Euphransia
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 937
- 778
Wadau nadhani wakati wa kutokuwa Na Wabunge ni sasa.Nimefikia uamuzi huo baada ya kuliona Bunge letu halina uwezo wa kuiagiza Serikali Na Serikali ikalazimika kutekeleza.Mifano ni mingi Serikali kuligomea Bunge.Kwa mfano wakati wa sakata la Escrow kuna maagizo yalitolewa Na Bunge lakini Serikali haujatekeleza Na Bunge liko kimya.Jana wabunge walitaka suala la Utekwaji watu Serikali itoe Tamko lakini Serikali haikutoa .Kuna miradi inaendelea hapa nchini bila Bunge kujua Kwa maana ya kupanga Bajeti ya miradi hiyo.Binafsi naona fedha wanazolipwa Wabunge zingepelekwa kwenye Miradi ambayo ndio wananchi wanataka.