Sir Isaac Newton aliandika kuhusu 2060 kuwa mwisho wa dunia

Sir Isaac Newton aliandika kuhusu 2060 kuwa mwisho wa dunia

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
993
Reaction score
1,882
‎Wakati wengi wanamkumbuka Isaac Newton kwa kuweka misingi ya physics ya kisasa na kubalilisha jinsi tunavyoelewa ulimwengu kwa ugunduzi wa gravity na laws of motion, watu wachache wanajua kuwa pia alijishughulisha sana na tafsiri za maandiko ya Biblia, hasa kitabu cha unabii cha Daniel na Ufunuo wa Yohane.

‎Sir Isaac Newton ameandika vitu vingi zaidi kuhusu biblia na imani kuliko maandiko yake kuhusu hesabu na physics yakijumlishwa. hivyo alikua curious sana kwenye mambo ya dini.

‎Katika maandishi yake ya binafsi (ambayo hayakuchapishwa wakati wa uhai wake), Newton alijaribu kuchambua namba na alama za kinabii zilizomo kwenye Biblia. Akitumia mahesabu hayo, alifikia wazo kwamba mwaka 2060 unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa mfumo wa dunia wa sasa.
‎Hata hivyo Newton hakusema dunia italipuka au kuangamia kabisa mwaka huo. Alimaanisha kuwa ukawa mwaka ambao utaratibu wa dunia utabadilika sana, na kua mwanzo wa kipindi kipya cha kihistoria au kiroho.

‎Muhimu zaidi, Newton aliandika wazi kuwa 2060 ni mwaka wa mapema zaidi unaowezekana. Lengo lake lilikuwa pia kupinga watu waliokuwa wanatabiri tarehe za mwisho wa dunia, kwa kuonyesha kuwa kwa tafsiri yake tukio hilo haliwezi kuwa mapema hivyo.

‎Kwa hiyo, hata mmoja wa wanasayansi wakubwa kabisa katika historia alikua na curious kujaribu kuelewa siri za wakati wa mwisho, akichanganya sayansi, historia, na tafsiri za maandiko ya dini.
 
There's nothing like mwisho wa dunia.

Hakuna mwisho wa dunia.

Hii Dunia kila mtu aliikuta na kila mtu ataiacha kama ilivyo.

Ukifa ndio mwisho wako wewe mwenyewe, sio mwisho wa dunia.
hakusema dunia itaisha au watuwote watakufa ila aliiongelea itakua mwanzo wa zama mpya kuhusu system mbalimbali kama corruption au labda vita itakuwa old school
 
Hapo katuingiza chaka
hakusema dunia italipuka au kuangamia kabisa mwaka huo. Alimaanisha kuwa 2060 utakua mwaka ambao utaratibu wa dunia utabadilika sana, na kua mwanzo wa kipindi kipya cha kihistoria au kiroho.
( haya ni moja ya maandiko yake ambayo hakua ameyachapisha kwa uma. Sir Newton aliogopa sana kukosolewa alitaka kuwa sahihi mara zote, hata maandiko kuhusu laws of motion na gravity yalichapishwa zaidi ya miaka 20 baadae. baada ya kuandikwa na kukaa ndani tu kwa muda wote)
 
michio kaku alisema pia ndani ya miaka kama 40 au 50 dunia huenda ikaingia kwenye type 1 civilization kutokana na kardshev cilivization scale, hivyo huenda newton alimaanisha hivyo pia
 
Back
Top Bottom