Sinywi pombe tena!

Shukuru

JF-Expert Member
Sep 3, 2007
748
15
Jamaa mmoja alikuwa na desturi ya kwenda baa na rafiki yake kwa kipindi kirefu, kwa bahati mbaya rafiki yake huyu alifariki dunia. Jamaa akawa kila akienda baa anaagiza bia mbili na glass mbili, kisha anamimina kila bia kwenye glass yake, halafu anakunywa huku na huku mpaka zote zinaishia kwa kupishana fundo moja, kisha anaagiza zingine tena mpaka atosheke kwa staili hiyo hiyo.

Mhudumu aliyekuwa anamhudumia akawa anapata maswali mengi juu ya tabia ya mteja wake huyu mkongwe. Baada ya kusubiri sana, siku moja yule jamaa allikuja na kuagiza bia moja na glass moja, ilipoisha akaagiza bia moja nyingine. Yule mhudumu akashangaa na kuamua kutoa dukuduku lake moyoni, akamuuliza kuwa kipindi cha nyuma ulikuwa unaagiza bia mbili kwa mpigo vipi leo unaagiza bia moja moja? Jamaa kwa masikitiko makubwa akasema;

"nililkuwa na rafiki yangu tukiwa tukinywa bia pamoja kila siku, mwaka jana rafiki yangu alifariki, na muda wote huo nilikuwa naagiza bia mbili, yangu moja na nyingine ya rafiki yangu kwa kumuenzi, sasa kuanzia leo nimeamua kuacha kunywa pombe kwani nyumbani mke amezidisha malalamiko, ila hii ni kwa ajili ya huyo rafiki yangu maana sijui kama yeye angeamua kuacha kama mimi...."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom