Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Mh.Samwel John Sitta ni Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Kimamlaka ni kiranja wa Bunge hilo kuhakikisha kuwa Wajumbe wanajadili Rasimu na kuipitisha. Ni kuwaongoza Wajumbe kufikia lengo lao la kuipitisha Rasimu tayari kupigiwa kura na wananchi kuwa Katiba mpya.
Kikanuni na kimamlaka,Mh.Sitta hana nafasi ya kuingiza maoni au mapendekezo yake katika Rasimu iliyopo. Wajibu huo ni wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambao watatenda kazi zao kulingana na Sheria na Kanuni zinazowaongoza ambazo Mh.Sitta anazisimamia.
Leo imeripotiwa kuwa Mh.Sitta amefanya ziara na kufanya mazungumzo ya faragha na Mwadhama Polycap Kardinali Pengo na Sheikh Issa Shaaban Bin Simba.Hawa ni viongozi wa juu wa kidini nchini kwa wakatoliki na waislamu. Nasema,sioni mantiki ya ziara hii.Nina sababu zangu.
Kwanza,kama ni kupokea maoni yao,iliyokuwa Tume ya Jaji Warioba ilikutana nao na kupata maoni yao.Na hakuna aliyebadilisha msimamo wake.Maoni yao yamo kwenye Rasimu iliyopo Bungeni. Kwahiyo,kuwatembelea tena hakuna mshiko.Pili,wao si viiongozi pekee wa kidini nchini.Kuwatembelea wao tu ni kuwatenga wengine na kuibua maneno yasiyo na maana.
Tatu, kuwatembelea viongozi hao na kufanya nao mazungumzo faraghani muda huu wa kujadili Rasimu,ni kuwachora kama wanaoweza kufuatwa,kushawishiwa na kutumiwa kupitisha ajenda mbalimbali za Mh.Sitta au yeyote awaye. Hakukuwa na haja ya ziara kama hii muda kama huu.
Naamini kuwa ziara hii,kama inahusiana na masuala ya Katiba mpya,haina mantiki na haikufaa kuwepo.