Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 21,978
- 57,746
1. Kuna mtu ananunua simu ya gharama ili wamuone na siyo kuwasiliana.
2. Kuna mtu anatembelea gari la kifahari ili wamuone na siyo kurahisisha usafiri.
3. Kuna mtu anajenga nyumba ya fahari ili wamuone na siyo kuishi!
4. Kuna mtu ananunua nguo za gharama ili wamuone na siyo kujisitiri!
5. Kuna mtu anavaa saa ya gharama ili wamuone na siyo kutunza muda!
6. Kuna mtu anasafiri kwa ndege ili wamuone na siyo kufika anakokwenda!
7. Kuna mtu akishika pesa anataka kila mtu amuone na siyo kwa matumizi. Huyu atapiga picha na kusambaza.
8. Kuna mtu akila chakula kizuri atataka wamuone na siyo kushiba. Huyu atapiga picha na kusambaza!
9. Hizi tabia za kutaka kuonekana onekana ndizo hufanya watu wengi kuwa wabinafsi!
10. Mtu anamiliki nyumba 100 na wakati kuna ndugu zake wa damu wanaishi maisha magumu kama mfupa!
11. Mtu anatembelea gari la mabilioni ya shilingi na wakati jirani zake jana wamelala njaa na hawana uhakika kama leo watakula!
12. Tabia za kutaka kuoneokana onekana zimefanya dunia iwe mahali hatari sana kwa binadamu kuishi!
13. Mwenye kidogo hana amani, mwenye kingi hana amani!
14. Mwenye kidogo hana amani kwa sababu hata hicho kidogo akizubaa atanyang'anywa na huyo mwenye kingi!
15. Mwenye kingi hana amani kwa sababu muda wote anaogopa kukabwa na mwenye kidogo!
16. Dunia itakuwa salama pale mwenye kidogo na mwenye kingi watakapokaa pamoja na kutafuta namna ya mwenye kidogo naye kuwa na kingi na siyo mwenye kingi awe na kidogo!
Credit : Dennis Mpagaze