Sioni uhalali wa kuwepo kwa TFDA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sioni uhalali wa kuwepo kwa TFDA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Apr 3, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tanzania Foods and Drugs Administration(TFDA) ni shirika lililoundwa kisheria ili liweze kuwalinda wananchi dhidi ya madhara yanyoweza kuwapata kwa kutumia dawa na vyakula visivyo faa.Hata hivyo shirika hili linalo ongozwa na mama Ndomondo limeshindwa kazi hiyo kabisa.Si mchukii Mama Ndomondo lakini ninachotaka mimi ni ufanisi,ambao sioni kabisa katika shirika hili.

  Katika tukio la hivi karibuni ambalo kwangu mimi ni kichekesho,mwananchi mmoja aligundua uwepo wa Metakelfin fake na aka-blow the whistle.Ninachojiuliza ni kwamba hivi TFDA imeachia wanachi ambao hata utaalam hawana, kazi ya ku-dentify madawa fake nchini?Na imekuaje TFDA iachie dawa hiyo ivuke mpaka wa Tanzania na hata kuuzwa kwenye maduka ya dawa.Hivi si kazi ya TFDA kuhakikisha kwamba dawa fake haziingizwi nchini mwetu kabisa?Katika uzembe huu,tunajua ni watanzania wangapi wameathirika kwa kunywa dawa hii,na ni wangapi wamekufa?Katika mazingira ya namna hii,inaonyesha wazi kwamba kuna dawa nyingi fake ziko kwenye shelves za maduka ya dawa,na watanzania maskini wengi wanaendelea kuathirika na kufa bila kuwa na chombo dhabiti cha kuwatetea!Hali hii ya kutisha itaachiwa iendelee hadi lini.

  Tumeshawahi kupigia kelele uwepo wa dawa fake kujaa kwenye maduka yetu lakini hakuna mtu anayesikiliza.Sio siri tena kwamba ukifika dukani,kama unaumwa malaria unaulizwa dawa ipi inakutibu.Ni aibu sana.Hivi mwananchi wa kawaida, asiyekuwa hata na chembe ya ufahamu juu ya madawa katika hali hii ataishi vipi?Kila mtu anajua yaliyotokea baada ya kuondoa Chloroquine kama tiba ya Malaria, ni aibu tupu.Hivi tunaelekea wapi.Mara SP,mara Quinine,mara Aluu,tunatangatanga tu.Kwa kweli mazingira yaliyopo kwenye mfumo mzima wa madawa ni wa kifisadi na kitapeli.Mazingira ambayo wenye nguvu kifedha wameachwa wafanye wanalotaka,wachezee afya za walala hoi wafe kama panzi,huku wao wakiendekea kujitajirisha.Ni mchezo mchafu sana.
  TFDA hasa ina kazi gani?Hapana, kwa kweli sioni.

  Sasa kwa vile,TFDA imeamua tulinde afya zetu,basi ni vema wakapokea tips hizi ili wazifanyie kazi.
  *Mwaka 2002 Deutch Welle waliongelea uwepo wa Cyproflaxin inayotengenezwa Ujerumani ambayo ni fake,na ambayo ni vigumu kuitofautisha na Cyproflaxin halisi,na ambayo inasambazwa duniani kote.
  *Mwaka wa jana mimi binafsi nilifungua capsule ya Chloramphenicol na kugundua kwamba unga uliokuwepo haukuwa mchungu kabisa, jambo linalo ashiria kwamba unga ule haukuwa wa active ingridient halisi ya Chloramphenicol.
  *Brands za Panadol zilizoko madukani sasa hivi nyingi zinamomonyoka kama bonge la udongo na ukiweka kwenye maji ndio kabisaaa, zinasambaratika mara moja, jambo linaloashiria kwamba si panadol halisi ila lipo tatizo!
  *Kwa ujumla matatizo ya madawa ni makubwa,na kama TFDA haikufanya kazi yake inavyotakiwa,we are sitting on a time bomb.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,260
  Trophy Points: 280
  Uhalali wa TFDA ni mambo ya legality, tofautisha na umuhimu, ili usione uhalali, there must be illegality, na ili usione umuhimu, ni kuifikiria kama TFDA haipo.
  Naomba tusizungumzie uhalali wa taasisi halali, bali pia umuhimu wa TFDA uko pale pale pamoja na matatizo ya hapa na pale katika utekelezaji. Panado ni madawa baridi ambayo hayahitaji kuandikiwa na daktari yanauzwa maduka yote kuanzia maduka ya dawa, dukawalla,kwa mangi mpaka kwenye vibanda kama voucher. kuwalaumu TFDA ni kuwaonea.
  madawa makubwa kama meterkelvin, na antibiotics zote, zinatakiwa cheti cha daktari na maduka rasmi ya dawa yenye mkemia na ambayo huwa yaakaguliwa. ukifanyautafiti, utagunduamaduka ya ukweli, yanuza dawa za ukweli.
  tatizo ni sisi watuniaji wa madawa kutaka kununua madawa ya ukweli toka kwenye maduka ya dawa baridi, unategemea nini?.
  wenye hayo maduka ya dawa baridi, hawana vibali kuuza madawa ya ukweli, hata ukiuliza, utaona muuzaji anaingia ndani, ndio anakuja na dawa.
  dawa za ukweli ni expensive, wabongowengi tunapenda rahisi. unategemea yule muzaji wa uswahilii akiweka dose ya ukweli ya antibiotics ya sh.30,000/=, nani atanunua?.
  tunayalea maduka yasiyostahili kuuza dawa, tukiuziwa dawa fake, tunalalamika.
  Naomba pia tutenganishe issue ya madawa yasiyofaa na madawa feki.
  kwa Tanzania yetu TFDA inajitahidi sana mpaka hapa tulipofika. kwa sisi wa zamani, tuakumbuka enzi za soko la kimataifa la Tandika, kila dawa ziliuzwa mkononi.
  Idumu TFDA ila iboreshe utekelezaji wa majukumu yake.
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mkuu nahisi kuna haja ya kuangalia sheria ya kuanzishwa kwa mamlaka hii kwani bado ni dhaifu sana. Kusubiri madawa yaingie nchini hadi yasambazwe madukani halafu kuchukua waandishi wa habari kwenda kukagua maduka matatu ni dhamira ya kuua maelfu ya waTanzania.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mh.. leo nimeguswa na huyu Tikerra!! ngoja nikajipange lakini ukweli ni kwamba bila TFDA tutalishwa mpaka mavi ya kuku kwenye capsules

  Kwa wale wanaokumbuka tulipotoka miaka ya sabini, tukapita kwa mzaa chiliko hadi tulipo na regulations zilivyokuwa enforced nadhani wanaelewa.

  ....Hivi mnaamini kwamba ni mwananchi ndiye aliye-blow the whistle? Au mnataka TFDA wawe wana magari kama yale ya pollution ya dawasco kwamba leo tunapita mkuranga kuangalia dawa feki?

  Mh... sasa mbona napitiliza?
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  You got sensible argument in there, I thing the TFDA incharge deserve to relinquish authority for this scandal.
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  TFDA wanatakiwa wawe na mchango muhimu zaidi!

  Kwani ni Taasisi ipi Tz utasema kweli ni serious ktk kulinda maslahi ya umma?

  Basi itabidi tufute taasisi zote...angalia hata BoT pesa kibao zilivyopotea za EPA?

  Wanaofanya ktk Taasisi hizi na kuboronga kwao ni reflection yetu sisi wenyewe!
   
 7. B

  Balingilaki Member

  #7
  Apr 4, 2009
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanzania food and drug authority hata isipokuwepo maisha yataenda tu ni chombo ambacho watu ukaa kweny kiyoyozi wakisubiri taarifa za magazeti tena ya nje na simu kutoka kwa watu baki ili wafanye kazi...............chombo hiki kinaiongezea serikali mzigo tu wala hamna lolote
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Tikerra, tatizo si TFDA, baliw atendaji wake wameshindwa kutumia instruments zilizopo kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kikamilifu
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Taasisi zetu za umma zina matatizo gani ya kiutawala? Ni woga wa watu kufanya kazi au kuna nini mana huwa sielewi namna ambavyo hizi taasisi zinafanya kazi.Nyingi haziko proactive.Wanasubiri kitu kitokee ndio waonekane nao wapo. Kwanini karibu kila taasisi ya serikali inaendesha mambo kwa reactive style?
   
Loading...