Sio kila Mhaya ana dharau

Sio kila Mhaya ana dharau

muttamwombe

Member
Joined
Jul 28, 2014
Posts
98
Reaction score
62
Naandika hivi nikiwa na masikitiko makubwa sana juu ya ukabila unaoota mizizi hasa katika kipindi cha hvi karibuni ndani ya nchi yetu! Hivi karibuni aliyekuwa Waziri wa nyumba na makazi mama Tibaijuika alikaririwa akisema MILIONI KUMI NI KWA AJILI YA MBOGA!

Kwa kweli hii ni dharau kubwa sana; lakini hoja yangu ni kuhusu maneno yanayoendelea kwenye mitandao mbalimbali ikiwahusisha wahaya wote na huyu MTU! Kimsingi hili jambo linanikera sana maana ni kuendekeza ukabila na ubaguzi kwani mtu mmoja hawezi kuwa KIGEZO cha kuwaamulika watu wote wa jamii husika!

Bila shaka ninyi ni mashahidi juu ya kauli nyingi zilizowahi kutolewa na watu wa aina mbalimbali hasa viongozi lakini hazikuhusishwa na ukabila! Tafadhali epukeni ukabila kwani ulileta madhara makubwa Rwanda & Burundi pamoja na Kenya! Ni hayo tu kwa Leo..
 
attachment.php
 

Attachments

  • 1425079816063.jpg
    1425079816063.jpg
    81.4 KB · Views: 8,204
Ndio maana naendelea kusema kuwa ukiona unambagua binadamu mwenzako kwa kigezo cha ukabila au udini ujue hauna tofauti na wale wanaowabagua wenye ngozi tofauti wakati binadamu wote ni sawa! Kila binadamu ana mapungufu yake na unapochukua mapungufu ya mtu mmoja ukayajumlisha kuwa ya jamiii anakotoka huo ni ubaguzi wa hali ya juu! Naandika hivi nikijua kuwa kuna taasisi nyingi sana na nyeti hapa Nchini na nje ya nchi zinashikiliwa na wahaya na zinafanya vizuri...mbona hayo hamyaoni?
 
Back
Top Bottom