Sipati picha siku ya hukumu itakuaje

Sipati picha siku ya hukumu itakuaje

Hebu fikiria siku ambayo halaiki ya watu imekodoa macho kuangalia matendo yako yote yaliyo ya wazi na yale ya siri.

Hebu piga picha yule rafiki yako uliyemchukulia mke wake anakuona unazini na mke wake.

Hebu piga picha mzazi mwenzako anakuona vile unamtoa kafara mtoto wenu kisa utajirike.

Hebu piga picha tunakuona ukiwa unaroga majirani zako na wakati kanisani au msikitini hukosi.

Hebu piga picha tunaona ukiwapanga majambazi wakavamie kwa mjomba, binamu au baba yako.

Hebu piga picha wewe mchungaji au shehe unaonekana ukizini gesti na mhumini wako.

Hebu piga picha wewe unayetoa kafara raia wasio na hatia ili ushinde uchaguzi wa jimbo lako.

Hebu piga picha ulivyomuaga mmeo kuwa unaenda sokoni au kwa rafiki yako kumbe unaenda gheto la mchepuko wako.

Hebu piga picha siku hiyo kale katabia kako ka kudanganya wana JF. kanaonekana wazi.

Hebu piga picha siku ambayo yule Adam na Hawa uliyemsikia na kumsoma unamuona kwa macho.

Hebu piga picha pale unapogundua kwa mara ya kwanza watoto ulionao sio wako.

Hebu piga picha wafanya kazi wenzako kwa mara ya kwanza wanajua kua ulipata cheo chako baada ya kutanua mabaja.

Hebu piga picha siku ambayo kwa mara ya kwanza JF members tunajua jina lako halisi.

Mimi nimejaribu kupiga picha na kisimu changu sipati picha kamili.

Unaambiwa kila jambo unalolitenda litaletwa hadharani haijalishi la wazi au la siri.

Unaambiwa mimea, mawe , mchanga, vitanda oxgen na kila kitu kinachoonekana na kisichoonekana huwa vinarekodi matukio ya wanadamu.

ASANTENI
Mungu amuhukumu binadamu kwa lipi? Kabla ya Mungu hajamleta mtu duniani hakujua kama huyu mtu akija duniani atakuwa malaya, mwizi, muongo, n.k? Kama alijua kwanini alimuumba hivyo hivyo ilihali anajua kuwa atakuwa ni mzinzi, au muongo, tapeli, n.k na atamuhukumu vipi mtu wakati yeye Mungu ndiye aliyeamua huyo mtu awe hivyo?
 
Mtoa mada umeleta jambo zito sana,ni jambo ambalo wengi watakubeza kwa sababu afya,uzima na dunia inatuhadaa,ili jambo hili kila mtu atalithibitisha siku ambayo roho yake inatengana na kiwiliwili,na ili uweze kulifikiria hili,ni lazima uwe na akili timamu.

Mtu yeyote mwenye akili timamu ni lazima ajiulize maswali haya.

1:Yeye ni nani,jibu ni kiumbe.
2:Na kama ni kiumbe,muumbaji ni nani?ni mungu.
3:Mungu alikosa cha kufanya mpaka ameumba ulimwengu,na viumbe vingi sana?angeweza angekuunba tu wewe mende uwe unaishi chooni,panya,kunguni,mbuni,lakini kwa huruma yake amekuleta kuwa mwanadamu kwa huruma yake lengo ni kufanya mambo ambayo anayaridhia na kuacha makatazo yake..
 
Hii dunia tungekuwa tunaishi kama wanyama ndio ingeifurahia,unafanya lolote tu unalojisikia kufanya muda wowote.
Kwani waliopanga ustarabu, sheria na utaratibu ni Mungu au ni watu?
 
Mtoa mada umeleta jambo zito sana,ni jambo ambalo wengi watakubeza kwa sababu afya,uzima na dunia inatuhadaa,ili jambo hili kila mtu atalithibitisha siku ambayo roho yake inatengana na kiwiliwili,na ili uweze kulifikiria hili,ni lazima uwe na akili timamu.

Mtu yeyote mwenye akili timamu ni lazima ajiulize maswali haya.

1:Yeye ni nani,jibu ni kiumbe.
2:Na kama ni kiumbe,muumbaji ni nani?ni mungu.
3:Mungu alikosa cha kufanya mpaka ameumba ulimwengu,na viumbe vingi sana?angeweza angekuunba tu wewe mende uwe unaishi chooni,panya,kunguni,mbuni,lakini kwa huruma yake amekuleta kuwa mwanadamu kwa huruma yake lengo ni kufanya mambo ambayo anayaridhia na kuacha makatazo yake..
Wakati unajiuilizwa hilo swali jiulize swali lingine ya kwamba laiti kama Mungu angekupa nafasi ya kuchagua kuwa anataka akupeleke duniani #Eidj5# ila utakuwa na matendo ya kukupeleka motoni na mwisho wa siku utachomwa moto; je ungekubali akuumbe?
 
hapw itakuwa balaa

"Hebu piga picha pale unapogundua kwa mara ya kwanza watoto ulionao sio wako..."
 
Hebu piga picha wale Chaputa wakiwa wanapiga Punyeto live bila chenga.
 
Hebu piga picha wale Chaputa wakiwa wanapiga Punyeto live bila chenga.
wakichukuliwa waume kwa wake wapiga chaouta wakahamishiwa bara la antaktika wanaweza kulijaza na nafasi isitoshe
 
Mtoa mada umeleta jambo zito sana,ni jambo ambalo wengi watakubeza kwa sababu afya,uzima na dunia inatuhadaa,ili jambo hili kila mtu atalithibitisha siku ambayo roho yake inatengana na kiwiliwili,na ili uweze kulifikiria hili,ni lazima uwe na akili timamu.

Mtu yeyote mwenye akili timamu ni lazima ajiulize maswali haya.

1:Yeye ni nani,jibu ni kiumbe.
2:Na kama ni kiumbe,muumbaji ni nani?ni mungu.
3:Mungu alikosa cha kufanya mpaka ameumba ulimwengu,na viumbe vingi sana?angeweza angekuunba tu wewe mende uwe unaishi chooni,panya,kunguni,mbuni,lakini kwa huruma yake amekuleta kuwa mwanadamu kwa huruma yake lengo ni kufanya mambo ambayo anayaridhia na kuacha makatazo yake..
Asante mkuu
 
Kwani walivileta akina nani? Tatizo letu tumekaririshwa vibaya na tunashindwa kujihoji sisi wenyewe. Na hivyo vitabu vimetudumaza hatutaweza kuendelea
Binafsi kitabu kiitwacho Biblia nakiamini sana maana ni cha ajabu sana.

Kimejaa ahadi na sheria na shuhuda za kweli kabisa...

Elimu niliyoipata hapa duniani mpaka level ya juu kabisa...bado cjaona kama inafikia hekima ya hiki kitabu mkuu..

Nakushauri ukisome.
 
Kotekote kivipi? Naomba nieleweshe wa kwanza kausikaje na mwingine kausikaje kwenye kupanga hizo sheria, taratibu na ustarabu?
Sio la muhimu maana hoja yangu kuwepo hizo sheria na taratibu ambazo zinatufanya tusijiachie kama wajachiavyo wanyama.
 
Sio la muhimu maana hoja yangu kuwepo hizo sheria na taratibu ambazo zinatufanya tusijiachie kama wajachiavyo wanyama.
Ndio maana nimekuuliza hizo sheria na taratibu zimepangwa na nani?
 
Ndio maana nimekuuliza hizo sheria na taratibu zimepangwa na nani?
Kupangwa na nani sio muhimu,japo siku zote wachache tu katika wengi ndio hupanga cha muhimu ni kwamba zipo na mtu ukifanya kinyume hizo sheria zinafanya kazi.

Mfano kwa starehe zako mwenyewe ila unazuiliwa kuvuta bangi au kutumia madawa ya kulevya,yani tunaishi kadri sheria zinavyotaka.

Mara unafungwa miaka 30 kisa una mahusiano na mwanafunzi ambaye ameshatoa sana mimba..ahhh
 
Back
Top Bottom