu, ulitaka tujadili nini? kama unataka kujadili uchumi na mapenzi basi katafute sehemu nyingine. usiongee bila kufikiria
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hivi katika mawazo yako umeona kuna hoja? Khaa! unanchekesha, pumba zikiitwa hoja mchele utaitwaje?
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  May 28, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,776
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe kunasiku yoyote ulishawahi kukubaliana na hoja yoyo yenye kumkosoa kikwete au utawala wake?
   
 12. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 867
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  naona upo gambani kufa na kupona..sijawahi kushuhudia wewe ukikubaliana na hoja yoyote iliyotolewa jamvini ya kumkosoa jk..
   
 13. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  sasa pumba ni zipi?
   
 14. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa upande wako pumba ni hoja yoyote iliyo dhidi ya JK! Tukiwa na mitizamo kama ya kwako tutafika kweli? Kama unamtakia mema JK ni vizuri kumweleza ukweli kama amekaa uchi ili ajifunike nguo badala ya kumpakaa mafuta kwa mgongo wa chupa kwa maslahi binafsi ya kuganga njaa!
   
 15. O

  Omr JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pumbaaaa
   
 16. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  maendeleo yanakuja vipi kama viongozi wa kisiasa hawako vizuri?kuna nchi imeendelea bila vyama vya siasa?
   
 17. O

  Omr JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi zinaendelea zikiwa na vyama vya maana, sasa CDM ndio chama? Chama cha wahuni kitaleta maendeleo Gani?
   
Loading...