samnas
Member
- Oct 11, 2015
- 35
- 1
Hakujua amwambie nini mwalimu ili aweze kumruhusu aingie ndani na kujiunga na wenzake ili wasome. Mwalimu mashaka alijulikana shuleni hapo kwa ukali na tabia yake ya kuwaonea watoto wa kiume na kupendelea wa kike. Kiukweli alichukiwa na watu wengi shuleni hapo, alitamani sana mtoto wake ''SUMA'' aongoze katika somo la hisabati ambalo alikua akilifundisha ilhali mwanawe huyo hakua na utayari wa kuliweza somo hilo. Hashir mtoto asie na bahati alichukiwa na mwalimu huyo kwasababu tu ya kumpita mtoto wake, mara zote hashir alichukua nafasi ya kwanza kwenye somo hilo na masomo mengine mengi huku Suma akiambulia kushika mkia.
Mikunjo ya uso ilidhihirika kwenye paji la uso, jasho la hasira lilionekana likishuka kutoka utosini mwa mwalimu Mashaka, Macho yake yaliokithiri wekundu kwa kukasirika kila mara yaliwafanya wanafunzi kumtunga jina la utani na kumuita ''Teja msomi''.
Haikua rahisi kumtambua ni muda gani ana furaha, muda wote aliikunja sura na kufanya mikunjo idhihirike kwenye paji lake la uso, pua yake pana iliyojawa na majasho muda wote ilirowesha sharubu zake zilizomfanya aonekane kama wakoloni wa zamani.
Alikua na midomo mipana aliyowacha wazi na kudhihirisha meno yake yasioyokua na mpangilio vizuri, mwili wake mwembamba na uvaaji wake kulimfanya aonekane tofauti na walimu wengine katika shule hio ya serikali ya HEKIMA.
Ilimbidi Hashir atulie na kusubiri hukumu yake kama vile mtuhumiwa akiwa mahakamani siku ya hukumu. Sura yake ya upole na woga vilimfanya achekwe na wenzake shuleni hapo huku wanafunzi wenzake wakimuongelea, wakimcheka na kumuoneshea ishara ya viboko.
Hashir hakupendezwa na tabia hio, alijikuta akitokwa na machozi na kutamani kuomba msamaha. Mwalimu mashaka hakua na roho ya huruma hata kidogo, angekua ni mtu mwenye madaraka ya juu basi kutoa roho ya mtu kwake isingekua taabu ili kuzidisha kipato na kua kiongoz wa juu zaidi.
Mpaka kipindi cha hisabati kinaisha saa nne kasoro mwalimu mashaka hakumruhusu hashir aingie ndani. na alipomaliza kipindi chake, kwa jazba na hasiraa za hali ya juu alifungua mlango na kumuangalia hashir aliekua bado kapiga magoti,,na kumfokea pamoja na kumpa matusi ya nguoni
'' wewe mbwa, kwann umecherewa?? Si nakuuliza wewe? Huna jibu eenh? Nyan'gau mkubwa wewe, sasa utantambua mimi nani...twende huku pumbav wewe'' (huku akimburuza mithli ya gunia la viazi alimpeleka mpaka ofisini kwake) hashir alilia sana na kusononeka moyoni mwake, hakujua hatma ya maisha yake na kwanini kila siku ni yeye anayekumbwa na matatizo, je Mungu hakusikia kilio cha mtoto huyu? Nani angejitolea kumsaidia kwa hali na mali ili aweze kupata maisha bora,,aliteseka sana hashir bila kujua lini mateso hayo yatafikia ukingoni.alilalamika sana hashir na kujiona mtu aliekosa bahati kwa kupatwa na matatizo kila siku.
''Muachee!! Muachee!! We mtu gani usiekua na huruma? Muache nimesema muachee!! Kwani nani anakuogopaa?..'' ''roho mbaya huyooo''
''Huna hadhi ya kuitwa mwalimu wewee!!''
Zilisikika sauti kwa wanafunzi wa shule hiyo, kabla mwalimu mashaka hajafika ofisini tayari alishazungukwa na kundi kubwa sana la wanafunzi pamoja na walimu, wakimfokea kwa unyama anaoufanya. Mwalimu mashaka alichukia sana na kujikuta akimzabua makofi hashir huku akimpiga mateke mithli ya mnyama. Kitendo hiki kiliwagusa wengi sana hasa rafiki kipenzi wa hashir, ''CHIDY'', hakua nyuma kumuona rafiki yake kipenzi akionewa, alijikaza kiume na kujitoa kimaso maso bila kujali mtu yoyote wala kuogopa chochote. Kwa nguvu zote aliokota jiwe la saiz na kumrushia nalo mwalimu mashaka bila ya huruma. ""PAAAAAA!!"" ""Yalaaaaaa!!...'' Ilisikika sauti ya mwalimu mashaka akiugulia kwa uchungu sana huku damu zikim bubujika kichwani na kupoteza fahamu....kwa mbaali alionekana mwalimu mkuu akitokelezea akiwa na sura ya hofu na wasi wasi umemtanda kichwani, alitaka kujua nini kimejiri..
'' eenhee,, kuna nini tena hapa?? Aliuliza mkuu
..
..
..je unataka kujua nini kiliendelea? Usikose kufatilia riwaya hii ya kusisimua sehemu ya #4