Sio dhambi kuungwa mkono na CCM - Kansa Mbarouk

Sio dhambi kuungwa mkono na CCM - Kansa Mbarouk

Mgombea Uenyekiti CHADEMA Kansa Mbarouk amelalamikia wafuasi wa chama hicho wanaosema hafai kuchaguliwa kwa sababu anashabikiwa na CCM.

Katika mahojiano na gazeti la FAHAMU mgombea huyo amesema haoni dhambi kupendwa na mashabiki wa CCM kwani hiyo ndiyo demokrasia.

Mgombea huyo anayeshutumiwa kuwa kibaraka wa CCM amewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema kumchagua kwa sababu ndiye anayefaa.

Uchaguzi mkuu wa Chadema unafanyika Septemba 14 ambapo Kansa Mbarouk anashindana na Freeman Mbowe Mwenyekiti anayemaliza muda wake na akitarajiwa kutetea nafasi yake kwa ushindi wa kishindo.

Huyu Kansa ataangukia pua na kuaibika vibaya sana. Baadae ndo ataelewa kutanguliza tumbo kwenye ishu muhimu ni kununua dharau kwa bei rahisi
 
Kuna wakati wowote ule ambao Mbowe alimwambia Zito asigombee? Acha umbea, Zito alishauriwa na Baraza la Wadhamini. Hakuzuiwa bali alishauriwa. Hakuzuiwa na Mbowe wala kushauriwa na Mbowe.

Mbowe kaweka kibaraka agombee mbona alimuogopa Zitto Kabwe?
 
Kwa hiyo ccm watampigia kura?
 
Mbowe kaweka kibaraka agombee mbona alimuogopa Zitto Kabwe?

Mbowe amwogope Zitto? Sasa mbona kaongoza kikao cha kumfukuzilia mbali? Mbowe huyu aliyemfuga Zitto tangu hajulikani hata na mjumbe wake wa nyumba kumi leo amwogope? Wewe Faiza unamwogopa mbwa uliyemfuga mwenyewe?
 
Kushabikiwa na CCM siyo dhambi ila kushabikiwa na CCM ni kifo.
 
Huyu Kansa ataangukia pua na kuaibika vibaya sana. Baadae ndo ataelewa kutanguliza tumbo kwenye ishu muhimu ni kununua dharau kwa bei rahisi

Anadhani kugombea na Mbowe ni kupata umaarufu wa bure.
 
Kuna wakati wowote ule ambao Mbowe alimwambia Zito asigombee? Acha umbea, Zito alishauriwa na Baraza la Wadhamini. Hakuzuiwa bali alishauriwa. Hakuzuiwa na Mbowe wala kushauriwa na Mbowe.

Ni kweli Mkuu.Mbowe hajawahi kumzuia kijana Zitto kugombea.Mbowe mara zote anaalika watu wa kujipima naye ili wakue kisiasa.
 
Kwa hiyo ccm watampigia kura?

Uko sahihi mkuu.

Huyu Kansa kila siku anaombewa kura na magazeti ya CCM ya Uhuru,Mzalendo,JambaLeo na HabariLeo.Pia Televisheni ya CCM TBC wanampigia debe eti amuondoe Mbowe.
 
Yaani anataka kuwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani halafu anaungwa mkono na chama kilicho madarakani?!
Huyu jamaa ndio pimbi kweli.
 
Anadhani kugombea na Mbowe ni kupata umaarufu wa bure.

Jamaa amechungulia fursa! Ameona hawezi kushinda hata nafasi moja kwenye chaguzi za ndani ya chadema akaamua kwenda kupiga hela za wajinga in the name of "mpinzani wa Mbowe!"
 
Mbowe amwogope Zitto? Sasa mbona kaongoza kikao cha kumfukuzilia mbali? Mbowe huyu aliyemfuga Zitto tangu hajulikani hata na mjumbe wake wa nyumba kumi leo amwogope? Wewe Faiza unamwogopa mbwa uliyemfuga mwenyewe?

Mkuu niongeze kidogo kwenye uliyoandika...

Hata kubaki kwenye chama mpaka mwaka huu ilikuwa ni huruma ya Mbowe tu.Mara nyingi Mbowe alikuwa anamuombea msamaha kwenye vikao vya juu akidhani huyu dogo angebadilika kumbe ukishaanza usaliti huachi ni kama kula nyama ya mtu.
 
Jamaa amechungulia fursa! Ameona hawezi kushinda hata nafasi moja kwenye chaguzi za ndani ya chadema akaamua kwenda kupiga hela za wajinga in the name of "mpinzani wa Mbowe!"

Ni kweli kabisa usemayo Kamanda
 
Back
Top Bottom