Sipati picha siku ya hukumu itakuaje

Hakuna siku ya mwisho, we kama huitumii dunia kisa eti utaingia sijui peponi unapoteza muda wako. Waliotuletea dini ndo wanaogoza kwa zambi za kuuana na kutuletea virusi vya magonjwa, ndo wanaoongoza kwa roho mbaya jiulize mbona hawafikirii hayo ya peponi/motoni?
Sio wote mkuu..halafu usifuate mtu fuata vitabu.
 
KWA WAKRISTO

1. Waebrania 9: 27

2. Warumi 14: 10-12

3. 2Wakkritho 5: 10

4. 1petro 4:5

5. Yohana 12: 31

Kuna mafungu zaidi ya 60 kwenye biblia.


KWA WAISLAMU

Quran 80: 33-42

ASANTE
nimeyasoma hakuna mahali nimesoma..
kutakuwa na picha...
pia sijasoma hukumu itakuwa inahusisha kikundi cha watu eti kwamba wengine ni watazamaji...
hukumu ya Mungu ni kamilifu hahitaji mashuhuda
 
Hebu fikiria siku ambayo halaiki ya watu imekodoa macho kuangalia matendo yako yote yaliyo ya wazi na yale ya siri.

Hebu piga picha yule rafiki yako uliyemchukulia mke wake anakuona unazini na mke wake.

Hebu piga picha mzazi mwenzako anakuona vile unamtoa kafara mtoto wenu kisa utajirike.

Hebu piga picha tunakuona ukiwa unaroga majirani zako na wakati kanisani au msikitini hukosi.

Hebu piga picha tunaona ukiwapanga majambazi wakavamie kwa mjomba, binamu au baba yako.

Hebu piga picha wewe mchungaji au shehe unaonekana ukizini gesti na mhumini wako.

Hebu piga picha wewe unayetoa kafara raia wasio na hatia ili ushinde uchaguzi wa jimbo lako.

Hebu piga picha ulivyomuaga mmeo kuwa unaenda sokoni au kwa rafiki yako kumbe unaenda gheto la mchepuko wako.

Hebu piga picha siku hiyo kale katabia kako ka kudanganya wana JF. kanaonekana wazi.

Hebu piga picha siku ambayo yule Adam na Hawa uliyemsikia na kumsoma unamuona kwa macho.

Hebu piga picha pale unapogundua kwa mara ya kwanza watoto ulionao sio wako.

Hebu piga picha wafanya kazi wenzako kwa mara ya kwanza wanajua kua ulipata cheo chako baada ya kutanua mabaja.

Hebu piga picha siku ambayo kwa mara ya kwanza JF members tunajua jina lako halisi.

Mimi nimejaribu kupiga picha na kisimu changu sipati picha kamili.

Unaambiwa kila jambo unalolitenda litaletwa hadharani haijalishi la wazi au la siri.

Unaambiwa mimea, mawe , mchanga, vitanda oxgen na kila kitu kinachoonekana na kisichoonekana huwa vinarekodi matukio ya wanadamu.

ASANTENI
Hebu picha picha ulivyo hide your ID!
 
Hakuna siku ya mwisho, we kama huitumii dunia kisa eti utaingia sijui peponi unapoteza muda wako. Waliotuletea dini ndo wanaogoza kwa zambi za kuuana na kutuletea virusi vya magonjwa, ndo wanaoongoza kwa roho mbaya jiulize mbona hawafikirii hayo ya peponi/motoni?
Hii dunia tungekuwa tunaishi kama wanyama ndio ingeifurahia,unafanya lolote tu unalojisikia kufanya muda wowote.
 
Back
Top Bottom