Sio vibaya nikiwakumbushia hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio vibaya nikiwakumbushia hii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Nov 5, 2009.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280

  "Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja
  anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa
  ugonjwa huu ni mkubwa,mimi nashauri muwe makini .
  Jitahidini sana kukaa bila kupiga.

  Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si kupiga piga kwani hii
  gharama yake ni kubwa.Kama shida ya kupiga itakuwa kubwa, basi
  hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, na hivi vinapatikana kwa
  wingi na gharama yake si kubwa.

  Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata madhara yanayoweza
  kupatikana
  kutokana na mionzi iliyoko katika simu hizi za kisasa.


  Ni mwiko kabisa kupiga Voda kwa Voda kwani hii ina
  hatari kubwa mno. Pia unashauriwa kutopiga
  tigo kabisa kwani hii inaweza kuharibu kabisa mfumo wa mawasiliano ya simu yako.

  Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna
  hamu angalau ya kupibu, lakini hii nayo ni hatari,
  kwani mwenzako akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi
  sana kwako kuamua kupiga kabisa.

  Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu
  zitamaliza chaji, hii si kweli.Hakikisha tu kwamba
  simcard iko katika hali nzuri,hii ndio ina kumbukumbu
  zote na ndio inaongoza mawasiliano yote.

  Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana.
  Usidanganyike na simu kuwa eti ina Kamera au double
  skrini. Hizo ni mbwembwe tu.Kuna simu nyingi sana feki
  siku hizi zinauzwa zimevishwa cover
  mpya,usidanganyike.

  Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, tafuta sehemu
  inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia
  sana kwani simu ukitumia peke yako inadumu zaidi
  kuliko ile yenye subscribers wengi."
   
Loading...