Sio katika kila mafanikio ya Mwanaume, Mwanamke yupo nyuma yake

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Sio kila Mwanaume aliyafanikiwa kimaisha basi Mwanamke yupo nyuma yake. Kuna Wanaume wanapitia kipindi kigumu sana kuyafikia mafanikio na wapo na Wanawake zao

Unakuta Mwanamke huna muda na huyo Mwanaume wake wa kumfariji na kumtia moyo. Kutwa kucha kumsimamga, kumsema vibaya eti masikini na inafikia hatua Mwanamke huyo anakukimbia hata kama umezaa nae watoto kisa tu hujafanikiwa kimaendeleo

Sasa kwa muktadha huu wa kusimangwa na Mwanamke wako kisa huna hela siku ukizipata utasema mafanikio yako yapo nyuma ya huyo Mwanamke wakati kila siku alikua anakupa stress tu kwa gubu, kejeli na masimango mengine

Utasema mafanikio yako yapo nyuma ya Mwanamke wako endapo alikua pamoja na wewe katika magumu uliyokua unapitia Yani anakufariji, kukutia Moyo, kama huna kazi nae ana kazi basi anakupa mtaji hata kwa kukukopesha

Hapa ukifanikiwa utasema kabisa mafanikio haya yamechangiwa na Moyo wa huruma na upendo wa mke wangu

Ila sio Hawa wanawake wa siku hizi ni mabingwa wa kuturudisha nyuma kimaendeleo na wengi hawapo pamoja nasi katika kuyatafuta maendeleo

Bora ukosee kujenga ,kuliko kukosea kuoa utapata tabu Sana
 
inawezekana mwanamke anayezungumziwa huwa sio mwingine tofauti na mama!
ronaldo7rl-20191026-0001.jpeg
 
Sasa wewe nani unapingana na ukweli?


1. Nakukuta kapuku, nakupa assist ya aina yoyote ile, unatusua.

2. Nakukuta kapuku, nakustresisha hadi akili inakukaa sawa, ikibidi nakuacha kabisa, unapata hasira, akili zinaamka ulikozisahau, una'haso', unatusua.


3. Nakuzaa, nakulea, nakusomesha, unapata kazi nzuri/unafanya biashara kubwa, unatusua.


1,2 & 3 zote ni mafanikio ambayo mwanamke yuko nyuma yake.
 
Ila Mama lazima awe nyuma yako.. hii sio ombi ni lazima.
Kwa lolote lile utafanikiwa kwakua nyuma kulikua au yupo mama (Mama ni mwanamke pia)
Nilitaka kuuliza, kwamba, mtu anaweza kufanikiwa bila ya kuzaliwa na mama?

Yani usijali kama mama kalea au kafariki akizaa au katelekeza mtoto.

Ukishazaliwa na mama tu, mafanikio yoyote utakayopata kuna mwanamke angalau mmoja, mama, kachangia.

Angeweza kufanya abortion usizaliwe kabisa.

Hayo mafanikio yangetokea vipi?
 
Atoto,
Ni kweli lakini huyu mwanamke uliyemsemea hapa ni yule aliye ongea na shetani pale bustanini SIO YULE ALIYETAKIWA AWE MSAIDIZI.
 
kufanikiwa ni nini ? Ukijibu maana ya kufanikiwa hautakuwa na ukakasi kwenye hii sentensi,,,

Pili huyo aliyesimangwa ni mawili either asingesimangwa asingepata usongo wa kufanya alichokifanya (prove them wrong) au angepata partner mzuri angepata mafanikio zaidi...

Success is not a how far you got, but the distance you traveled to get there....
 
Tatizo umeoa kwa kuangalia shape na sura instead of smart brain hayo magubu sijui makitu gani mengine lazima yakupate pengine hata zaid na cheating lazima ufanyiwe maana mke anataka amaintain status yake kwa mashosti, pochi kaliii simu ya maana, mafanikio utayasikia kwa kwenzio tu
 
Back
Top Bottom