samnas
Member
- Oct 11, 2015
- 35
- 1
Ochu akiwa na mkewe zuwena wameketi kwenye sofa kubwa baada ya kupata chakula cha mchana, mfanyakazi SADA alikusanya vyombo vilivyokua mezani na kwenda kuviosha, aliwaacha Ochu na zuwena wakiongelea kuhusu mambo ya kifamilia.
''Mke wangu....ni mwaka wa kumi na tatu sasa tangu tumkatae mtoto wetu, na hatujapata tena mtoto miaka yote hii,, tatizo ni nini?'' Aliuliza ochu aliekua hajui tatizo la mkewe kutozaa mtoto tangu walipomtelekeza hashir chini ya daraja,
''Mmh, mme wangu katika koo yetu hamna mtu tasa, mpaka nimezaa tukamtelekeza mtoto wetu yaonesha kabisa sina utasa, sasa sijui tatizo ni nini mme wangu'' alijitetea zuwena aliekua katika mfazaiko mkubwa,, tendo lile la kukitelekeza kichanga chini ya daraja kilimuumiza sana moyoni na kuhisi ametenda dhambi kubwa sana kwa muumba, alijiona mtu dhalili na asie na umuhimu katika jamii, hali ile ya kutopata mimba kwa miaka 13 ilimshtusha sana na kuona kama ni adhabu anapewa na muumba.
''Haiwezekani,, lazima tufanye utafiti hili suala mke wangu,, nina uchu sana wa kupata mrithi , najutia sana kitendo nlichofanya kumkataa mwanangu,, sijui ntaiweka wapi sura yangu mie,,''
''Nahisi uzazi utakua umejifunga...''
''Mmh inawezekana pia, ila wacha kesho tudamkie zahanati tuone nini tatizo..sawa mke wangu?''
''Sawa mume wangu..''
Walikubaliana wawili hao na siku iliyofuata bila kuchelewa walikwenda mpaka kwa dokta hamir huko mjini kariakoo,,walikuta msongamano wa wakina mama na watoto zao, Zuwena alitamani sana na yeye angelibeba mtoto lakini haikua hivyo, ndoto zake zilififia na kupotea, walikwenda mapokezi na kupewa kikadi kilichoandikwa tarakimu ''1027'' na kusubiri mpaka namba hio iitwe. Waliketi kusubiria mpaka ilipoitwa ndipo zuwena huku moyo ukidundaa, alikaribishwa na muuguzi mtanashati aliyeifanya kazi yake vile ilivotakiwa, aliingia na zuwena chumba cha matibabu na kufanyiwa uchunguzi.
Ochu akiwa nje kwenye benchi macho yake yote yalikua mlangoni kwa daktari akitamani auone ukifunguliwa ili ajue nini kimejiri. Zilipita dakika 20 bila zuwena kutoka, hakuchoka kusubiri mpaka pale liposikia namba nyingine ikitajwa. Alinyanyua uso wake na kuangalia mlangoni tena, alimkuta mkewe akija na uso uliojawa na huzuni, mara moja ochu alitambua majibu si mazuri, alimsubiri kwa hamu amsikie nini atamwambia,, alipigwa na butwaa la ajabu na kujikuta akijishika kichwa na kuachia mdomo wazi pale zuwena alipomjibu kuhusu uzazi wake.
''Ati nini?? Uzazi umejifunga?? Hivi kakupima vizuri lakini??''
''Ndio nlimuuliza mara tatu akanipa jibu hilo hilo..'' zuwena alijibu huku macho yake malegevu yakilengwa na machozi
""Aisee?! Sasa tutafanyaje .... Sitaki kuamini kama sitapata mtoto tena''
''Unafikiri tutafanyaje wakati mtoto wako mwenyewe nilomzaa ukamkataa,? Ah mi sjui bana nifanye nini, nshachoka maisha haya kuishi bila ya mtoto!!''
Walipigwa na butwaa wawili hao na kuwafanya wagonjwa wengine waache mambo yao na kutupia masikio yao kwa wanandoa hao wawili.
.
Ochu alikua na mali za kutosha, tabia yake ya ucheshi na uthamini ilimfanya jina lake liweze kujulikana katika mji au jiji la daressalaam, alikua ni mtu wa makamo aliekata mvua 43, uso wake ulionawiri ndevu zilizo chanwa vizuri na rangi yake nyeupe alionekana kama muarabu wa unguja, alitamka kiswahili fasaha kilichowavutia wengi, ni mtu wa maneno na mcheshi, umbo lake lilionesha dhahiri kwamba hakua na shida iliyokua ikimtatiza wakati huo, ni mtu mtanashati na maridadi kwa kujiweka safi muda wote, alioana na zuwena akiwa na umri wa miaka 21 huko tanga muheza mwaka 1992,alipendezwa na uzuri wa zuwena na tabia yake ya upole na wivu. Alijilinda sana na kujikwepa na wanaume wengine mpaka anamaliza elimu yake ya sekondari na kuolewa na bwana ochu hakuwahi kufanya mapenzi au kujenga mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote.
Zuwena aliumbika vizur, ni mwanamke mwenye kuamsha hisia za watu wengi,alivutia sana kwa umbo lake namba nane pamoja na sura yake , ijapokua alikua mweusi lakini si wakuchukiza, weusi wake ulimpendezesha, alipenda ucheshi na ndio maana aliendana sana na bwana ochu, macho yake ya kurembua yalipendwa na wengi na ndiyo aliyomrithisha mtoto wake '' hashir'' , walijutia sana kwa kitendo cha kumtupa hashir chini ya daraja la vingunguti, baada ya zuwena kujifungua,, mzee ochu alimkana hashir kua si mtoto wake kwa sababu hawakufanana, hakufanana na baba wala mama,, hivyo zuwena baada ya kuona amemkera mumewe na hakutaka ndoa yao iharibike, ilim bidi amtelekeze hashir sehemu hyo na kurudi kwa mumewe ,, japo kitendo kile kilimuumiza sana moyoni kila siku, nafsi ilimsuta sana , hakua na la kufanya zaidi ya kumtupia lawama mumewe baada ya kupewa majibu ya kua hataweza kupata mtoto tena, kila alipowaza kitendo alichokifanya miaka 13 nyuma aliumia sana mpaka kutokwa machozi, hakuona raha ya kuishi tena na aliona dunia imemuelemea, mungu sasa anamuadhibu baada ya kufanya kosa kubwa..
..
..
..
..nini kingetokea baada ya familia hio kukosa muelekeo? Usikose kufatilia riwaya hii ya kusisimua sehemu ya #6