Siri iliyo ndani ya Katiba

Mulokozi GG

Member
Jul 14, 2021
34
44
Mfumo wa utawala tulio nao sahivi wa demokirasia katiba ni muongozo wa Taifa kiuchumi, kijamii, michezo na sanaa; hivyo inatosha kusema kuwa katiba ni muongozo wa jumla juu ya uelewa wa jamii inayo tumia katiba husika.

Hili ni dhahili sababu katiba ndio chujio la kile kinacho pokelewa na kuendelea kuwepo kwenye jamii husika. Katiba ni sawa na kiongozi cha mwalimu, kama ilivyo dhahili kwa mjibu wa mitihani hakuna mwanafunzi yeyote mwenye uelewa zaidi ya kiongozi cha mwalimu. Hivyo hata kwenye mataifa yetu uelewa, ujuzi, kasi ya maendeleo na idadi ya wawekezaji wanao wekeza katika Taifa husika ni matokeo ya kabita na sheria za Taifa husika.

Katiba ni sawa na bahari, sisi tunao tumia hiyo katiba ni sawa na viumbe wanao ishi kwenye hiyo bahari. Hakuna kiumbe yeyote hata siku moja ambaye ni mkubwa zaidi ya nyumba/bahari anayo ishi. Hivyo hakuna mtu mwenye akili zaidi ya katiba anayo itumia(kisheria).

Sababu binadamu tunavyo viwango tofauti vya uelewa, katika mda tofauti tofauti Watanzania tunaanza kuhisi na kuona siri na uwezo ulio ndani ya katiba. Tunaanza kuona na kuhisi katiba yetu inaubana uwezo wetu wa kutenda na kufikiri pia, kwani hakuna tendo jema zaidi ya fikira nyuma ya tendo husika.

Katiba iliyo tumika kipindi nchi yetu inapata uhuru nchi ikiwa na wasomi wasiozidi 100 na kufanyiwa marekebisho kidogo tu, ni hatari na ndogo zaidi ya chumba cha mahabusu tukisema tuendelee kuitumia katika nchi ambayo vijana zaidi ya 50,000 wanahitimu Chuo kikuu kila mwaka.

Sauti inayo ongezeka kila kukicha inayo dai maboresho ya kabita inayo tumika kuongezea Taifa la Tanzania, ni sauti inayo paswa kuiamsha akili ya kila anaye litakia mema Taifa la Tanzania. Kwani ukiisoma katiba yetu vizuri ni dhahili bila kujali masilahi binafusi na kutanguliza maendeleo ya Watanzania kuielewa, kiroho, kijamii, kiuchumi, kitekinolojia na katika sanaa na michezo; Katiba mpya ni kitu kinacho paswa kupewa kipaumbele na mtu yeyote anaye litakia maendeleo Taifa hili.

Katiba hii siyo kwa ajiri ya CCM, CHADEMA, ACT Wazalendo, CUF, NCCR Mafeuzi au chama kingine chochote. Katiba mpya siyo kwa ajiri ya kuiweka CUF au CHADEMA madarakani au kwa ajiri ya kuitoa CCM katika madaraka bali katiba mpya ni kwa ajiri ya maendeleo ya kila nafsi ya Mtanzania.

Katiba mpya ni kwa ajiri ya kuleta umoja katika uongozi, uvumivuli wa kisiasa na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali tulizo nazo hivyo kuongeza kasi ya maendeleo katika Taifa letu na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa Watanzania walio wengi.

Hivyo yeyote anaye kwamisha kwa njia moja au nyingine au kugomea mabadiliko ya katiba kwa kujua au kwa kuto kujua, kwa masilahi au kwa sababu ya uoga ajue analisababishia Taifa na kizazi hiki pamoja na kizazi kijacho cha Watanzania hasara kubwa ambayo ni vigumu saana kuipima kwa kitu chochote kinacho onekana. Watanzania tukitanguliza Utanzania, umoja, uzalendo na utu katiba mpya ni ufunguo siyo tu katika furusa za uchumi, umoja na uongozi bali hadi kwenye uelewa na ubora wa matendo ya Watanzania kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom